Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla, amesema baadhi ya wanasiasa wanaoikosoa serikali wanapaswa kuwa wa kweli kwa umma, kwani nao wamefaidika na fursa mbalimbali ikiwemo kupewa vitalu vya uchimbaji kama wachimbaji wadogo katika eneo la Bukombe.
"Ukiwa unapiga kelele umekaa katika nyumba ya vioo usirushe maneno, Lema na Heche na wenyewe badala waseme ukweli wamepewa vitalu vya kuchimba kama wachimbaji wadogo huko Bukombe, na wenyewe wamepata Lema anatoka Arusha, Heche anatoka Mara Tanzania hii ni moja"