Majibu ya Rais Samia Suluhu hata Kama yangekuwa uongo lakini Yanaridhisha

Upinzani hawana Agenda wanayoipigania.

Ni Kama ngedere anayerukia Tawi hili na hili

Kama wangekuwa na Agenda moja wakaipigania mpaka ikakamilika huenda wangekuwa mbali.

CCM wanachoringia ni kuwa na Upinzani dhaifu sana
Huu ndio ukweli.

CCM hawaringii polisi wala Tume ya Uchaguzi, wanachoringia ni kuwa na UPINZANI DHAIFU SANA.
 
HUYU SAMIA NI MUONGO, ANATAKA KUTUAMBIA UCHAGUZI ULIOPITA ULIKUWA HURU NA WA HAKI? WANACHOLALAMIKA HAO WAPINZANI KUBWA ZAIDI NI KUWA NA KATIBA ITAKAYOONDOA BIASNESS KWENYE HII TUME YA UCHAGUZI YA OVYO. NDIYO WATU WATASUBIRI SEHEMU NYINGINE YA KATIBA, LAKINI HILI LA TUME HURU, WEWE SAMIA UNATAKIWA ULIFANYA SASA, HUPENDWI WEWE NA SERIKALI YAKO, KWANINI MNALAZIMISHA MPENDWE????
 
Sasa ndio maana watu tunasema kwamba wanaodai katiba wanadai kwa maslahi yao ndio maana tunaona wanapiga kelele.

Kelele iliyokuwepo ni tume huru tuuu hayo mengine ni kuzuga tu,wanakatiba mpya wasiwatie wananchi katika ajenda zao za kimaslahi aisee.
 
Mbowe ana Uhuru wa kufanya na kudau kitu chochote kile, kudai katiba mpya haijawahi kuwa kosa la jinai acha ujinga
 
Mimi binafsi nilihoji toka mwanzo kwamba mnataka katiba mpya ili iweje?

Sijawahi pata majibu toka kwa machadema
Muulize kikwete kwanin alihidhinisha zile ela za tume ya katiba ya warioba kuzunguka nchi zima na bunge la katiba umeuliza swali la kijinga Sana
 
Sasa ndio maana watu tunasema kwamba wanaodai katiba wanadai kwa maslahi yao ndio maana tunaona wanapiga kelele.

Kelele iliyokuwepo ni tume huru tuuu hayo mengine ni kuzuga tu,wanakatiba mpya wasiwatie wananchi katika ajenda zao za kimaslahi aisee.
We ni mjinga sana, kulikua na haja gani kuwa na bunge la katiba na kuanzisha Ile tume ya warioba ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya na husu Samia naye alishiriki
 
Mwenye rasmu ya katiba iliyopendekezwa anipe ili nione kama naweza unga tela la katiba mpya
 
Mimi Mkristo na ninakubaliana na Samia
 

Unaweza kuwa sahihi, ndio maana nikasema hata Kama ni uongo lakini unaridhisha
 
Mambo mazuri yapi watu wamekaa miaka 60+ still wanafunzi wanakaa chini mazuri yapi ambayo hayaonekani
Kama unaamini hakuna mazuri sawa.

Mimi mazuri nayaona yamefanyika japokuwa ninatamani yafanyike zaidi,wewwe huoni mazuri yoyote yaliyofanyika ati kwa sababu tu kuna mambo mengine hayajafanyika.

Hakuna ugomvi mkuu,wewe endelea kuona mabaya,ssi wengine tutaendelea kuona mazuri.

Chaguo ni lako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…