Majambazi 10 yalijipanga mstari mmoja barabarani usiku kuzuia gari langu lisipite

Wana bodi, naomba niwapashe habari ya tukio la hatari sana nililokutana nalo siku chache zilizopita. Kweli Waswahili hawakukosea waliposema: "duniani kuna mambo... tembea uone."

Siku hiyo ya tukio, mimi na marafiki zangu wawili tulikuwa tunafanya kazi fulani nyumbani kwangu kuanzia jioni. Kazi hiyo ilikuwa nzito na ilitakiwa iishe siku hiyo hiyo. Tukaifanya hadi saa saba hivi usiku. Baada ya kazi hiyo kukamilika, hao marafiki zangu wakaniambia wanataka warudi nyumbani kwao, kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu. Ila hawakuwa na usafiri wao binafsi na muda huo magari yote ya abiria yalikuwa yameishafunga kazi. Hivyo ikabidi nichukue gari langu na kuwapeleka hao ndugu mpaka nyumbani kwao. Tulifika kwao bila tatizo, nikawaaga, nikageuza gari na kuanza kurudi nyumbani kwangu.

Kilometa kama nne, kabla ya kufika nyumbani kwangu, nikiwa barabarani, kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa, ghafla, mita kama mia mbili mbele yangu, nikaona watu wapatao kumi wanajitokeza na kuingia katikati ya barabara. Baadhi yao walitokea upande wa kushoto wa barabara na wengine walitokea upande wa kulia wa barabara. Kwa haraka sana wakajipanga mstari mmoja unaokatiza barabara huku wamepanua mikono yao kunizuia nisipite! Akili yangu ikaniambia hao lazima ni majambazi. Wanacholenga hapo ni kunifanya nisimamishe gari kisha wanidhuru au kuiba gari langu. Hivyo nikaona kusimamisha gari sio uamuzi wa busara, niendelee tu kuendesha gari. Nikajiuliza, nikiwakaribia wasipoondoka barabarani, itakuwaje? Si nitaua mtu? Nikaamua tu nisisimame. Nikatamka: "Kwa Jina la Yesu Kristo...shetani shindwa na ulegee." Nikakanyaga mafuta, nikaongeza gia, nikawasha "full lights" na kusonga mbele. Wakati huo hapakuwa na magari yoyote yanayopita barabarani.

Mita kama kumi kabla ya kuwafikia hao majambazi, nikaona wanatawanyika wenyewe kwa haraka huku "wakishangilia" hee hee hee heeee!! Nikapita hapo na sikupunguza mwendo mpaka nilipokaribia nyumbani.

Kwa tukio hilo, nimehakikisha Jina la Yesu lina uwezo wa kusambaratisha hata majambazi. Lakini pia nmejifunza sio vizuri kuendesha gari usiku, kuna hatari nyingi. Ni kweli Mungu akiwa upande wetu hakuna awezaye kuwa juu yetu(Warumi 8:31). Na maadui wakija kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba(Kum 28:7). Hata hivyo tusimjaribu Mungu. Mimi siku hiyo sikumjaribu Mungu kwakuwa sikuwaza wala sikutarajia kukutana na majambazi wengi hivyo tena kwenye barabara yenye taa za barabarani na majumba mengi kila upande wa barabara. Naamini kwa sababu sikumjaribu Mungu, alinipigania na kunilinda, nikarudi nyumbani salama.
Msalimie mwamposa
 
Mbona ishu simpo na ndogo sana hiyo?

Mimi niliwahi kugonga mmoja alichelewa kukimbia.

Nikaja kusikia ni polisi jamii hawa sijui katibu wa mtaa.

Nikawaambia wajifunze kusimamisha watu vizuri usiku. Reflector haikupi authority yoyote.

Pole sana mkuu.
 
Hao majambazi hawakuweka hata mawe [emoji1787][emoji1787][emoji1787] upasue hizo tairi
 
Kumbe lengo ni kuhubiri, anyway naogopa kukutajia hao majambazi maana utaniona nakuchonganisha ila ungeweka wazi hiyo kazi mliyokuwa mkifanya ningetaja bila wasiwasi

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Majambazi yakashangilia😂😂😂 acha masihara😂
Nalog off
 
Vibaka wazuie gari kwa mikono kuna watu waoga sana aisee mwanaume haitakiwi uwe muoga muoga bhana daah kwa uoga huo unaweza kuwahesabu vibaka kweli ? Vibaka hawana hana siraha yeyote unawaita majambazi...
 
