Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?

Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?

Kuna article nimeandika fupi tu inajumlisha na hint za ushahidi toka katika Geology/Geography. Sina hakika wangapi wameisoma ila naona kama wameiruka hivi maana maswali mengi yanaulizwa na nimeyaainisha majibu kule.

Kama ulivyosema Ukisoma Geology, Engineering, Science, Linguistics, Philosophy, Historia, na field zote za Sayansi halisi unaweza usiiamini Biblia ila utakubali kuwa Biblia si kitabu cha kawaida. Kuna mambo mle hayaelezeki yamefikaje kama ingekuwa ni invention ya watu maana kuna mengine na Teknolojia tunayojidai nayo tumeyajua juzi, ila mle yapo maelfu ya miaka!
Sawia kabisa
 
Hawakufanya makosa we ndo huelewi
Soma vizuri utagundua walisubiri yakauke
Na kukauka inamaana yanyonywe na ardhi
Mkuu unajua maji ya kuijaza dunia nzima, hebu fikiria urefu wa mlima everest na uwe chini ya maji ardhi gani inaweza nyonya maji yote hayo kwa akiri yako.
 
hapo namba tano hapo hebu naomba ufafanuzi vizuri kwamba ulitumia vipimo gani kujua kwamba titanic ni kubwa kuliko safina hebu nielezee kiundani zaidi
Mkuu ulikuwa unatoroka Sunday school hebu google Noah's ark utapewa details na vipimo vikiwa in modern measurement.
 
Akili za facebook ukizileta kwa akili kubwa jf nitatizo tukuulize basi tangu uanze kunywa maji umekunywa bahari ngapi na yanaenda wapi
 
Yapo angani ,ukweli ni kwamba kiasi cha maji yaliyopo angani(mvuke na mawingu) ni kikubwa kuliko hata maji yaliyopo kwenye bahari zote na chini ya ardhi,kwa sababu kuna mawingu mengine yanayofanya giza na kumfunika Mungu.
Kumfunika MUNGU?so unataka kusema MUNGU yupo mawinguni?
 
Mkuu unajua maji ya kuijaza dunia nzima, hebu fikiria urefu wa mlima everest na uwe chini ya maji ardhi gani inaweza nyonya maji yote hayo kwa akiri yako.
Biblia ina majibu yote.
Mungu alimwagiza Nuhu kujenga safina akiwa na miaka 500
.Nuhu alijenga safina inasemekana miaka 98
.Nuhu aliingia ndani ya safina mwaka wa 600 siku ya 17 ya mwezi wa pili ,
.Nuhu akikaa ndani ya safina kwa muda wa miezi 11 na siku 10 ,kwa sababu alitoka ktk safina mwaka wa 601 ,mwezi wa kwanza siku ya 27.
.Maji ya gharika yakipungua Mungu alipovumisha Upepo juu ya nchi,maana yake maji yalichange kuwa water vapour(mvuke).Pia chemichem za ardhi zilifungwa na madirisha ya mbinguni yalifungwa.
.Nuhu alikusanya chakula cha kutosha kwa ajili yake na wanyama waliokuwa ndani ya safina.
Nb viumbe wanaoishi katika maji hawakudhulika na hii gharika hivyo walizaliana sana kwa sababu chakula kilikuwa kingi sana.
Soma Mwanzo 7:1-9:25.
 
Mambo ya imani magumu sana maana kuna sehemu huhitaki kuhoji ni kusadiki tu
 
Kwa muda sasa najaribu kujiuliza hili swala kwamba Bahari ilikuwepo tangu kuumbwa kwa hii dunia ila maji yalioangamiza kizazi cha enzi za Nuhu yalipotelea wapi katika uso wa dunia au ndio kusema kina cha bahari kiliongezeka?

Mwenye uelewa juu ya hili naomba anisaidie.
Jibu kwanza swali hili: maji yaliyofanya hiyo Safina ya Nuhu ielee yalitoka wapi?
 
Ukitaka kujua uwezo wa watu kufikiri wewe soma tu mada kama hizi ndipo utaweza kushangaa sana....

Mtu anahoji jambo lililotokea miaka maelfu huko utadhani limetokea mwaka jana. hivi ni kweli hatujui kabisa kuwa kulikuwa na tofauti kubwa sana ya kimazingira na hali ya hewa kipindi kile na leo?

Hata hivyo,unapohoji na kujibu masuala ya ki-Biblia unapaswa ufikirie kwa namna ambayo siyo sawa na hii ambayo unaifikiria kwenye aisha ya kawaida kwasababu kuna mambo yaliyoko kwenye biblia ambayo hayawezekaniki kwa namna ya kawaida kwasababu mtendaji hafungwi na kanuni zinazokufunga wewe....

Sasa kama mtu anahoji namna wanyama wanaoishi kwenye mazingira fulani kuweza kuishi kwenye safina ambayo haina mazingira hayo huyo ni moja kwa moja anafungwa na kanuni ambazo aliyewafanya wanyama hao wakaishi kwenye safina hafungwi nazo....

Hilo ni sawa na kuhoji walichokuwa wanakula wanyama siku zote,yaani ni kichekesho kikubwa kabisa....

Hujui tu kuwa kuna mwanamama mmoja alitumia unga kidogo sana aliokuwa nao bila kuisha kwa siku mingi tu,jambo ambalo haliwezekaniki kwa akili zako za kawaida ambazo kwa kiwango kikubwa zimejengwa na mazingira na jamii yako na hivyo kuzifanya kuwa ziyo zako.....

Tunashindwa kuelewa hata mambo madogo kama haya,inasikitisha sana....
Mkuu pokea mkono wangu popote ulipo.
Kweli biblia ni ngumu kuielewa kwa sayansi ya mwanadamu
Lakini kwa kweli climate change is real. Mi na umri huu wa under 35 nimeshuhudia maeneo yaliyokuwa yanapata mvua august to Jan usiku na mchana sasa ni ukame wa kutisha, vipi miaka 1000 iliyopita ilikuwaje.
 
Yange evaporate bado yange kuwa kwenye system ya dunia sasa hayapo ndio maana mtoa mada anahoji yalienda wapi.
Mambo ya Mungu si ya kuhoji kwa akili za kibinadamu!!!
Ni kama kuuliza moto uliounguza sodoma na gomora ulitoka wapi!!!
Bahari iliyotenganisha ili wanaisraeli wapite kipindi cha Musa ilishikiliwa na nini?
Ni kama kuhoji uumbaji pia!!!

The acts of God cannot be comprehended using human mind!!!
 
Nami naomba nikuulize,

Maji ya mvua ya El niño ya mwaka 1997/1998 yalienda wapi?
Kweli mkuu, kipindi kile nilishuhudia, kwa macho yangu mabonde yamejaa maji, hayavukiki ila leo hata tone hamna
 
Back
Top Bottom