Majaliwa asema CCM kumpeleka kwa wananchi Rais Samia 2025

Hii sasa ni kufuru!.. Uchaguzi tumefanya miezi kumi iliyopita, Mpaka October 2025 kuna miaka minne kamili. Badala ya kuwaza namna ya kushughulikia kilichomo kwenye ilani iliyonadiwa na ahadi zilizotolewa, tunapenyezewa nyeti za nani atakayesimama kugombea?. Kampeni zimeanza mapema? [emoji848] 😳

Ukweli ni kuwa kuna watu walikua wanajipanga hiyo 2025, miongoni mwao ni hao mawaziri. Kifo cha Rais JPM kwa kiasi fulani kimeharibu hizo program zao. Ni muhimu sana kwa Waziri Mkuu kuweka msimamo wa serikali na Chama chao bayana. Otherwise, vikumbo vikianza shughuri za umma hazitakiwa na ufanisi.
 
Rais Samia kampa madaraka Majaliwa, na awamu hii atafanya kazi ya maana. Alikuwa akimuogopa JPM kwani hakutabirika.

Samia anatabirika na anayo huruma ya Mama mzazi, anao uwezo wa kupima kinachofanyika na kuja na jawabu linaloangalia utendaji wa haki.
Nadhani anaweza kuwa waziri mkuu wa kwanza kutoboa miaka 15, ila urais 2015 sidhani, January ni tishio kwao wote, may be limtokee janga la kisiasa in between
 
daah!! naona Kama historia huenda ikabadilika ktk taifa hili,baada ya miaka zaidi 50,nahisi Kama huenda utawala ukaangukia kwa bendela nyngne na sio hii ya kijani.utani tu jamani!
 
Nadhani anaweza kuwa waziri mkuu wa kwanza kutoboa miaka 15, ila urais 2015 sidhani, January ni tishio kwao wote, may be limtokee janga la kisiasa in between
January anaweza kuwa rais kama Mama itatokea akashindwa kugombea. Mama kampa cheo January ili kulivuta kwake kundi lake la CCM na sio vinginevyo.
 
Nilikosea hapo, January anaweza kuchukua 2030 kama akitulia hii miaka iliyobaki! Mpinzani wake mkubwa ni H. Mwinyi akiamua kugombea
 
Mkuu siyo CCM tu, leo hii Mwamba akiibuka na msimamo wowote huko kwenu kuna mtu wa kumpinga? Muhimu tuiombee nchi yetu mema while tunakosoana ndani kwa ndani, nimependa aproach ya CDM kutaka kuongea na Rais, naye kama ana akili akae aongee nao
Mkuu mwamba ni mtu anaeshaurika, anaesikiliza , anaetatua, kwetu CHADEMA tamko lolote likitolewa na kiongozi kuanzia taifa , mpaka kwenye Kanda jua limepitia vikao rasmi,unaendeshaje chama ambacho KILA mtu kambale, Sasa aliyoyasema uyo Bwana mkubwa ,yamepitia vikao GANI rasmi ndani ya Chama chenu,je yeye Kama kiongozi anawezaje amulia wenye chama chao, nanyi mpo ,mmeki na ile ya zidum fikra za kiongozi/ mwenyekiti

Nazungumza hivi binafsi nataka vyama vyote kua imara , na hapo utam wa siasa Ndo unapokuja,

Sasa chama chenu kimekufa,Ndo maana mnaona mnabebwa na dola , na matatizo yote yanaanzia hapa

Ccm inataji watu wapya kuludisha chama kwenye mstari, kiongozi lazima akieshim chama ,sio chama kimueshim kiongozi, njoo mjifunze CHADEMA
 
Napenda sana ninapojibizana na mtu kama wewe chief, Kongole kwako, ngoja tusubiri kikao cha Hangaya na Wapinzani kitatoa maamuzi gani, Kuna mambo 3 muhimu ya kuyajadili na ijulikane yanafanyika vipi; "MIKUTANO YA HADHARA, HOW TUNAKWENDA KWENYE KATIBA MPYA, NA UHURU WA WAPINZANI KUFANYA SHUGHULI ZAO ZA KISIASA KAMA CCM WANAVYOFANYA".
 
Mkuu hata mie binafsi napenda watu wenye fikra pevu ,hoja hujibiwa kwa hoja sio matusi mkuu,Ongera sana
 
Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.

Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.

"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.

Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.

Amesema katika mitandao ya kijamii wapunguze kuzungumza mambo mengi ili kusudi wanapotamka mambo machache yaonekane kuwa na maana kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi
Well said my PM!!

Lakini ilifaa sana hili jambo liongolewe au lipigiwe chapuo na viongozi wa CCM badala yako wewe PM kwa maana ya Karibu Mkuu, Mwenezi n.k
 
Umeongea ukweli kwenye hili, hayo ilibidi yatamkwe na Shaka or KM
 
Mkuu hata mie binafsi napenda watu wenye fikra pevu ,hoja hujibiwa kwa hoja sio matusi mkuu,Ongera sana
Kesho Kwenye joto la asubuhi la G.Hando atakuwepo B. Membe, saa moja asubuhi ya TZ, kuna mtu atavuliwa nguo huko! Tupeleke maskio yetu huko
 
Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.

Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.

"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.

Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.

Amesema katika mitandao ya kijamii wapunguze kuzungumza mambo mengi ili kusudi wanapotamka mambo machache yaonekane kuwa na maana kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi
Bila katiba mpya maccm yatauana,
Umoja wa kiunafiki siyo salama
 
Sahau kura yangu nitamkanselii yeyetuu ila ubunge ntampa wa ccm
 
Back
Top Bottom