Majasusi wa Tanzania fungueni macho. Teueni watu wenye uwezo sio kwa kujuana

Umeandika ujinga mtupu,shivji na muhongo hamna kitu
 
Kuna jina la rais umekutana nalo kwenye thread yangu? Au vipi?
 

Kazi ya TISS sio kuipangia nchi nani awe nani. Kufanya hivyo ni kukiuka mandate yake. Umetoa mfano wa watu ambao hakuna aliyewazuia kugombea uongozi. Lissu na Muhungo, wote, wameshajaribu kuwania kiti cha Rais hawakufanikiwa. Professor Shivji yeye hajawahi kugombea hata udiwani. Ulitaka TISS wafanye nini?

Hata huko Marekani, Bush Sr na Bush Jr hawakuwekwa na CIA. Juhudi zao ndizo zilizowawezesha kukipata kiti cha Rais wa Marekani. After all, in a democratic country, haiwezekani kumuandaa mtu fulani kushika kiti cha Rais au PM. Ndiyo maana hata outsiders kama Obama na Trump walifanikiwa kukipata kiti cha Rais wa Marekani.
 

Hivi watu wengine mna ugonjwa gani? Nadhani tukuache tu, kwasababu hata mwaka tu hujui una miezi mingapi.
 
Umeshachelewa mkuu. Tunakujua wewe huwa unajifanya kuandika herufi kama darasa la saba B lakini wewe ni msomi mkubwa na uko deep sana.
 
Bado Mama Samia namkubali sana
 
Majasusi wa kulamba asali tu ndio wapo. Taifa halina maono, viongozi dhaifu full kupapasa.
 
Jasusi aliyebobea anaweka chekecheo Ololosokwani anatenganisha mbaazi na mahage ikishindikana atupia MCHANGA
 
Jamaa mmoja aliteuliwa kuwa mkuu wa TPDC kelele zikapigwa akafutwa fasta
 
Uko sahihi na Nadhani linaeleweka, ila NAWAZA hao Majasusi wengi ni makada + akili ndogo

Lkn ni muhimu kufanyia kazi ushauri wako...maana uhakika Mchwa watafanya na wanafanya yao...

Akili kubwa sana hii
Suluhu ya idara hii isiwe chini ya waziri anayeteuliwa na Rais aliyepo madarakani.Msiwalaumu waliomo kwenye hiyo idara.Tujilaumu na Bunge letu kuchanganya wanataaluma wa idara nyeti na makada CHAWA NA WAPAMBE hadi Bosi ananuna.
 
Sina uelewa mpana lakini kuna mambo mengi ya kujiuliza kwa nini?
Moja ream paper tunauziwa Tshs 25000 wakati kabla ya awamu ya sita ilikuwa 12,000.
Mafuta ya kupikia,mikoa mingi wanalima alizeti ,za kuahuzwa nje ni tshs 32000 za ndani ni 37,000 sasa hapo wanaoagiza nje wakiagiza mengi wakulima watakosa soko lakini kwa nini bei yetu ipo juu?.
Tatu,nchi jirani wanapitia Tanzania sababu ya barabara tukifumbia macho badala ya kuzitanua wapite vizuri tuvune pesa mmeacha jirani yetu akijenga zake tukikimbiwa tusishangae.
 
Nimeona umemuweka Shivji hapo, ni hivi, taifa litahitaji academicians, watu ambao mawazo ya tafiti zao yanapaswa kutazamwa kwa uzito fulani kwa ajili ya mustakabali wa taifa, sio kila msomi awe mwana siasa, nchi ijengwe na nani sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…