Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 50,587
- 71,492
kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu.......kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa,
nieleweshe hapa kwanza
[emoji28][emoji28][emoji28]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu.......kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa,
nieleweshe hapa kwanza
Yesu ni Mungu
Msalimie mwamposaWana bodi, naomba niwapashe habari ya tukio la hatari sana nililokutana nalo siku chache zilizopita. Kweli Waswahili hawakukosea waliposema: "duniani kuna mambo... tembea uone."
Siku hiyo ya tukio, mimi na marafiki zangu wawili tulikuwa tunafanya kazi fulani nyumbani kwangu kuanzia jioni. Kazi hiyo ilikuwa nzito na ilitakiwa iishe siku hiyo hiyo. Tukaifanya hadi saa saba hivi usiku. Baada ya kazi hiyo kukamilika, hao marafiki zangu wakaniambia wanataka warudi nyumbani kwao, kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu. Ila hawakuwa na usafiri wao binafsi na muda huo magari yote ya abiria yalikuwa yameishafunga kazi. Hivyo ikabidi nichukue gari langu na kuwapeleka hao ndugu mpaka nyumbani kwao. Tulifika kwao bila tatizo, nikawaaga, nikageuza gari na kuanza kurudi nyumbani kwangu.
Kilometa kama nne, kabla ya kufika nyumbani kwangu, nikiwa barabarani, kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa, ghafla, mita kama mia mbili mbele yangu, nikaona watu wapatao kumi wanajitokeza na kuingia katikati ya barabara. Baadhi yao walitokea upande wa kushoto wa barabara na wengine walitokea upande wa kulia wa barabara. Kwa haraka sana wakajipanga mstari mmoja unaokatiza barabara huku wamepanua mikono yao kunizuia nisipite! Akili yangu ikaniambia hao lazima ni majambazi. Wanacholenga hapo ni kunifanya nisimamishe gari kisha wanidhuru au kuiba gari langu. Hivyo nikaona kusimamisha gari sio uamuzi wa busara, niendelee tu kuendesha gari. Nikajiuliza, nikiwakaribia wasipoondoka barabarani, itakuwaje? Si nitaua mtu? Nikaamua tu nisisimame. Nikatamka: "Kwa Jina la Yesu Kristo...shetani shindwa na ulegee." Nikakanyaga mafuta, nikaongeza gia, nikawasha "full lights" na kusonga mbele. Wakati huo hapakuwa na magari yoyote yanayopita barabarani.
Mita kama kumi kabla ya kuwafikia hao majambazi, nikaona wanatawanyika wenyewe kwa haraka huku "wakishangilia" hee hee hee heeee!! Nikapita hapo na sikupunguza mwendo mpaka nilipokaribia nyumbani.
Kwa tukio hilo, nimehakikisha Jina la Yesu lina uwezo wa kusambaratisha hata majambazi. Lakini pia nmejifunza sio vizuri kuendesha gari usiku, kuna hatari nyingi. Ni kweli Mungu akiwa upande wetu hakuna awezaye kuwa juu yetu(Warumi 8:31). Na maadui wakija kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba(Kum 28:7). Hata hivyo tusimjaribu Mungu. Mimi siku hiyo sikumjaribu Mungu kwakuwa sikuwaza wala sikutarajia kukutana na majambazi wengi hivyo tena kwenye barabara yenye taa za barabarani na majumba mengi kila upande wa barabara. Naamini kwa sababu sikumjaribu Mungu, alinipigania na kunilinda, nikarudi nyumbani salama.
Umesababisha nacheka sana hapa wewe KakaMkubwamkuu nakutakia asubuhi njema.
Mkuu unahuakika""
Halikuwa group la walevi!!??
Wakiomba Rift[emoji2]
Kwani ndie huyu huyu wa mguu wa tembo kifuani[emoji44][emoji44] akiwa ugenini!?Mkuu hii ilikuwa baada ya kukanyagwa na Tembo kifuani au kabla?
Unavutaga bangi?Wana bodi, naomba niwapashe habari ya tukio la hatari sana nililokutana nalo siku chache zilizopita. Kweli Waswahili hawakukosea waliposema: "duniani kuna mambo... tembea uone."
Siku hiyo ya tukio, mimi na marafiki zangu wawili tulikuwa tunafanya kazi fulani nyumbani kwangu kuanzia jioni. Kazi hiyo ilikuwa nzito na ilitakiwa iishe siku hiyo hiyo. Tukaifanya hadi saa saba hivi usiku. Baada ya kazi hiyo kukamilika, hao marafiki zangu wakaniambia wanataka warudi nyumbani kwao, kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu. Ila hawakuwa na usafiri wao binafsi na muda huo magari yote ya abiria yalikuwa yameishafunga kazi. Hivyo ikabidi nichukue gari langu na kuwapeleka hao ndugu mpaka nyumbani kwao. Tulifika kwao bila tatizo, nikawaaga, nikageuza gari na kuanza kurudi nyumbani kwangu.
Kilometa kama nne, kabla ya kufika nyumbani kwangu, nikiwa barabarani, kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa, ghafla, mita kama mia mbili mbele yangu, nikaona watu wapatao kumi wanajitokeza na kuingia katikati ya barabara. Baadhi yao walitokea upande wa kushoto wa barabara na wengine walitokea upande wa kulia wa barabara. Kwa haraka sana wakajipanga mstari mmoja unaokatiza barabara huku wamepanua mikono yao kunizuia nisipite! Akili yangu ikaniambia hao lazima ni majambazi. Wanacholenga hapo ni kunifanya nisimamishe gari kisha wanidhuru au kuiba gari langu. Hivyo nikaona kusimamisha gari sio uamuzi wa busara, niendelee tu kuendesha gari. Nikajiuliza, nikiwakaribia wasipoondoka barabarani, itakuwaje? Si nitaua mtu? Nikaamua tu nisisimame. Nikatamka: "Kwa Jina la Yesu Kristo...shetani shindwa na ulegee." Nikakanyaga mafuta, nikaongeza gia, nikawasha "full lights" na kusonga mbele. Wakati huo hapakuwa na magari yoyote yanayopita barabarani.
Mita kama kumi kabla ya kuwafikia hao majambazi, nikaona wanatawanyika wenyewe kwa haraka huku "wakishangilia" hee hee hee heeee!! Nikapita hapo na sikupunguza mwendo mpaka nilipokaribia nyumbani.
Kwa tukio hilo, nimehakikisha Jina la Yesu lina uwezo wa kusambaratisha hata majambazi. Lakini pia nmejifunza sio vizuri kuendesha gari usiku, kuna hatari nyingi. Ni kweli Mungu akiwa upande wetu hakuna awezaye kuwa juu yetu(Warumi 8:31). Na maadui wakija kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba(Kum 28:7). Hata hivyo tusimjaribu Mungu. Mimi siku hiyo sikumjaribu Mungu kwakuwa sikuwaza wala sikutarajia kukutana na majambazi wengi hivyo tena kwenye barabara yenye taa za barabarani na majumba mengi kila upande wa barabara. Naamini kwa sababu sikumjaribu Mungu, alinipigania na kunilinda, nikarudi nyumbani salama.
Naamini kama nisingetaja Jina la Yesu, wasingetoka barabarani. Majambazi yaliyokula bange, si yanaona gari linalokuja mbele yao ni kama panya tu!
AmenThere is power in the blood of Jesus to break every chain[emoji445][emoji445][emoji445]
Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app