Oscar Lyrics
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 3,011
- 5,188
Jirani kama jirani ni mtu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku hasa hasa kama ikitokea mkawa mnaelewana vizuri.
Mnaweza kushirikiana katika shida na raha, wakati mwingine jirani yako anaweza kuwa msaada mkubwa kuliko hata ndugu yako wa damu.
Pamoja na yote hayo wakati mwingine inaweza kutokea jirani akageuka kuwa kero au hata adui mkubwa, akatamani hata kukuona ukipitia changamoto mbalimbali za kimaisha.
Mimi binafsi nimewahi kukutana na majirani wema sehemu mbalimbali ambazo nimewahi kuishi kabla ya kuhamia kwangu.
Lakini pia kuna majirani wakorofi, kwa mfano kuna mmoja alikuwa anafungulia Subwoofer utadhani kuna Disco au sherehe nyumbani kwake, ukimsemesha utakutana na maneno machafu hatari.
Kwa upande wako wewe, Unawazungumziaje majirani zako? iwe ni hasi au chanya, share tupate experience.