Ndio maana nikasema mambo yanayoiheshimisha wilaya Kinondoni
Hivyo vitu vya kawaida kwenye nyumba za kupanga
Ila ndo hivyo wilaya ya Kinondoni ni zaidi ya wilaya ya Temeke katika nyanja nyingi tu
Kinondoni maeneo duni yapo mengi tu pia TEMEKE maeneo ya watu wakipato Cha Kati na Cha juu tu yapo mengi semaa hauijui Temeke,unapajua mbagala tu
...mfano was maeneo duni Sana ya kinondoni
1)
.Kawe Mzimuni uswaz Sana pameachwa mbali Sana na Mbagala yote kwa Ujumla
2.Tegeta kwa Ndevu eneo la Msichoke ni hatari na ukabaji ni Jambo la kawaida hakuna Barabara za kupita mavi hovyo hovyo kutapakaa mitaani Miguu ya kuku na utumbo kawaida Sana
3.Tegeta Machinjoni mpaka Uwanja wa Panga ni hatari tupu hapafai kwa Maisha ya binadamu vibaka ni Wengi wanakaba mpaka Mchana
4.Kunduchi Mtongani ni Uswazi hasa hata viwanja Bei rahisi Sana no value at all. Huko Panya road normal Sana.
5.Bunju Usalama yaani ni Vituko tupu hapo wamechanganyika Malofa na wanaojiweza
6.Mbweni Maputo huko ni hovyo sijawahi Maisha ya ajabu Kama hayo hapa Dar es salaam
7.Msasani Maandazi Road Kama unataka kwenda shoppers hakika nawaambieni Mbagala Ipo juu Sana kuliko Hilo eneo yaani ni chafu Sana muda wote linanuka tope na vinyesi
8. Kinondoni Shamba yaani ni Uswahilini iliyopitiliza Hali ya kawaida
9.Mwananyamala kuanzia kwa sindano,kidile,Manjunju, Mama yako yaani ni Uswahilini huwezi amini macho yako kukabwa na kuvunjiwa ni kawaida