DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hilo nalo ni neno au ni hoja yenye mashiko. Tena ikumbukwe samaki anakula pia vitu vingine ambavyo huenda navyo vimeshachafuliwa na vitu vinavyoweza kusababisha saratani.
Huku kwetu umasaini tunawapata pia samaki esp.sangara na sato kutoka Mwanza. Kwa hiyo na sisi pia tuko kwenye risky population.
Utafiti wa kina unahitajika.
 
Mtu yeyote anayeifahamu Formaline vizuri atakubaliana na mimi kwa harufu yake tu huwezi kutumia kuhifadhi nyama au samaki mteja asijue. Wauza nyama na samaki wana uhuni mwingi ila kwa hili la Formalin wanasingiziwa!

Aliyesoma Chemistry na ambaye amewahi kuiona Formalin atakubaliana na mimi.
 
Wahusika wakitaka wanaouwezo wa kujua kila kinachofanyika huko mabuchani !! Narudia Wakitaka !!
Hizi dawa za kutunzia maiti ni hatari sana kwa binadamu, na wavuvi huzipendelea. Madhara yatokanayo na matumizi haya ni mengi ukiachilia cancer.

Hili tatizo lilikuwa kubwa sana Uganda hadi serikali ikaingilia kati, na hii hali ikapungua. Given proximity na mwingiliano wa wavuvi wa Tanzania na Uganda, uwezekano wa hii tabia kuwa ime-spill over Tanzania ni mkubwa sana.

Kwendana na serikali dhaifu tulizonazo, Mwananchi ni lazima Abebe jukumu l afya yake 100%.
 
Kuna kitu nimeokota hapa, kimenitesa mda
Kipi hicho!!?

Au ni hiki;-

"Mama Samiah hoyeeeeh!

"Makamu wa Rais philip Mpango hoyeeeeh"!

"Waziri mkuu KASIM majaliwa hoyeeeeh!

Bwana asifiweeeeeh!

Mawaombea mh.Rais mama Samiah suluh,philip Mpango na KASIM majaliwa!!

Niishie hapo!

Una maanisha hivo!!?
 
Hapana mkuu
 
Majokofu ya ferry na airport ni Kwa ajili ya kusafirisha mikoa mingine na viwandani, samaki wa kuvuliwa na sumu labda.

Bt wamefanya narrow research na kujump kwenye conclusion .

CCM ni janga la Taifa. Ameeen
 
Maji ya kuoshea maiti ni maji ya kawaida tu..Hayana uwezo wa kuhifadhi kitu....
 
Ombea hata maharage maana ukinunua maharage Kwa mfanyabiashara anaenda Kwa mganga, hubadilika na kuwa mavi ya mbuzi. Shetani mbaya sana.
Mavi ya mbuzi ??! Sidhani hawana sayansi hiyo! Halafu unawakweza sana!! Hawana nguvu hizo ! Never !!
 
Mkuu umechanganya mada.

Siyo maji ya maiti, maji yanayotoka kuoshea maiti ni maji taka kama yalivyo maji yanayotoka bafuni baada ya kutumika.

Ile dawa inayotumika kuhifadhia maiti isiharibike, ndiyo dawa sasa inayotumika kuhifadhia samaki na wale watu wabinafsi wasiojali maisha ya wengine.

Kwake yeye ni: samaki asioze fedha ipatikane na si afya ya mteja!

Ni sawa na wakaangaji wa samaki Feri wanavyotumia mafuta ya mitambo ya transformer kukaangia samaki na kuuzia watu.

Hiyo biashara inaeleweka na hakuna hatua za maana serikali ilikwisha kuchukua kunusuru afya za watu wasioelewa chochote kuhusu kemikali hatarishi wanazolishwa na watu wasio waaminifu bila kufahamu.

Ukiangalia mfumuko wa gonjwa wa kansa hospitali ya Osheni road utasikitika, chanzo chake nini, ni haya matakataka wanayolishwa kila siku na watu wasiokuwa waaminifu.
 
Hayo maji yanatumika kivipi?
Kama wewe ni male mwanaume mtongeze demu anayeuza duka la nyama au samaki kwa mpemba atakueleza yote na kuyasifia.
Mbona hii kitu iko wazi Sana...ndio maana tunaambiwa tuombee vyakula hata kabla ya kuviingiza nyumbani.
 
Maslahi ya biashara za watu yameguswa! Wapuuzi wakubwa hao, ukweli sasa tunaujua, Mpango kasema wazi wazi.
 
Mavi ya mbuzi ??! Sidhani hawana sayansi hiyo! Halafu unawakweza sana!! Hawana nguvu hizo ! Never !!
Sawa vegetarian, sikutishi. Omba tu na Kila kiti kitakuwa sawa.

Nmekumbuka kiti, Mahindi usinunue unga, nenda nunua Mahindi halafu yaoshe mwenyewe ndo usage unga, Kuna dawa ya kuzuia wadudu kubungua pia husababisha saratani.

Ndugu vegetarian, hujiulizi APPLE linatoka south Afrika linakaa container zaidi ya mwezi Bado unalikuta fresh???
 
Naomba kuuliza,haya maji ya kuuoshea maiti,ni maji Dawa au ni yale maji yanyokusanywa baada kuoshea maiti na kuhifadhiwa?
Sio maji dawa, ni take yanayokusanywa baada ya kuosha maiti na kuhifadhiwa.
Kama upo Arusha nikueleze kibanda cha kwenda kununua ....@ opposite na na soko kuu kwenye vile vile viduka vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…