Maisha yako ya Ndoa yamekuwaje baada ya kutofanikiwa kuoa/kuolewa na 'your dream man/woman?

Maisha yako ya Ndoa yamekuwaje baada ya kutofanikiwa kuoa/kuolewa na 'your dream man/woman?

Maisha ya ndoa hayana copy&paste kila mtu ana namna anaishi maisha yake na anayafurahia na kero nitakazozipata mimi siyo atakazozipata mwenzangu.

Nina ndoa ya miaka tisa with three kids namshukuru Mungu ungeniuliza hili swali siku ile ya ndoa ndugu wanashangilia nimeowa huku mimi kichwani nimejaa woga na mawazo hakika ningesema tofauti ila matarajio na ninachokiona ni tofauti,vijana oweni nakuhakikishieni oweni!
Shukrani sana Saint Anno kwa ushauri mzuri, ubarikiwe wewe na familia yako..!!
 
Yule ana mbwela mbwela shauri yake atafika stage ya kutaka anaye pumua🤣🤣🤣🤣
Kuna wawili nimempatia namwambia wikend niwalete visingizo kibao mara mitihani ya cpa sijui nini....kusoma hakuna mwisho
Haha..
Hivyo wataka kusema yeye ndiye anazingua..!!?
 
haha thats where a problem is, mfano mimi nina expirience sana na mahusiano ya wakati huu na still bado mdogo tu ila hamna kitu kinanitatiza kama likija suala la wapi au ni nani ni sahihi kwangu.... Sihitaji kufanya mistake tena round hii, Nimetuliza ball namuomba tu Mungu wangu.
Ili ujibiwe kiukweli unapaswa nawe uwe umetuli haswa, siyo unaendelea kuruka ruka and you're here praying,
 
Mtazamo wangu unaendana na law of attraction. Naamini kuwa kila mtu hua kuna aina ya mtu anayotaka kuspend lifetime nae. Lakini pia wengi wanakosea hapa kwa kuweka mtu specific kbsa, lets say mtu anasema kbsa mimi namtaka Carleen ndo awe mwenzi wangu. Nothing is free hii dunia. So, kwangu mimi naamini kua you have to put up the qualities zooote unazotaka kwa mwenzi wako, then hapo ndo kazi inapoanzia. Kazi yenyewe ni moja, kuhakikisha kua mtu mwenye quality hizo zote akubali kuwa na mtu kama wewe. So hapo u have to work kuhakikisha wewe pia una qualities hizo zote, na hapo ndo unaeza kukutana na mtu mnaeendana. Na pia hata changamoto mkikutana nazo ni rahisi kuzitatua
Ukitulia you're smart enough ila mpaka utulie tumekoma..!
I like that one, kuna kitu muhimu umeniongezea sana.!!
 
sijutii naifurahia sana familia yangu...japo siku tegemea kama itakuwa ya furaha kwani mimi kabla sijawa na mtoto nilikuwa na principle yangu kuwa sitaki kabisa mtoto wangu akose malezi ya wazazi wawili...na sikuwa napenda nione mwanangu analelewa na baba mwingine hali ya kuwa baba yake nipo....hivyo huyu baby mama alipo pata mimba nikawa na uhakika kuwa ni yangu nikasema liwalo na liwe siwezi kuacha mwanangu alelewe na baba mwingine na mimi baba yake ningalipo...nikaoa kishingo upande...the last is story naifurahia familia yangu ya baba, mama na mtoto mmoja...na tunajipanga kuongeza mtoto mwingine...​
Woooow'...!
What a beautiful testimony..!
Mungu azidi kuwatunza Prince..! Muendelee kupendana na kuwa na furaha daima..! Ameen.!
 
Haha.
Naomba uzoefu wako crush tafadhali..!

pexels-yan-krukov-8197497.jpeg


Bado najaribu ku-decode the meaning behind huu mjadala. Kichwa kimewaka moto ngoja nikiweke kwenye maji ya baridi kwanza
 
Nimeandika kulingana na research niliyowahi kuifanya.

Kuna wakati nilikuwa na shauku ya kutaka kufahamu maswali kama haya uliyoyauliza, nikatenga muda kuchunguza baadhi ya ndoa za watu wa karibu.

Katika hizo ndoa wapo ambao wameamua kujifunza kupendana (conclusion yangu imetokea hapa)
Uko sahihi kwenye hili, vijana wengi wa zamani miaka 70's-89' walichaguliwa wake na Wazee wao lakini waliweza kujifunza kupendana na wakaweza, kutokea hapo wakaanza kuishi Kwa Amani na upendo miaka na miaka wakihesabu anniversary za 25,30,45 pamoja.

Kitu ambacho wengi hawajui ni kuwa ukikaa na mtu Kwa muda mrefu unamzoea na kumpenda.

Na hakuna kitu Kinafanya Ke/Me wapendane kama kula Msosi pamoja.
 
Back
Top Bottom