Majambazi 10 yalijipanga mstari mmoja barabarani usiku kuzuia gari langu lisipite

Kwa hiyo usingetaja jina la Yesu wasingetoka barabarani?
Amenikumbusha jamaa mmoja.

Jamaa alikuwa na kesi ngumu sana, kesi ilikuwa mbaya anafungwa miaka mingi.

Tukampigania akapata wakili mzuri, wakili akashinda kesi.

Jamaa kutoka, akafurahi sana. Sasa tumekaa yeye na wakili na mimi, jamaa akawa anamsifia Yesu sana kwa kumshindia kesi.

Wakati wakili yuko pale pale.

Nikaona yule wakili amesononeka lakini kajizuia tu kusema.

Kimoyomoyo alikuwa anasema "kazi nimefanya mimi, sifa anapewa Yesu".
 
Duh mkuu pole naamin MUNGU yu pmja nawe
 
UKAKANYAGA MAFUTA UKAONGEZA GIA[emoji35][emoji2959] !?! Bora ungeacha tu uongo mtumishi.
 
UKAKANYAGA MAFUTA UKAONGEZA GIA[emoji35][emoji2959] !?! Bora ungeacha tu uongo mtumishi.
Hapo nimeongea uongo upi? Uongo nauchukia kama ukoma. Au umechanganyikiwa na neno "kukanyaga mafuta?" Hiyo ni lugha ya madereva ikimaanisha kukandamiza zaidi accelerator(gas pedal). Sio "kukanyaga mafuta ya upako"
 
Kwanza kabsa nikupongeze kwa swala moja lakuesabu majambazi nakujua wako kumi... Pili ingekua nimimi wewe ningevuta mafuta nikiwakaribia nazima taaa😅
 
Kwanza kabsa nikupongeze kwa swala moja lakuesabu majambazi nakujua wako kumi... Pili ingekua nimimi wewe ningevuta mafuta nikiwakaribia nazima taaa😅
Hahaa, baada ya kuzima taa ungefanyaje?
 
Umenichekesha sana mkuu hivi unajua majambazi kweli,,wanahata mda wa kushikana mikono,hizo bunduki zao na mapanga wataweka wapi
 
Naamini kama nisingetaja Jina la Yesu, wasingetoka barabarani. Majambazi yaliyokula bange, si yanaona gari linalokuja mbele yao ni kama panya tu!
Hofu ni kama mbele kuna magogo au mawe.Zaidi ya hapo ni kuchezea tairi tu.
 
Hii ni baada ya kukanyagwa na tembo au kabla..........una matukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…