Majibu ya Rais Samia Suluhu hata Kama yangekuwa uongo lakini Yanaridhisha

Lini ulilazimishwa na nani aliyetulazimisha? Tuwekee huu ushahidi husika.
 
Wanakatwa kwa ridhaa yao?
Pengine wapo walioridhia na pengine wapo ambao hawajaridhia na wala kukubaliana na hali.

Hivyo suala libaki kila mtu ajisemee mwenyewe,kama mimi nimeshakubaliana na hali
 
Interview ya Salim Kikeke na Samia jana imefanya mambo makuu manne yafuatayo:

1.Imemfunua Samia ni nani,anataka nini na ana mpango wa kuifanyia nini Tanzania.Imemfunua kuwa ni dikteta muoga na asiejiamini.

2.Imemshusha Salim Kikeke kupindukia.

3.Imeumiza image ya BBC.

4.Imedhalilisha waandishi wa habari.
 
Pengine wapo walioridhia na pengine wapo ambao hawajaridhia na wala kukubaliana na hali.

Hivyo suala libaki kila mtu ajisemee mwenyewe,kama mimi nimeshakubaliana na hali

Ww ni mfaidika wa hizi tozo kandamizi, hivyo huwezi kuacha kuridhika.
 
We jamaa naona umeandika kutokana na mahaba yako au ndio mwisho wa uelewa wako ukiangalia kiundani yale mahojiano yameacha maswali mengi kuliko majibu. Pia yameonyesha namna uongozi tuliona unavyoyachukulia mambo yeye maslahi ya kitaifa katika mtazamo finyu, nikiongelea kwenye hizo point zako mbili ulizochukua÷suala la mikutano ya kisiasa na suala la kukamatwa kwa Mbowe
*Suala la mikutano, kwamba mikutano haiko kikatiba ila inaruhusiwa iwapo imeorodheshwa katika katiba ya chama husika pia inatakiwa ipate kibali cha polisi Sasa suala la kujiuliza Je vyama vya siasa kazi yake nini na vinafanyaje kazi, je sheria ya vyama vya siasa inasemaje kuhusu mikutano ya kisiasa na ni wakati gani inatakiwa ifanyike, ni wakati wa uchaguzi kutoa elimu kwa wapiga kura au wakati mwingine wowote baada ya uchaguzi ili kutoa elimu ya uraia na pia kushawishi watu ili kupata wanachama wapya?, Pia kuhusu kibali cha polisi,je polisi kazi yake kutoa kibali au kuamua kukataza au kukubali mikutano?
*Kuhusu suala la kukamatwa kwa Mbowe,kwamba alikua na kesi toka mwaka jana na wenzie walishakamatwa na walishaukumiwa, Sasa wenzie waliohukumiwa ni wakinanani, kwanini Mbowe hakukamatwa toka wakati huo akamatwe Sasa?
Kwa maoni yangu naona mama amepuyanga kwenye hayo mahojiano kwa sababu majibu yake mengi yalikua mepesi Sana pia yalikosa rejea ie kikatiba,sheria, takwimu au tafiti na pia ninavyoona siasa za Tanzania ziko biased Sana maana tunaona chama tawala wanafanya siasa za uhuru zaidi kwa kimvuli Cha serikali huku upinzani wao wanapigwa Sana danadana
 


Maswali yalikuwa rahisi mno
 
Kuna tatizo gani upinzani wakiwa na agenda zaidi ya moja wanazozipagania katika nchi?

Upinzani hauwezi kupigania agenda ya katiba mpya, uhuru wa habari na tozo za miamala ya simu kwa pamoja?
Upinzani hawana Agenda wanayoipigania.

Ni Kama ngedere anayerukia Tawi hili na hili

Kama wangekuwa na Agenda moja wakaipigania mpaka ikakamilika huenda wangekuwa mbali.

CCM wanachoringia ni kuwa na Upinzani dhaifu sana
 
Kuna tatizo gani upinzani wakiwa na agenda zaidi ya moja wanazozipagania katika nchi?

Upinzani hauwezi kupigania agenda ya katiba mpya, uhuru wa habari na tozo za miamala ya simu kwa pamoja?

Sijakataa.

Ila wapiganie chenye soko si unajua Siasa pia ni Kama biashara
 
Na wewe unampinga SSH kwasababu siyo dini yako ?
 
Unaweza kuwa sahihi, ndio maana nikasema hata Kama ni uongo lakini unaridhisha
Hivi wewe ukoje, tangu lini majibu ya uongo yakaridhisha? Au ni yale mambo ya Zanzibar kuwa tumefungwa lakini chenga tumewala? Acheni uswahili simamia haki wewe.
 
Hivi wewe ukoje, tangu lini majibu ya uongo yakaridhisha? Au ni yale mambo ya Zanzibar kuwa tumefungwa lakini chenga tumewala? Acheni uswahili simamia haki wewe.


Hujawahi ona Uongo unaoridhisha
Kisha ukakutana na ukweli usioridhisha?

Waulize Mahakimu na majaji watakuambia,
Au waulize waliopo ndani ya ndoa
 
Sasa mbona unang'nga'niza wawe na bidhaa moja tu?!
Bakheresa mwenye bidhaa za juice, ice cream, hotel, unga na media biashara yake sio sustainable ?
Kila kitu duniani ni Kama biashara tuu.
Angalia soko linahitaji nini ili Biashara iwe sustainable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…