Majimbo ya Ubunge yaliyosimamisha wagombea wa CCM bila wagombea wa Upinzani
Sai pande za south ni mwendo wa kupita bila kupingwa aisee[emoji23][emoji23]

Sababu kuu eti hawakukidhi vigezo, sasa kinachonishangaza mimi eneo bunge atakosekanaje mtu mwngine kando na ccm anayejua kusoma na kuandika.

Manake pande za south kigezo kikuu ni kujua kusoma na kuandika tu, mengine ni mambo madogo, kama vile ukiwa mnyonge mwenzio anakuminya hadi ukubali.

Yaleyale ya serikali za mitaa ya 99%, kw mwendo huu tuzo la udikteta anapewa jiwe.

Wewe lockdown ya hapo Kenya naona imekulevya.

Si bor siasa za bongo kuliko za hapo kwenu za kikabila?
 
Tumia akili, sio kila chama kimesimamishwa wagombea majimbo yote
Kwahiyo wagombea wa ubunge vyama kumi 15 jimbo la mtama kwahiyo hakuna hata mmoja aliyejua kujaza fomu au kufika kwa muda Amejua nape pekeyake jami munacheza na sindano ktk jicho
 
Yeye anajua hawezi kushinda ndio maana hajataka kuhangaika
Benson Kigaila - Naibu Katibu Mkuu CHADEMA nakulaumu sana kwa hili. Ungerudi tena hapa jimboni wananchi wako tulikuwa tayari tumejipanga kukupigania. You deserve it ila sijui ulikwamia wapi tu. Saa nyingine wapinzani tunashindwa kwa sababu ya mikakati tu
 
WABUNGE WA CCM WALIOPITA BILA KUPINGWA UBUNGE

1. Hamis Taletale (Babu Tale) (Morogoro Kusini Mashariki)
2. Alexander Mnyeti (Misungwi)
3. Prof. Palamagamba Kabudi (Kilosa)
4. Abdulaaziz Abood (Morogoro)
5. Japhet Hasunga (Vwawa)
6. Shanif Mansoor (Ngudu, Kwimba)
7. Ahmed Shabiby (Gairo, Morogoro)
8. Kassim Majaliwa (Ruangwa, Lindi)
9. Jonas Vanzland - (Mvomero, Morogoro)
10. Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini)
11. Joseph Kamonga (Ludewa)
12. Elias Kwandikwa - (Ushetu, Simiyu )
13. Nape Nnauye - Mtama, Lindi
14 . Job Ndugai (Kongwa)
15. Anthony Mavunde (Dodoma Mjini)
16. Deo Ndejembi (Chamwino, Dodoma)
17. Dk Ashatu Kijaji (Kondoa)
18. Vita Kawawa (Namtumbo)
19. George Malima (Mpwapwa)
20. Geofrey Mizengo Pinda ( Kavuu )

Kwa kilichofanyika au kilichofanywa wala haiitaji Akili kubwa sana kuweza kujua kuwa 'Bwana Mkubwa' anawahitaji sana kwa 2020 hadi 2025 yake.
Najaribu tu kuangalia majina ya ndugu zangu;
1. Kawawa
2. Nnauye
3. Ndejembi
4. Pinda
Nk. Najiuliza tu kwanini na urais wasiwaengue na wakapitishwa watakiwao bila kupingwa ili watu wasiumie wala kuumizwa na demokrasia yetu?
Je wabunge hao waliopitishwa bila kupingwa watajiona mahodari na kiwango chao cha kukubalika majimboni hakitakuwa na mashaka?
NEC wangelikuwa na akili na wenye weledi wangelidanganya toto kwa kupitisha pasi kupingwa na wabunge wa upinzani ili tuone maajabu!!
 
