Makamanda tusitegemee Mbowe kudai Katiba Mpya. Tayari ameshaingia kwenye 18 za CCM

Makamanda tusitegemee Mbowe kudai Katiba Mpya. Tayari ameshaingia kwenye 18 za CCM

Mimi kuna mtu kabisa alinitamkia kuwa siku zote mbowe sio chadema miaka hiyo yote, yeye yupo pale kama kivuli.

Mtu huyo akaendelea kuniuliza maswali, akaniuliza je nina uakika mbowe alikuwa akilala selo? Za chini zinasema hakuwahi kulala selo hata siku moja.tunaona kapandishwa gari yanayojili huko ni siri.

Na ajaniambia si karudi uraian? Hawezi fungua mdomo wake tena, sana sana atapiga kelele zile za kawaida tulizozizoea.
Watu kutoka mbeya walikwenda kumsalimia mara kadhaa gerezani.

Kamanda asitiwe hila mbovu
 
Unadai kipya cha zamani tu kukitekeleza tumeshindwa. Sasa swali katiba hii inavunjwa kila leo kuna guarantee gani katiba mpya haitavunjwa.
 
Hivi Moshi wa kuni mbichi wa Mzee Polepole haujakuibua tu wewe mtoa hoja ?

Mazungumzo na maridhiano ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo yanayowazunguka wanadamu hasa hasa haya ya kisiasa.
Kaa hivyo ndivyo, kulikuwa na haja gani ya kusema "hatuwezi kumpa muda rais, tutamlazimisha ili tupate katiba mpya"
 
Yes coz amejua hata afanye nn katiba mpya haiwez kuja Kwa wakati huu

Sasa ulitaka afanye nn?

Ww unataka apambane na katiba mpya then anakaa jela wakati ww umekaa Tu home na familia yako
Kun watu walitaka yeye apambane wao wale kuku Canada
 
Wewe ni CCM, labda kuna wachache wasiolifahamu hilo ila wengi wanaufahamu u CCM wako.
Bora hata ungekuwa neutral kama majority walivyo humu janvini lakini wewe ni CCM through and through.
Pumbavu zako, yaani kusema kweli ndio nimekuwa CCM?
 
Katiba mpya itakuja muda muafaka kama tu wananchi wa makundi yote wataamua kuidai. Hatutaki katiba mpya ya kudaiwa na chama fulani au kundi fulani la wanasiasa Mwishowe kuleta katiba isiyofaa au kukwamisha mchakato na kututia hasara kwa misuguano ya kichama kama ilivyokuwa ktk mchakato wa awali ambao tulipoteza billions of money.

kwa sasa tujenge nchi tusonge mbele. Kila jambo litakuja kwa wakati wake; wakati haujafika.
 
Pumbavu zako, yaani kusema kweli ndio nimekuwa CCM?
Pumbavu wewe na mama yako mzazi, unapanic kuambiwa ukweli kwamba wewe ni CCM. Mbona unafahamika kitambo na hii si mara ya kwanza unaambiwa ukweli.
 
endelea sasa kudai katiba mpya kama siyo ccm achana na Mbowe
CCM huyo adai katiba mpya? kazi yake ni kushambulia viongozi wa CHADEMA na kupinga strategies za CHADEMA.
Angekuwa neutral at least ningemuelewa, lakini huyo CCM kindakindaki adai katiba mpya?
Tena mshauri ahamasishe ile rasimu ya Warioba ndiyo itumike kama reference kwa ajili ya katiba mpya kama atakubali, mpuuzi mmoja hypocrite tu.
 
Kaa hivyo ndivyo, kulikuwa na haja gani ya kusema "hatuwezi kumpa muda rais, tutamlazimisha ili tupate katiba mpya"
unafahamu ni sababu zipi zilizomfanya Mh. Rais kuamua kumwita Mbowe IKULU the same day alivyokuwa anatoka gelezani ili wazungumze? jitafakari kijana mambo ya siasa bado uko mchanga mno.
 
Mimi kuna mtu kabisa alinitamkia kuwa siku zote mbowe sio chadema miaka hiyo yote, yeye yupo pale kama kivuli.

Mtu huyo akaendelea kuniuliza maswali, akaniuliza je nina uakika mbowe alikuwa akilala selo? Za chini zinasema hakuwahi kulala selo hata siku moja.tunaona kapandishwa gari yanayojili huko ni siri.

Na ajaniambia si karudi uraian? Hawezi fungua mdomo wake tena, sana sana atapiga kelele zile za kawaida tulizozizoea.

Ila unashangaza Sana. Juzi tu hapa uliiandama CHADEMA kwamba ndio inamfanya Mbowe akae gerezani kwasababu CHADEMA ilikataa kumuombea msamamha Mbowe na kukata Mbowe asiombe msamaha.

Leo Mh Mbowe katoka gerezani kelele zimegeuka kwamba Mbowe sio mwanachadema.

Halafu hicho kimvuli Cha Mbowe kilikuwa wapi wakati Mbowe anatajwa kwenye madawa ya kulevya na bashite? au hicho kimvuli Cha Mbowe kilikuwa wapi wakati bilcanas ya Mbowe inavunjwa?. Unapoambiwa Jambo jiongeze.
 
Mbowe anazeeka sasa, yaani mpaka kufa awe anapigana tu na serikali wengine wasifie humu JF. Seif naye kabla ya kulala mavumbini alijionea azungumze tu na serikali na agongamishe miguu maana unasimama kutetea watu wasiojulikana watiifu kwa serikali.

Kweli kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sidhani kama ni kazi ya Mbowe kudai katiba mpya,ni jukumu la Kila raia mwenye akili timamu kudai jambo lolote Kwa mamlaka ambalo linaonekana halina maslahi Kwa ustawi wa nchi.......

Tz tumekariri vibaya kuona wanasiasa wa upinzani ndiyo wanaotakiwa kukosoa,kukemea na kuzisema kero za wananchi.
 
Wanasiasa wa Africa
Bado cheo serikalini tu
Popcorns

Tunapenda kukosoa wanasiasa wa upinzani lakini wakati wa madhira au tabu wanazopotia huwa tunawacheka na kuwatenga. Wakati Mbowe yupo ndani mlimuita Gaidi, leo katoka mnadai atapewa cheo serikalini. Tangu lini Gaidi akapewa cheo serikalini?.

Tuache unafiki wa kukosoa tu bila kuwa na uhalali wa kukosoa. Wenye uhalali wa kumkosoa Mh Mbowe ni wale waliokuwa kill siku wanaenda kuhudhuria kesi yake sio wewe ulikuwa kwenye Mambo yako, leo Mh Mbowe katoka unakuwa was kwanza kukosoa.
 
Mbowe alishaelekea kibra siku kadhaa kabla hajatoka jela!

Hii ya kumsifia sifia Samia na kumshukuru kwa kuonesha utu kwenye kesi yake wakati yeye ndio aliemfunga ilitqkiwa iwazindue machadema. Lakini watazindukaje? Akili hiyo wanayo?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app

Unapokuwa kiongozi inatakiwa uwe na diplomatic language. Ulitaka Mh Mbowe aanze kumporomoshea matusi Mama Samiah?. Rais Samiah ndio kamualika Mh Mbowe ikulu na Mbowe kumuelezea dukuduku zote alizonazo. Mbowe hana Cha kupoteza maana CCM uwe mstaarabu bado watakusumbua tu. Yeye ameamua kuushinda wema kwa ubaya.
 
Back
Top Bottom