Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?

Mkuu hata mimi ni mkristo kama wewe ila lazima tukubali kuna mambo kwenye bible yana walakini inawezekana waandishi walifanya makosa kwenye kusimulia hivo visa.
Au inawezekana wewe unafanya makosa. By the way, umesoma article niliyoiandika page zilizopita? Labda itakusaidia kugundua kuwa aliyekosea ni wewe na Biblia kama ilivyo ada iko sahihi kabisa!

in case hukuiona: Yesu Kristo ni Bwana na Mfalme!: Swali #4 - Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?
 
Maji ya mafuriko huwa yanaenda wapi? Si unaona pale jangwani hugeuka Kama kisiwa kidogo kwa muda?
 
Wanjama walikuwa wanakula chakula kilichomo kwa uwezo wa mungu
Af wanyama milion wanatosha maana wanyama wakubwa ni tembo twiga kifaru simba na wengine wachache waliobaki ni wadogo2
Kiufupi ukiunganisha na uwezo wa Mungu wanatosha
Na kuhusu kusambaa. Vitu vyovyote husambaa duniani kutafta chakula
Na hao pollar bears ni kama bears wa kawaida sema kutokana na wao kuishi sanasana sehem ya barafu mwili wake unafanya adaptation

Af kumbuka geographic conditions change
Unavyosemea kuna wanyama hawawezi kuishi kule hyo ni kutokana na geographical condition ya sikuizi
Ata science inatwambia kadri siku zinavyoenda majangwa yanazidi na joto linaongezeka

Narudia tena ni uwezo wa Mungu

Pia naomba utafakari hili: kama Mungu hakuumba chochote Kipi kilikuwa cha kwanza kati ya kuku na yai???
 
Hiyo historia ni ya kibaguzi ya kiafrica
Ushaona wapi wazungu wakisema walikuwa manyani
Ndo maana adi leo wanatuita manyani
 
Mkuu hata mimi ni mkristo kama wewe ila lazima tukubali kuna mambo kwenye bible yana walakini inawezekana waandishi walifanya makosa kwenye kusimulia hivo visa.
Hawakufanya makosa we ndo huelewi
Soma vizuri utagundua walisubiri yakauke
Na kukauka inamaana yanyonywe na ardhi
 
ukisoma bible ukachanganya na history au geography utakuwa confused sana
Somehow, ingawa ukisoma physical geography kwa undani san ina ushahidi mwingi sana wa kushikika kuhusu mambo ya kibiblia. Kama unaangalia chanel ya National Geographic and Discovery, utakubali hili.
 
Bustan ya eden sio bustan,,ni uwepo wa mungu mahali pale walipokuwepo adam na hawa.. Ndio maana alipowafukuza alimaanisha anajitenga nao kuwa karibu kama awali lakin sio kuwatupa moja kwa moja...
 
hapo namba tano hapo hebu naomba ufafanuzi vizuri kwamba ulitumia vipimo gani kujua kwamba titanic ni kubwa kuliko safina hebu nielezee kiundani zaidi
 
unafikiri upo serious kuuliza maji hayo yalienda wapi wakati unaona kabisa robo tatu ya dunia ni maji? theluthi moja tu ndio ardhi, zaidi sana, Mungu ni muumbaji anaweza kukausha yakabaki anayoyataka.
 
Somehow, ingawa ukisoma physical geography kwa undani san ina ushahidi mwingi sana wa kushikika kuhusu mambo ya kibiblia. Kama unaangalia chanel ya National Geographic and Discovery, utakubali hili.
Kuna article nimeandika fupi tu inajumlisha na hint za ushahidi toka katika Geology/Geography. Sina hakika wangapi wameisoma ila naona kama wameiruka hivi maana maswali mengi yanaulizwa na nimeyaainisha majibu kule.

Kama ulivyosema Ukisoma Geology, Engineering, Science, Linguistics, Philosophy, Historia, na field zote za Sayansi halisi unaweza usiiamini Biblia ila utakubali kuwa Biblia si kitabu cha kawaida. Kuna mambo mle hayaelezeki yamefikaje kama ingekuwa ni invention ya watu maana kuna mengine na Teknolojia tunayojidai nayo tumeyajua juzi, ila mle yapo maelfu ya miaka!
 
unafikiri upo serious kuuliza maji hayo yalienda wapi wakati unaona kabisa robo tatu ya dunia ni maji? theluthi moja tu ndio ardhi, zaidi sana, Mungu ni muumbaji anaweza kukausha yakabaki anayoyataka.

Haaa haaaa, teeeh teeeh , aiseee nimecheka sana kwa jinsi ulivyoandika!
Nimekupa "like" for sure, you disserve it!

Naamini ataelewa tu, hata kama hataki au hana uwezo huo wa kuelewa!
 
Hiyo niliyotumia hapo inaitwa "logic" hivyo, inahitaji akili kubwa kuelewa nilichoandika.
UNAJUA LOGIC INAHUSISHA REASONING SS YA KWAKO HIYO SIJUI NI REASONING AU RESONATING mm sijaona REASONING HAPO
 
Aisee kumbe kuna watu kufikiri ni tatizo?!

Kwani mvua inayoshesha ,mf kawaida tu ,km hapa dar siku moja na inaleta mafuriko ,maji huwa yanatoka wapi?
Na yakikauka watu wakarudi kwny makazi yao huwa yanakua yameenda wapi yale maji?

Eti walikula nn, soma biblia uone maelekezo aliyopewa Nuhu kabla na baada ya kujenga safina,kabla na baada ya gharika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…