Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

wasambaa kwa tabia hizo ndo wenyewe hao ukoo mzima utahamia kwa ndugu au kama mtoto wao kaolewa na mume mwenye unafuu wa maisha basi timu nzima itaweka kambi ya pre season hapo nyumbani
Kati ya vitu ambavyo Wasambaa hatujajaliwa, basi ni ubinafsi na uchoyo kwenye chakula. Ukioa/ukiolewa na Msambaa, kubali kuishi kijamaa.

Hayo ndiyo maisha ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia.
 
Dah, umeongea point Sana, Mimi sipendagi wageni kwangu, hila sasa itabidi niwe mkarimu kwakweli! Nikweli binadamu tuwe na Moyo wa kusaidiana
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚hao ni hatari sitosahau walivyonimalizia sofa zangu, tv inaangaliwa kuanzia 12 asubuhi mpaka ngoma tisa night kali kulala nalala kwa tabuu kisa wao
na sifa ya wizi na umalaya kwa wanawake!
 
wasambaa kwa tabia hizo ndo wenyewe hao ukoo mzima utahamia kwa ndugu au kama mtoto wao kaolewa na mume mwenye unafuu wa maisha basi timu nzima itaweka kambi ya pre season hapo nyumbani
hii n kweli hua nawaona wasambaa wakishuka kwny burdan,tashrif,nacharo, shambalai, ksk na kiluwa ase anashuka babu,shangaz, mamdogo, shemeji hapo kila mmoja kaja na vitoto vyake vitatu
 
Wachaga hawapo?
 
Kama unakwazika na ndugu kujaa kwako bila shughuli maalumu waambie live kuwa maisha ni magumu waende kwao wakajitegemee au waende Mombasa kuna vitu vya bure wapendavyo.
Kwanini upate shida na upo home kwako.
Speak out!!
Ukonga Mombasa hii hii nnayoijua mimi au Mombasa ipi mkuu?
 
Halafu unapata pesaaa mingi! japo unalisha kundi la watu!! pia ni ufahari kutegemewa na watu wakubwa kwa wadogo! wengiiii!! najisikiaga sana....

nilipo huku nje ya nchi ili mradi tu uwe Mtanzania ninakutunza bila shida na km unaanza maisha njoo kwangu ila usiwe mwizi nina uwezo wa kujua Mwizi ni yupi! lkn shambani kama kawaida!

usiwe mvivu kufanya kazi, za shamba /viwandani, hapa nina Mgahawa wangu utakula humo lkn lipa , nitakulipa posho ya chakula na kazi za kufua vyuma na kuosha magari! kama mia tano hivi! na shamba!

kulima shambani na kuvuna, ujenzi km hujui kujenga utakuwa kibarua wa mafundi kwenye kampuni yangu ya ujenzi!! mambo yako yakiwa safi tambaa!...ukiumwa wkt uko kwangu unatibiwa hospitalini kwangu unalipia!

Ukiona kulala chini huwezi nina milki Hostel utaenda hapo utalipia hela kidogo!! hata ndugu wa damu wakija kwangu mwendo ni ni ivoivo tu! so sinaga hasara!
 
Makabila ya watu wakarimu yote wanajali sana undugu, huwa hawajali sana vitu kama msosi, sijui maisha magumu wao ndugu akija nyumbani kwake anafurahi tuu wala haoni tabu.
Katika hili, Mungu atubariki Wasambaa kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…