Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Swali zuri,Tupo.
Ni upuuzi kuita ndoa feki kisa mtu kaja na uhitaji, hiyo ndio ndoa yenyewe. Kwenye ndoa kinachotupeleka ni mahitaji aidha ya kimwili, kiuchumi, kijamii au kiroho.
Sasa kama mwanaume unaita ndoa feki kisa mke kaja kufata mahitaji naomba uniambie ulitaka afuate nini? Au kigezo chako cha ndoa isiyo feki ni kipi??
Tunachotaka sie wanaume wengi ni kuwa mwanamke akiwa na sisi kwenye ndoa, kitu cha kwanza kinachotakiwa kiwe kimemleta ni kuwa anatakiwa awe amevutiwa na muonekano wetu wa nje k.v urefu, sura, rangi, yani kwa kifupi mwanamke awe na hisia na sisi, kama ni huduma za kipesa kwa ke mwanaume anaejielewa atatoa tu.
Shida ni kuwa mwanamke anakuwa hana hisia na mwanaume, ila anakuwa Yuko na mwanaume sababu ya hela tu, hiyo kitu ndo inatuuma sisi wanaume, ndo maana tunaiita ndoa feki. Zurie