Felix Tshisekedi alitangazwa ni Rais akiwa na wabunge wangapi? Trump je? Jiulize upinzani ulipataje kura million 6 ilihali wabunge wake hawakufika 30% ya bunge zima la 11?
Mkuu kwa tume ipi lakini ya kumpa urais mpinzani? Ikiwa ubunge "zinduna zimeanza!" Je wakati wa matokeo ya kura hali itakuwaje?
Kwaheri upendo, kwaheri mshikamano wetu!!
 
Hadi sasa NEC 18 upinzani 0. Apo bado policcm na upinzani, refa akiwa NEC
 
Hivi kichwa cha thread hii ni sahihi? Ni kweli wapinzani hawakuweka WAGOMBEA?
 
Ningekuwa mshauri wa Lissu ningemshauri aachane na mashauri ya kuwekea pingamizi.

Asiwaige waliozoea vya kunyonga. Mwanaume mzima anaratibu mpinzani wake atekwe ili apite bila kupingwa.

Wanaume wa namna hii wanakosa uhalali wa kujiita wabunge wa jimbo ili hali hajachaguliwa.

Cha kushangaza, hadi waziri mkuu naye anatamani asipingwe. Jamani, mambo yote ambayo serikali ya awamu ya tano imetekeleza tena chini yake, leo hii anatafuta ubunge wa viti vya mapingamizi.

Ndugu JPM, nakushauri, kama huyu waziri mkuu atapita kwa fadhila za viti maalum vya mapingamizi, hafai kuendelea kuwa waziri mkuu, na anakidharilisha CCM.

Ni aibu kubwa kwa wagombea wa CCM wanaowaza ushindi wa mezani au wa sitting room. Ni aibu.

Matendo hay yanayofanywa na wagombea wachache unakipotezea mvuto chama.

Tukutane kwenye kisanduku cha kura

Maendeleo hayana chama
 
Ni mzungu mtanzania alikuwa Diwani kafanya makubwa Sana mvomero

Tanzania Ina waafrika Weusi waarabu, wahindi na wazungu au hujui hilo?
Hao wapo popote pale ila angekuwa upinzani lazima angewekewa pingamizi.
Wangeanza sio raia wa Tanzania mara lete vyeti vya kuzaliwa babu, bibi, mama,baba.
Nina hakika unaelewa vyema mazingira ya siasa zetu za bongo hususani uwe chama cha upinzani.
 
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mvomero Mkoani Morogoro,Hassani Njama amethibitisha kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Jonas Van Zeland amepita bila kupingwa baada ya kile alichotaja ni kutokana na Wagombea wa Vyama vingine kutokidhi baadhi ya vigezo
Ila wa CCM wamekidhi vigezo vyooote pasipo mashaka!!! 😀 😀 😀
 
Mkurugenzi wa Tume amesikitishwa na kitendo cha wakurugenzi wa Mikoa kutangaza baadhi ya wagombea wamepita bila kupingwa, wakati huo huo anasema Hana taarifa zakuenguliwa baadhi ya wagombea, wakati huo huo yeye ndiye bosi wa uchaguzi nchini.

Najiuliza Hawa watu wanasomana au kila mtu anafanya kwa utashi wake? Kama mkurugenzi wa Tume anashindwa kuwasimamia watendaji wa chini Ni vipi anaamini taarifa wanazomletea?

Huwezi kuwa na tume yenye wagombea nchi nzima then ukawa na watendaji waliokaa makao makuu pekee na ukategemea ufanisi.

Maamuzi yote yaliyotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi majimboni na kata yalikuwa batili na yalitangazwa kinyume cha sheria.

Sheria sheria sheria sheria sheria sheria
 
Nyie ndio mnajua sheria, acheni mambo ya kulazimisha jambo liwe mnavyotaka.

Mnaingilia utendaji wa taasisi na kutengeneza taharuki za kishamba katika jamii.

Wamiliki wa vyombo vya habari inatakiwa wawe makini katika kipindi hiki na muda wote, mtakuja mlie na kusaga meno.
 
Waambieni wagombea wenu wawe makini kwenye ujazaji wa forms hapo 2025.

Ishatoka hiyo
 
Back
Top Bottom