Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

Dalali si sawa na agent sababu.

Agent sio mbabaishaji.

Labda msajiriwe mnaweza kukaa sawa sasa.
 
Mkuu wewe muoga mno.
Yaani mjini hapa mtu anitishe kiasi hiko?
Halafu napendaga ligi za hivyo.
Unkinidindishia ndo nafanya kusudi.

Bora uje kistaarabu tukae mezani naweza walau kukupa hela ya serengeti 4.
Ila vitisho mhh
Hiyo imetokea juzi dalali mwenzangu ameonyeshwa nyumba na dalali mwengine dalali mm nikipata mteja hapa JF nikampgie yule dalali mwenzangu ambaye nafanya naye kazi tukauza nyumba tunagawana mtu bee.

Mteja alivyolipia nyumba akunitafuta tena kunijulisha kwamba amefanikisha maana mm nikipata mteja nampgia agent (jamaangu) anaenda kuuza nyumba harafu usiku tunakutana bar kufanya mgawo kifupi tunaaminiana sana.

Ss yule dalali wa 3 tuliyemzunguka na aliyemuonyesha mshikaji nyumba akapeleka mteja anakuta Mali ishauzwa akapagawa akaanza msako kwa madalali akupata jibu ikabidi amtaiti amdai mteja ,mteja ikabidi anipigie mm ,hapo ikabidi niende kuongea na madalali wenzangu akiwamo yule tuliyemzunguka,kumbe kihistoria aluwahi kutuzunguka xo kesi ikaishia hapo tukampiga Castle Lite with a bite mbili akatulia ila vinginevyo mteja angelipa hela ya udalali mara mbili.
 
Dalali si sawa na agent sababu.

Agent sio mbabaishaji.

Labda msajiriwe mnaweza kukaa sawa sasa.
Watu tumesajiriwa babu tupo kiofisi zaidi,japo kwenye msafara wa mamba na kenge wapo pia,hata madokta feki,na ma engineer feki wasiopitia ERB wapo pia ndio hao wanaangusha magorofa na madaraja kila day.
 
Miaka flan nyuma huko nliingia kwenye udalali sasa nikapata mteja wa Costa hiz bus nikamtoa mkoa tukaingia mjin DSM tukapata Costa nikaweka changu cha juu kama 4m jamaa mwenye gari akakubali sababu alkua anauza 18m mie nikamwambia jamaa 22m kimbembe kikaanza jamaa mwenye gar kwao n bagamoyo akasema hzo hela nataka cash Mambo ya benk sitaki hvyo tukamlipie bagamoyo.

Kwenye kuandikishana tukaenda mahakamani tukamkuta mmama mmoja hv maneno mengi nikamwambia kwenye hii pesa ya mauziano Sheria inataka mahakama ichukue 5% ya mauzo ila mie sikuzibii rizki nikamwambia mwenye gar na mnunuz walipe 10% kila mmoja na wote waliridhia tena bila risit ya mahakama sasa yule mama akaambiwa huyu jamaa ana 4m yake hii gar nauza 18m yule hakim nlimuona mjinga eti akawaita wale jamaa pamoja akawachana wasinipe kitu ndo ikawa mwanxo was kukosa 4m yangu nlioitafuta huku na kule kwa mbinde kuzunguka mikoa ila hakujua mie na mnunuz tunarud pamoja mpaka gar ifike mkoa Zaid ya 1000km ndo anipe changu.

Tukaenda bank tukatoa pesa tukampa jamaa tena nimemkumbuka jina huyo jamaa anaitwa Dharau ni maarufu Sana bagamoyo, Sasa kusubir ile 4m ndo hola piga simu not reachable mpaka tukaenda mkoa hola japo nashukuru jamaa alinitoa tulichikubaliana sasa nikaanza kuuchukia udalali kwa hasira sana.

Tokea siku hyo nikiwa na inshu ya kukutana na dalali nampa condition ya hitaji langu akilitimiza namwambia sikupi hiyo hela unayotaka nakupa 20k ikizid Sana 50k akikataa namwambia basi poa mie nafanya ninavyojua nakutana na mwenye Mali nampa chake napewa funguo mchexo umeisha.

