Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani

Labda kwenye sekta zingine lakini kwa wasanii hatuna, shoo zao utasikia sema yeeah
Bora wasanii hao kuliko kwenye sports, movies, professionals(doctors, engineers, journalists, authors, pilots etc) hata kwenye biashara kimataifa hatupo kabisa. Msanii wa music japo kiuhalisia tunaye mmoja tu anayepambana/anayepambanishwa kimataifa but against odds he is fighting.
Hatujawahi kuwa na basketball player let's wa hata kufikiriwa kupambana kiwango alichofika Hakeem Olajuwon au football player wa kufikiriwa kupambana kiwango alichofika Mikel Obi au Nwako Kano au JJ Okocha, Watanzania wengi wivu na hate ndiyo hufanya mtu anayepambana achukiwe.
 
Nakubali. Ni kama Fela Kuti alivyojulikana mpaka nje ya Nigeria. Identity muhimu sana.
 
Wakongo walishatoboa kimataifa Ndugu Mdau. Mpaka Bongo na Africa Mashariki yote walishaiteka kwa muziki wao. Kwa aina yao ya muziki wao ni bendi zaidi tofautisha na hiki kitu kinaitwa "muziki wa kisasa wa vijana" huu anafanya mtu mmoja jukwaani.
 
Unaambiwa mtanzania akiona fursa kwanza aipige yote iishe ndo anaita watu wawili watatu, kila mtu anataka ale peke yake
 
Tofauti ya diamond na hao ni nini kama wote hawajatoboa? If anything dayamondi kashinda tuzo zaidi na kupafomu kwenye stages nyingi zaidi.
usirudie tena kuwahusisha Bi.Kidude & Remmy Ongala na huo upuuzi mwingine.
Ndiyo maana nimekuuliza how old are you??

Yani unamtaja mr.nice kwenye list moja na Bi.Kidude na Remmy Ongalla alafu unauliza wameshawahi kufanya wapi show πŸ˜‚

Strictly Tanzania ndiyo mziki gani πŸ˜‚
 
Nakubali. Ni kama Fela Kuti alivyojulikana mpaka nje ya Nigeria. Identity muhimu sana.
Fella Kuti wakati anapiga shows MGM Grand Arena kina Marijani na Mbaraka Mwinshehe walikuwa wanapiga shows DDC Kariakoo au lango la Jiji au Amana Bar Ilala.
 
Umesema ukweli bado tupo kwenye kabox kadogo tunavimbiana tu tukitoka nje kuna vikubw azaidi yetu
 
Lugha nayo ni tatzo,kiswahili kina laana

Jk wa kwanza alaaniwe na hii lugha yake inayotudidimiza badala ya kutupaisha
Kuna wakati pia tukubali kwamba kuna watu wametuzidi vipaji naturally.... Kenya & Uganda wanaongea kiingereza vizuri lakini kimuziki tuko juu yao. USA na Qatar ni matajiri kupindukia ila kwenye riadha wanazidiwa na nchi maskini Kenya kiasi kwamba wanagawa uraia kwa wanariadha wa hiyo nchi tena kwa kuwashawishi. South Africa pamoja na utajiri wake ila kwenye mpira inakalishwa na nchi maskini kabisa. Mimi nadhani nchi iweke nguvu kwenye vitu ambavyo tuna vipaji navyo. Kwa mfano ndondi na riadha.
 
 
Kiswahili kinawamaliza Wabongo..Wabadilike Kiswahili hakilip saanaa
 
As long as wanapata hela na fame ya kuishi vizuri bongo hapa tuishi nao hivyohivyo lakini halo wajuba hatuwawezi kama huyu diamond wetu kwa sasa hasimami hata na fireboy
Kwanini Diamond? Kwanini usimseme Samatta kwamba hasimani kwa madogo wapya wa Kipopo wanaotingisha ligi za Ulaya?
 
Tuna Hashim Thabit jamani πŸ₯ΉπŸ₯Ή

Unayosema ni kweli uraia pacha una faida kubwa sana sijui kwanin wanabana natumain kwenye katiba mpya wataweka
Basketball players wa Kipopo wapo kibao na wanatingisha sana NBA.
 
We can only hope.

Thabeet alijaribu ila inabidi tuwe nao wengi.
Thabeet, Samatta na Diamond wamepambana kiasi chao lakini tungekuwa na wapambanaji wengi kwenye fani tofauti tofauti wangekuwa wanatiana morari.
Bado tuna safari ndefu sana kama point of reference tunayolazimisha kuitumia ni Nigeria, ukiacha connections zao, aggressiveness yao, exposure yao pamoja na pesa wanazowekeza wenyewe kwenye kila idara walikuwa juu tangu miaka mingi iliyopita hivyo wanasaidiana na kuonyeshana njia ili kupunguza vikwazo vya njia ya kufika kwenye mafanikio.
 
Kwanini Diamond? Kwanini usimseme Samatta kwamba hasimani kwa madogo wapya wa Kipopo wanaotingisha ligi za Ulaya?
Katika sentensi yangu nimeongelea muziki mkuu, ndo maana nimemtaja yeye kama top artist wetu, huo mpira siuelewi ndugu
 
Mkuu sema una chuki na vijana wa music wa sasa, sasa unabisha diamond kuperform platform ya Grammy?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…