Maji ya chupa ya Kilimanjaro yameanza kupotea sokoni Dar

Maji ya chupa ya Kilimanjaro yameanza kupotea sokoni Dar

Yanachumvi'aje wakati kitaalamu tunaambiwa hayo siyo maji ya 'kudimbula' bali ni purified (distilled)water, yaani maji mvuke!

Sasa chumvi inaingiaje kwenye mvuke!

Au walishabadili ama kukoleza sana hayo madawa yao wanayoweka!

Huo ndiyo mwanzo wa kutoka kwenye reli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaelewa nini unaposikia distilled water?
 
Ladha ya Maji ya Kilimanjaro ni ileile haijabadilika hata kidogo.
 
Ladha ya Maji ya Kilimanjaro ni ileile haijabadilika hata kidogo.
Hata mimi nawashangaa hawa wademkaji, tatizo wabongo wengi elimu duni..............yaani unapima ubora wa maji kwa kutumia ladha ya ulimi badala ya kuangalia madini yaliyomo. Ukisoma mineral content kwenye maji ya kilimanjaro ni tofauti kabisa na hayo ya Hill na hili ndo linaweza kutofautisha ladha lakini siyo ubora. Kuna minerals lazima uzipate kwenye vyakula na maji na kama ukipungukiwa inakula kwako....
 
Dar kunyweni maji mtakayo. Nipo kanda ya juu kusini kuna Rungwe, Mkwawa, Chemchem, Kitulo, Dew nk. Niache kunywa hayo nitafute Kilimanjaro!

Unashangaa mtu ana duka Mwakalele ndanindani huko anaweka maji kutoka mikoa 6 huko! Huo uzalendo mnaosema si uanzie nyumbani kwako basi?
 
Hayana faida nzuri kwa wauzaji na utokaji wake ni wa polepole.

Ila kwenye bar za wachaga au maduka yao huwezi kuyakosa.
Nikweli kabisa wanywaji ni wachaga, nina rafiki yangu mmoja hanywi maji tofauti na Kilimanjaro
 
Dar kunyweni maji mtakayo. Nipo kanda ya juu kusini kuna Rungwe, Mkwawa, Chemchem, Kitulo, Dew nk. Niache kunywa hayo nitafute Kilimanjaro!

Unashangaa mtu ana duka Mwakalele ndanindani huko anaweka maji kutoka mikoa 6 huko! Huo uzalendo mnaosema si uanzie nyumbani kwako basi?
Maji ya huko ni real spring water kwahiyo matamu sana..sana yaani unakunywa hadi raha
 
Kwa sisi tunaofanya water quality,tunakuambia kuwa maji yanayotengenezwa dar es salaam yote chanzo chake Ni DAWASCO,kasoro maji ya AFYA tu,yaliyopo kigamboni.

Utajiuliza Ni kwa nn? Jibu Ni rahisi tu ,kutumia maji ya dawasco gharama ipo chini,maana tayari wameshacontrol pH(alkalinity na acidity)kitu ambacho kwenye utengenezaji wa maji Ni gharama kidogo,hvyo kwa kutumia maji ya dawasco Kuna gharama utaziepuka,Ni vitu vidogo utatakiwa ugharamike Kama kiasi Cha chlorine kwenye maji,kiasi Cha mwanga unaipita kwenye maji(turbidity)

Ukija kwenye maji ya chemchem kama kitulo,udzungwa, Kilimanjaro,ndanda, Abbey n.k vitu Kama pH na nutrients zingne vpo katika uwiano mzuri kasoro chlorine baadhi ya maji inakuwa ipo juu inayopelekea hata meno kuungua

Kwa hyo sio kweli maji ya Kilimanjaro Yana chumvi,labda Ni fake,pia sio kweli kwamba maji ya Kilimanjaro yanatengenezwa kibaha,

Maji ya Kilimanjaro yanatoka Moshi ,eneo linaitwa shirimatunda Kama unaenda TPC
Hauwezi kuita maji ya Kilimanjaro Kama hayatoki eneo husika,
 
Renovation inahitajika apo especially packaging Wanachupa za ovyo pia quality imeyumba
 
Hata kabla ya Mengi kufariki, maji ya Kilimanjaro yalishapoteza ladha kabisa.

Kuanzia walipoondoa packaging ya maboksi, maji yalianza kuchakachuliwa mno na kuleta ladha mbaya.

Dew Drop madogo ndiyo maji ninayoyapenda sana.
Dew Drop ni best kuliko maji yote tatizo yanapatikana sehemu chache mno
 
Maji ya kilimanjaro iliwalenga watu wenye uwezo.... Baada ya wadau kuingia kwa kasi ktk biashara ya maji na kuuza kwa bei ya chini hapo ndipo soko la maji ya kili ilipoanza potea. Ila naona mpaka sasa maji ya kili bado wanawalenga watu fulani tu

Ova
 
Maji ya kilimanjaro tunayokunywa dar sio yale yanayotoka bonite. Yanantengenezwa hapo kibaha tu. Hata taste yake ni.chumvi tu. Tofauti kabisa na ukinywa yale origional ya moshi/arusha
Kibaha sehemu gani mkuu mimi naishi kibaha??
 
Na wewe siuwe una nunua kwa kabila lako acha kulalamika by the way charity begins at home, usipo myungisha ndugu yako huo ni uzwazwa
Silalamiki Bali nasema ukweli ama Kuna mjaluo anaweza akanunua duka la mkalenjini.
Nesi mkikuyu hawezi kufanya kazi wataita.
Mie nalikemea hili Mana waafrika ukabila unaturudisha nyuma.
Pia hatujakataa kuwa wapo waliosoma kuzidi wengine na kuwa na hela.
Ila sasa sio tiketi ya kujiona kuwa uu unique na kuwatukana wengine.

Kumbuka ukabila ndio unaotuua afrika na ndio uliofanya tukatawaliwa na wakoloni.

Afu Kama una ubaguzi utaendelea mpaka nyumbani kabisa.
Nina Imani unajua ukiwa pale Moshi mjini utaiskia hizi kauli yaani huyu mrombo kajaza warombo wenzake kwenye iyo ofisi,huyo mmarangu ama mkibosho anaongea
 
Back
Top Bottom