Majaliwa asema CCM kumpeleka kwa wananchi Rais Samia 2025

Ni kikao kilichopitisha hayo maamuzi ya hivyo.
 
Badala ya kufanya kazi wamekalia kampeni, CCM ni janga ndani ya nchi hii na maendeleo ya kweli tutaendelea kuyasikia kwa wengine tu, maana viongozi muda wote wanapambana kubaki madarakani
 
Hawana kazi hadi kuwaza kuhusu uchaguzi wa 2025!!
 
Hii sasa ni kufuru!.. Uchaguzi tumefanya miezi kumi iliyopita, Mpaka October 2025 kuna miaka minne kamili. Badala ya kuwaza namna ya kushughulikia kilichomo kwenye ilani iliyonadiwa na ahadi zilizotolewa, tunapenyezewa nyeti za nani atakayesimama kugombea?. Kampeni zimeanza mapema? 🤔 😳
 
Wanashinda insta na warembo wao na mavazi yao ya ajabu,utadhani ni wa bongo movie!
 
Tumuombe Mwenyezimungu atujaalie uzima hiyo 2025.
Na kama CHADEMA wakimuweka Mh. Mbowe unadhani mtanange utakuwa vipi..? (Free and Fair uchaguzi)
 
Hivi Majaliwa ni nani huko Ccm?? Maana naona ana vuka mipaka yake ya utawala..
 

Kuuliza si ujinga, Majaliwa asema CCM itampeleka samia kwa wananchi. Nani au kikao kipi kimekutuma useme hayo? Mwenza wa Rais haonekani, hasemi ,hajulikani aliko , wewe umetumwa na nani?​

 
Huyo mama akigombea sihangaiki kupiga kura yangu maana nitakuwa nimeinajisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…