Mbona wagombea wameridhika kutokutimiza masharti wewe una shauri nini hapa.

Ukiacha wachache walionunuliwa na wagombea wa CCM ila wengi ni figisu za POLICCM/NECCM kwa maelekezo ya wagombea CCM ,Nilimuona Devoth Minja alivyokuwa anapambania haki yake. Sidhani kama ni kweli hajapeleka picha katika form zake.
 
WABUNGE WA CCM WALIOPITA BILA KUPINGWA UBUNGE

1. Hamis Taletale (Babu Tale) (Morogoro Kusini Mashariki)
2. Alexander Mnyeti (Misungwi)
3. Prof. Palamagamba Kabudi (Kilosa)
4. Abdulaaziz Abood (Morogoro)
5. Japhet Hasunga (Vwawa)
6. Shanif Mansoor (Ngudu, Kwimba)
7. Ahmed Shabiby (Gairo, Morogoro)
8. Kassim Majaliwa (Ruangwa, Lindi)
9. Jonas Vanzland - (Mvomero, Morogoro)
10. Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini)
11. Joseph Kamonga (Ludewa)
12. Elias Kwandikwa - (Ushetu, Simiyu )
13. Nape Nnauye - Mtama, Lindi
14 . Job Ndugai (Kongwa)
15. Anthony Mavunde (Dodoma Mjini)
16. Deo Ndejembi (Chamwino, Dodoma)
17. Dk Ashatu Kijaji (Kondoa)
18. Vita Kawawa (Namtumbo)
19. George Malima (Mpwapwa)
20. Geofrey Mizengo Pinda ( Kavuu )

Kwa kilichofanyika au kilichofanywa wala haiitaji Akili kubwa sana kuweza kujua kuwa 'Bwana Mkubwa' anawahitaji sana kwa 2020 hadi 2025 yake.
 
Safari ni ndefu na vikwazo ni vingi.

Kama tutafika basi kwa tabu sana.
 
Na Kama Raisi atakuwa Mh Lisu?
 
Ccm 20 chadema 0
.
Hivi ushindi wa Lisu unatokea wapi?
 
Katika jimbo lililoniuma ni Dodoma Mjini, pale alipaswa CHADEMA isimamishe kwa gharama yoyote kwa ajili ya kulibeba 2025 ukizingatia wahamiaji ni wengi hivyo kuchochea mabadiliko.
Kulipoteza hili jimbo litakua na madhara kma yaliyotokea kupoteza jimbo la Nyamagana, itakua ngumu mnoo kulirudisha upinzani.

Dk Slaa kwenye majimbo ya kimkakati alikua vizuri naona Mnyika amepwaya sana hapo.
We can't afford to lose Dodoma Urban for christ sake!! Ni future political base.
Cc CHADEMA
 
Mwana kiona mbali Gentamycine, kwa maana nyingine hao ndio team ya campaign itakayozunguka na JPM kumnadi nchi kotemaana kwao uhakika tayari
 
Ccm 20 chadema 0
.
Hivi ushindi wa Lisu unatokea wapi?
Felix Tshisekedi alitangazwa ni Rais akiwa na wabunge wangapi? Trump je? Jiulize upinzani ulipataje kura million 6 ilihali wabunge wake hawakufika 30% ya bunge zima la 11?
 
Ushindi wa Lissu upo kwa wananchi
Wananchi wenyewe hawa waliomkataa Lisu kabla hata ya kampeni?

Nenda kwenye page zao huko facebook uone wanavyoshambuliwa hao wagombea wako
 
Sasa huyo wa jimbo la Mvomero-Morogoro mbona jina lake halifanani na jina la Mwafrika yeyote popote duniani. Au suala la kuchunguza uraia wa watu linatokea tu pale ukisema umenikanyaga naomba uondoe mguu...
Ni mzungu mtanzania alikuwa Diwani kafanya makubwa Sana mvomero

Tanzania Ina waafrika Weusi waarabu, wahindi na wazungu au hujui hilo?
 
Felix Tshisekedi alitangazwa ni Rais akiwa na wabunge wangapi? Trump je? Jiulize upinzani ulipataje kura million 6 ilihali wabunge wake hawakufika 30% ya bunge zima la 11?
Kwanza Tsheked hakushinda bali ule ulikuwa mpango wa Kabila,
Na mpaka sasa hivi Kabila bado ana mamlaka pale Congo kama hujui.
 
Sasa Lisu unamlinganisha na Lowasa kweli?
Hujaelewa swali? Logic ya kura za Urais na mgombea ubunge zinacorrelation?

Kumbuka kura za Urais unazoa majimbo yote ila kiti cha ubunge ni mpka uongoze kura jimbo husika.

Pia majimbo yana disparity, mfano majimbo ya Dar pekee yanaamua almost 15% ya kura za Urais ingawa haitoi wabunge zaidi ya 10. But majimbo ya zenji yanatoa 2% ya kura za Urais ila yanatoa wabunge 50??
 
Mkuu tutarudi hapa baada ya oktoba kubishania wizi wa kura kama kawaida yenu
 
Aisee wapinzani wamepigwa vibaya mwanzoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…