Hata haya huoni? Hilo "hekaru" lilivunjwa na Waislam au na warumi? Lilivunjwa Mamia ya miaka kabla hata hajaja Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na alipokuja na Waislam wakapewa ardhi ile kutoka kwenye mikono ya warumi ,dini ya Nabii Sulayman (Amani iwe juu yake), Uislam, ikasimamishwa tena katika ardhi ile tukufu. Na hata hao mayahudi waliokuwa pale wakaishi kwa amani kuliko walipokuwa chini ya warumi.
Na Jerusalem ilikuwa chini ya Waislam kwa miaka mingapi kabla hao mazayuni hawajaja kuanzisha dola yao katika ardhi ile, mpaka useme Waislam ndio wanataka kujenga "hekaru" lao kwa nguvu? Kama kwamba ni wao ndio walifukuzwa Ulaya na Wazungu wakristo na wakawakuta mazayuni pale.
Halafu ni Waislam ndio wana haki zaidi na Sulayman (Amani iwe juu yake) kuliko mayahudi, bali wana haki zaidi kwa Musa (Amani iwe juu yake) na Mitume wote wa Bani Israil (Amani iwe juu yao) kuliko mayahudi ambao waliwakataa wote na kuwafanyia vitimbi, waliwatukana na wengine wanawatukana (ikiwemo Sulayman) mpaka leo, na wengine waliwaua kabisa. Na wakaikataa dini aliyowachagulia Allah wakatengeneza dini yao kwa matamanio ya nafsi zao.