Shida ya udalali Wana chain ndefu ya kijinga yan wanataka uwalee Kama wanawake Kama wapo kumi wote uwaridhishe
 

Kwa kweli Mr. dalali muwatishe hao hao wa huko mimi hamnipati ng’oo, na huwa nikisema hunifanyi kitu namaanisha hunifanyi kitu kweli!

Kuna lugha ya mazungumzo ya biashara kwamba sina hii pokea hii, unakomaa unataka kodi ya mwezi unanisaidia kutafuta hela? Sio kila nyumba utaingia utamkuta mteja wako anazunguka na taulo, Mmezoeshwa vibaya mno!
 
Nimewaza hiyo kutoka chooni na kitaulo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
Ukutane na mwenye nyumba Mbea...
Unamfuata kimya kimya muyamalize..

Anamtonya dalalii..
"mtu wako yupo hapa anakuzunguka"...
Bongo kuna mambo yamekaa kikatuni katuni, ila ni watu ndio wanayafanya.
kikatun katun[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dea leo umeamua khaaaaaah mbavu zangu mieee, hyo taulo kuelekea maliwatoni, uwiiiiiiiiiiiiiiih
 
[emoji23][emoji23][emoji23]unatoboa tket afu unaivaa shngon
 
Si ushalipwa elfu kumi ya kumpeleka kwa mwenye mali (nyumba/kiwanja/etc) tatizo lako nini?

Wewe mwenyewe hauko kisheria. Hata pesa ya mwezi mmoja haiko kisheria. Acha tamaa na ridhika na buku teni uliyopewa.
 
Kuna zile aina za mikataba Kama umeenda shule ww utakuwa unaelewa kwamba Kuna kitu inaitwa" verbal contract",makubaliano ya mdomo .Unarakiwa ukubaliane kabla haujaonyeshwa nyumba,ila km dalali mmekubaliana malipo ya kodi ya mwezi harafu hautaki kumpa hapo ss ww unaingia kwny kundi la matapeli dada .
 
"vinginevyo mteja angelipa hela ya udalali mara mbili."

huyo mteja labda kama kaingia mjin na nguo kwny rambo ndo atalipa mara mbili.
 

Kuna tatizo gani tapeli akimtapeli tapeli?
 
Mkuu July NBA INARUDI TENA KARIBU TENA, Back to topic, Kazi ya udalali ni kama kazi nyingine ambayo ni rasmi na ina sheria ambazo zinaongoza shughuli hii. Madalali wengi wa mijini hawajasajiliwa na mamlaka za Serikali na hawatambuliki shughuli hiyo wanayoifanya. Wengi wanafanya kwa mazoea tu na si watu ambao unaweza kujua wapi wanapatikana kwani hata ofisi hawana, ni watu wa vijiweni. Ni muhimu sana kwa mteja au mmiliki kutafuta madalali ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria ili yanapojitokeza matatizo yanayohusiana na shughuli yake ya udalali unayo haki ya kisheria dhidi yake. Kama dalali hajasajiliwa shughuli yake ni batili kisheria na hatakama akikushauri kimakosa na kupata hasara ni vigumo kwako kumchukulia hatua za kisheria.
 
Mkuu tukubaliane jambo moja kwamba, Kwa Maelezo yako hapo juu yanaweza yakawa ni makubaliano tu na sio mkataba. Ili Ijulikane ya kwamba mikataba yote ni makubaliano ila sio makubaliano yote ni mikataba isipokuwa yamekidhi vigezo vya kimkataba. Vigezo hivyo vimewekwa na sharia ya mikataba ya Tanzania kwa jina la The Law of Contract Act, [R.E 2002]. Kwenye kifungu cha 10 cha sheria hiyo kinataja baadhi ya vigezo ambayo ni lazima yawepo kwenye makubaliano fulani ili yaweze kuwa mkataba. Vigezo hivyo ni kama vile lazima kuwe na makubaliano huru baina ya pande zinazohusika katika mkataba. Na makubaliano hayo hayapaswi kufikiwa kwa kushawishiwa na rushwa, kulazimishwa au nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…