Majirani zako ni watu wa namna gani?

Majirani zako ni watu wa namna gani?

Nashukuru napendwa na majirani zangu, hata km ni WANAFIKI bas ni huko nje, mie hawajanigusa directly.

Hapa napoishi, tuko 4, ila nimezoeana na m1, hawa wengine ni salamu tyuuh, pia wao sio washindaji wa home, ni kutoka asubuhi kurudi usiku mkalii.

Kwa kifupi hapa jobless ni mie pekee, afu mie ni mdogo kwa wote, ko kuna ka favor wananipaga naenjoy.

Nawapenda majirani zangu. 😘😘😘
 
Wakati nikiwa single niliwahi kupanga nyumba moja ambapo kulikuwa na mpangaji mmoja wa kike naye alikuwa single. Mimi nilikuwa nimepanga vyumba 2 vinavyojitegemea- kimoja upande mmoja wa korido na kingine upande wa pili. Huyo binti yeye alikuwa na chumba kimoja. Kwa kuwa sikuwa na mambo mengi nilikuwa natumia chumba kimoja tu. Kingine nilikuwa nimeweka makochi tu, sikitumii. Hivyo kwa kuwa tulikuwa majirani wema nikaamua kumwazima yule binti kile chumba nilichokuwa sikitumii akitumie tu, kodi nikwa nalipa mimi kiroho safi tu, bila nia yoyote ovu iliyojificha.

Nikawa naendelea na mishe zangu. Nikitoka kazini najipikia msosi halafu najifungua. Sikuwa mtu wa stori. Mara chache tukikutana kwa bahati salamu na stori mbili tatu, huyo najifungia chumbani kwangu. Muda ulivyozidi kwenda Jirani akaona sitii "neno" ikabidi ajilipue mwenyewe. Siku moja ghafla nasikia kauli hii ambayo sikuitarajia kabisa: "Kaka naomba unioe basi"
Daa! Nilipigwa na butwaa.
 
Mkuu sasa ukuta ulishajenga kwanini umtoze hela tena?
Ndiyo utaratibu unaotumika pote huku HD (uswahilini) Chief!

Mtu akichangia gharama anakuwa sehemu ya umiliki hivyo atakithamini tofauti na cha bure tu.

Ujenzi tunafanya kwa kujinyima mno,tuchangiane tu.

Fikiria aliyekopa akajenga na bado anakatwa/rejesha!!
 
Nashukuru napendwa na majirani zangu, hata km ni WANAFIKI bas ni huko nje, mie hawajanigusa directly.

Hapa napoishi, tuko 4, ila nimezoeana na m1, hawa wengine ni salamu tyuuh, pia wao sio washindaji wa home, ni kutoka asubuhi kurudi usiku mkalii.

Kwa kifupi hapa jobless ni mie pekee, afu mie ni mdogo kwa wote, ko kuna ka favor wananipaga naenjoy.

Nawapenda majirani zangu. 😘😘😘
Pole kwa ujobless mkuu.
 
Mi ndo ata sijui maisha ya majirani zangu tofauti na salamu, huwa najifungia sana ndani! Kuna siku mpaka mwenye nyumba alinigongea anasema usije ukafia humo ndani kumbe nipo tu sipendi kukaa nje sipendi watu wengi pia😒
Mimi pia nina tabia kama yako, yani najisikia burudani nikiwa peke yangu, sijui kama hili linaweza kuwa tatizo la kisaikolojia
 
Mimi pia nina tabia kama yako, yani najisikia burudani nikiwa peke yangu, sijui kama hili linaweza kuwa tatizo la kisaikolojia
Ukiwa unaburudika ni sawa ila kama una stress inaaffect vibaya maana itakuletea emotional comebacks mbaya tu, or else uwe umekubuhu kuwa lonely.. sidhani kama ni tatizo kisaikolojia inategemea kama muda wote ndivyo ulivyo au mpaka upigwe na kitu kizito, (angalia tabia za introverts pia)

binafsi stress zinakuja na kuondoka nikiwa ndani tu nikiwa stressed ata kama sina msosi kamwe sitoki nje! Ntakaa ndani mpaka nikae sawa! Namaliza siku mbili ndani tu🤦🏽‍♀️
 
Yaani nikae ndani bila kupita mtaani kutaniana na wazee na kuwadanganya aisee siwezi ,lazima nitembee tembee nitaniane na watu hapo siku naiona iko sawa hata nisipokula yaani
 
Tunatofautiana mzee, wengine tunapenda kukaa ndani ata mtu akija kupiga hodi au anauza mbogamboga hatuitiki😬
Dah kweli kutofautiana aisee .
Mimi hodi ikipigwa nipo ndani nafurahi nimepata mtu wa kupiga naye story maana kama hayupo serious na baishara ataishia hapo hapo kwangu maana kama kuna umbea wowote wa mtandaoni nitampa na yeye nitataka anipe stori za huko atokako yaani kikubwa tubadilishane maneno .

Ni hapo wazee wa kijiji chetu wakaniita Google maana kila ninaloulizwa hakuna nisilolijua na pia napenda kila mtu apate habari niliyonayo hata kama ni uongo lazima niuweke tu ili siku iende vyema .

Anyway hongera kwa hiyo kariba yako
 
Mimi sijui hata majina yao na wao hawajui chochote kuhusu Mimi tena mmoja hata hatusalimiani na kuonana haizidi mara nne kwa mwaka.

Picha:Alinifuata akitaka kuunanisha ukuta/fence kwangu nikakubali ila tuchangie gharama pasu akaleta uswahili nikamwambia "JENGA UKUTA WAKO".

Kajenga ila tumekuwa maadui.😀😀
Nyie ndi wale majirani wakorofi, yaani umejenga ukuta na hutaki aunganishe wa kwake hapo? Eti unamtoza, WTF jirani wa hivi simtaki.
 
Dah kweli kutofautiana aisee .
Mimi hodi ikipigwa nipo ndani nafurahi nimepata mtu wa kupiga naye story maana kama hayupo serious na baishara ataishia hapo hapo kwangu maana kama kuna umbea wowote wa mtandaoni nitampa na yeye nitataka anipe stori za huko atokako yaani kikubwa tubadilishane maneno .

Ni hapo wazee wa kijiji chetu wakaniita Google maana kila ninaloulizwa hakuna nisilolijua na pia napenda kila mtu apate habari niliyonayo hata kama ni uongo lazima niuweke tu ili siku iende vyema .

Anyway hongera kwa hiyo kariba yako
😅 Dr ushalewa
 
Duhh watu mmebarikiwa aisee,binafsi siwezi aisee na sio kwamba siwapendi watu au vipi, sipendi tu kuongea nao tena especially watu ambao siwajui sina chochote cha kunifanya niwe karibu yao, sijui nipoje, yani kama hatuna connection huwa siongei ovyoovyo mpaka nikuzoee sana!
 
Niko ✌🏻 sana na majirani zangu, though kila mtu na mishe zake, tunakutanishwa na matukio, na hivi tuna umaja wetu wa majirani ambao upo well organised na una pesa ndefu hadi mda huu. Safi sana!!
 
Back
Top Bottom