Wana bodi, naomba niwapashe habari ya tukio la hatari sana nililokutana nalo siku chache zilizopita. Kweli Waswahili hawakukosea waliposema: "duniani kuna mambo... tembea uone."

Siku hiyo ya tukio, mimi na marafiki zangu wawili tulikuwa tunafanya kazi fulani nyumbani kwangu kuanzia jioni. Kazi hiyo ilikuwa nzito na ilitakiwa iishe siku hiyo hiyo. Tukaifanya hadi saa saba hivi usiku. Baada ya kazi hiyo kukamilika, hao marafiki zangu wakaniambia wanataka warudi nyumbani kwao, kilometa kama kumi kutokea nyumbani kwangu. Ila hawakuwa na usafiri wao binafsi na muda huo magari yote ya abiria yalikuwa yameishafunga kazi. Hivyo ikabidi nichukue gari langu na kuwapeleka hao ndugu mpaka nyumbani kwao. Tulifika kwao bila tatizo, nikawaaga, nikageuza gari na kuanza kurudi nyumbani kwangu.

Kilometa kama nne, kabla ya kufika nyumbani kwangu, nikiwa barabarani, kwa mwendo wa kilometa kama 50 kwa saa, ghafla, mita kama mia mbili mbele yangu, nikaona watu wapatao kumi wanajitokeza na kuingia katikati ya barabara. Baadhi yao walitokea upande wa kushoto wa barabara na wengine walitokea upande wa kulia wa barabara. Kwa haraka sana wakajipanga mstari mmoja unaokatiza barabara huku wamepanua mikono yao kunizuia nisipite! Akili yangu ikaniambia hao lazima ni majambazi. Wanacholenga hapo ni kunifanya nisimamishe gari kisha wanidhuru au kuiba gari langu. Hivyo nikaona kusimamisha gari sio uamuzi wa busara, niendelee tu kuendesha gari. Nikajiuliza, nikiwakaribia wasipoondoka barabarani, itakuwaje? Si nitaua mtu? Nikaamua tu nisisimame. Nikatamka: "Kwa Jina la Yesu Kristo...shetani shindwa na ulegee." Nikakanyaga mafuta, nikaongeza gia, nikawasha "full lights" na kusonga mbele. Wakati huo hapakuwa na magari yoyote yanayopita barabarani.

Mita kama kumi kabla ya kuwafikia hao majambazi, nikaona wanatawanyika wenyewe kwa haraka huku "wakishangilia" hee hee hee heeee!! Nikapita hapo na sikupunguza mwendo mpaka nilipokaribia nyumbani.

Kwa tukio hilo, nimehakikisha Jina la Yesu lina uwezo wa kusambaratisha hata majambazi. Lakini pia nmejifunza sio vizuri kuendesha gari usiku, kuna hatari nyingi. Ni kweli Mungu akiwa upande wetu hakuna awezaye kuwa juu yetu(Warumi 8:31). Na maadui wakija kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba(Kum 28:7). Hata hivyo tusimjaribu Mungu. Mimi siku hiyo sikumjaribu Mungu kwakuwa sikuwaza wala sikutarajia kukutana na majambazi wengi hivyo tena kwenye barabara yenye taa za barabarani na majumba mengi kila upande wa barabara. Naamini kwa sababu sikumjaribu Mungu, alinipigania na kunilinda, nikarudi nyumbani salama.
Unavutaga bangi?
 
Bado sijaona comment inayosema;

"Hongera kwa kumiliki Gari"

🤣🤣🤣🤣
 
Naamini kama nisingetaja Jina la Yesu, wasingetoka barabarani. Majambazi yaliyokula bange, si yanaona gari linalokuja mbele yao ni kama panya tu!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we jamaa umenichekesha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wangeweka magogo, na mijiwe mikubwa, ingekuwa hatar.
 
Back
Top Bottom