Majina yangu matatu kamili yametoka katika walioitwa kazini na sikuomba, hii imekaaje?

Majina yangu matatu kamili yametoka katika walioitwa kazini na sikuomba, hii imekaaje?

Nenda tu, uyo unaefanana nae jina hana nauli yakwenda huko dodoma, hiyo ni bahati yako mkuu
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?

Majina yako ni ya kiarabu pekee au ya kizungu/kiingereza pekee?
Au mchanganyiko?
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Kama nafasi husika unaimudu na vyeti unavyo nenda Dodomz na vyeti vyako uchukue barua. Utumishi wana majina ya watu wote waliomaliza vyuoni na sekndari. Hii bahati yako. Vinginevyo kuna mtu alifoji vyeti vyako akaomba kazi akapata sasa hawezi kwenda kuchukua barua. Wewe ndiwe unastahili. KACHUKUE URIPOTI KAZINI.
 
Unapoomba kazi kuna ile hatua ya kuweka picha baada ya process za kazi huoni kama ile picha imefanya kazi yoyote. Sasa situation kama yako ndio ile picha itakuja kuamua nani ni nani? Pamoja na hivyo kuna NIDA namba unaweka, We nenda kachukue barua mkuu. Kesi za udanganyifu zinaanziaga mbali sana sio tukio la siku au masaa machache
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Kwa majina yenu ya kiisilamu, si kitu cha ajabu akina Said Ahmed Mohamed wakawepo wanne katika mtaa mmoja.
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Shida ipo tena kubwa tuu.
1. Je, kazi uliyoitiwa ndo uliyosomea?
2. Kabla hujaenda; Wasiliana na wanaokufahamu au mahali ulipoomba mtu akupe connection
3. Majina yamefanana, Taaluma imefanana? Hata picha vimefanana, na namba ya NIDA vimefanana?.
Mwisho: Ikija kubainika sio wewe Sheria itakupasa.
 
NASHUKURU KWA MAONI YENU...SIENDI KUDHULUMU HAKI YA MTU...
 
NASHUKURU KWA MAONI YENU...SIENDI KUDHULUMU HAKI YA MTU...
mkuu ww una uhakika gani huyo mtu ni haki yake vp kama alipata copy ya vyeti vyako huko kwenye photocopy au stationary ulipoenda kuscan vyeti vyako nae akachukua copy kisha akaenda kutengenezea vyeti vingine feki na akaviscan tena kwa picha yake au hujui mjini hapa kila kitu kinawezekana muhimu pesa yako..hiyo haki yake anaitoa wapi huyo mtu au ukute hana vyeti original hivyo hawezi kwenda huko ila ukienda ww hutaulizwa na mtu zaidi ya kusaini document tu..nenda kajaribu
 
Kabisa...
 
Mmefanana mpaka majina ya ukoo? Au ndio mariam Abdul mohamed. Hapo lazima utakutana na mwingine mwenye jina kama hilo. Usiende
Kwa waislamu, wengi hawatumii majina ua ukoo. Utaona tu;
1. Juma Ramadhani Mohamed
2. Yasin Ally Juma
3. Omari Said Abdallah

etc
Wa hivi kufanana majina matatu ni rahisi mno. Nenda pale hopitali ya Muhimbili (Dar), wale wa pale registration au wanapoanzia watu wa NHIF, manesi au wafanyakazi wa pale wanapata shida sana..!! Sababu ni majina ya hawa Jamaa wasiotumia majina yao ya ukoo. Kuwapata watu wanaofanana majina yote matatu kama haya hapa chini ni kazi sana;
1. Jakaya Mrisho Kikwete
2. Zainab Juma Massawe
3. Mwanhamis Said Mbwambo
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Inawezekana hasa wenye majina matatu ambayo yote ni kama first name. Yaani hakuna jina la ukoo kama Moshi, Mkandawile, Mwamfupe, Ngonyani, Msambichaka etc. watu wenye majina kama Abdalla Yasin Juma, Ally Mohamed Mfaume, Mariamu Juma Yahaya etc..!! Wa hivi kufanana nje nje.

Swali, je majina yako mamatu, kuna la ukoo kama Mtweve, Tweve, Komba, Nkondokaya, Lyoba, Mfinaga etc?
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Kule watakuuliza anuani mkuu.

Hapo ndio msiba utakapoanzia.
 
Inawezekana kuna mtu majina yake yote yanafanana na yangu?

Inawezekana nikienda kuchukua barua DODOMA, nikipewa italeta shida gani?
Kama uliwahi kupiga interview ya nafasi fulani hapo awali hukipata wana tabia ya kutoa majina kwa nafasi zingine bila wewe kuwa na taarifam hata mdogo wangu alipata kazi kwa style hii
 
Back
Top Bottom