Maji ya kilimanjaro sio mazuri siku hizi

kuna yale maji ya dew drop nilikua nayaona ya bei ghali sana navile vichupa wamedesign nikawa hata siyasogelei nikikumbuka nacheka sana
 
Kweli Au maji unayo kunywa yamechakachuliwa,na kutapika juu?
Mimi sinunuagi dukani mie nachukua kwenye magari ya coca na wanatuleteaga hapo dukani za kutosha .
Yachakachuliwe kuvipi
 
Kilimanjaro 💦 na Dasani 💦 ni maji bora kwa hapa nchini. Anayebisha atakuwa ametumwa na Zamzam
Nabisha siku hizi wanazidisha chemicali zinakuwa chungu sana . Hadi ukiyazidisha kuyanywa unapata kichefu chefu
 
Kuna mikoa ni kilimanjaro tu hamna kampuni zingine.Haya maji tulishayapigia kelele sana.
 
Watu wa mirungi mbona hawalalamiki maana ndio watumiaji wakubwa .
 
Dew drop, Buyegi na Hill. Kilimanjaro kwa kweli sio kama zamani. Nlidhani ni mimi mwenyewe aisee
 
Wewe utakuwa na kampuni Yako ya maji unataka kuwaharibia wenzako biashara yao. Hakuna maji mazuri kama Kilimanjaro. Huwezi kuharibu brand ambayo wameifanyia kazi miaka kwa statements za uwongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…