Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Tamko lisilokuwa na nguvu halina maana bora angenyamaza tu.
 
Ni kweli wastarabu kama nyie mpo!
 
Mkuu usiwe mnyonge kiasi hicho
 
Vilikuwa juu sana kulinganisha wa wapi?..au kulinganisha na kipato chetu?

No zile bei zilikuwa fair bana..wabongo tuache hizo..mfano Ttcl mtu alikuwa anapata 1.2 GB kwa 1k tsh kwa siku tano,,hii ni ghali?
Mkuu, sihitaji kulinganisha na mahali pengine ingawa hata tungeenda huko takwimu rasmi zipo zinazoonyesha gharama zetu zilikuwa juu.

Mimi nimejikita kwenye gharama za maisha za Mtanzania na matumizi ya sasa ya kila siku ya data ambayo tumezoea.

Inabidi bei zizingatie kuwa siku hizi Watanzania wengi wanapata taarifa zao nyingi, ikiwemo kwa njia ya videos, kupitia mitandao. 1.5 GB ni ndogo sana hata kwa matumizi ya kawaida ya kufuata habari. Kwa maana hiyo watu wengi wanalazimika kununua vifurushi vipya kabla ya vile vya awali kuisha muda wake (hii ina maana kiwango cha vifurushi hakitoshelezi mahitajo yetu).

Mtazamo wangu, kwa wastani vifurushi vya data vingekuwa kama 2500/= kwa 10 GB na 5,000/= kwa Unlimited. Bado faida ingekuwepo na serikali ingepata kodi yake. Tatizo lililopo ni tamaa tu ya serikali.
 
Mi nadhani huyu waziri angejiuzulu tu maana huwezi kupewa mamlaka na ukachezewa na makampuni kiasi hiki otherwise aseme anafaidikaje na dharau hizi za makampuni ya simu na upandishaji huu wa vifurushi na kwann anakosa meno mbele ya kampuni hizi...naamini nje ya chama kuna watanzania makini sana na ambao ni wazalendo na ambao hawawezi kuchezewa hata sekunde na kampuni yyte..Wito: Rais alishasema...Kama Waziri umeshindwa sema USAIDIWE.
 
cha msingi tuendelee kuibana serikali iki kilichotokea leo iwe mwisho
 
Wewe unajua bei wanayonunulia internet haya makampuni hadi uanze kuwapangia?..

Trust me,bei zilikuwa poa tu..
 

You think hiyo rollout ilifanyika overnight? You are dead wrong. Rollout kama hiyo ilipangwa na kuratibiwa kwa muda mrefu tu. Ujue changes kwenye live networks zinafata internal change processes sio vitu vya kuswitch on and off tu unavyofikira. Kuna change management process and approvals,,teams alignment to support the change,,rollback solutions/plans etc..and these kind of changes normally takes place during low maintenance window ambayo ni usiku after 12.00 AM. Tatizo la TCRA notice yao hawakuweka timeline. Walitakiwa wawe wameshawasiliana na Operators na kualign kuhusu rollback timeline and by that wangeweza kuinform kwenye ile notice new bundles plan rollback itakuwa effective lini. Wangefanya hivyo tusingekuwa tunadiscuss hii kitu. So blame TCRA on this!!
 
Lazima wapewe barua rasmi na hapo ndipo ucheleweshaji unaweza kutokea

Naamini waliagizwa kwa maandishi na maamuzi yoyote ya kutengua maagizo ya awali lazima pia yawe ya maandishi.
.
hayo maandishi yana kurasa milioni ngapi kuyaandika!
 
Wewe unajua bei wanayonunulia internet haya makampuni hadi uanze kuwapangia?..

Trust me,bei zilikuwa poa tu..
Kwani hiyo internet wananunulia wapi ambako sisi tatupajui? Unafanya kama hii biashara na hizi taarifa ni za siri sana. Hivi unajua, serikali ingeamua kuifanya Tanzania kuwa na gharama za chini sana za internet, ni jambo lililo ndani ya uwezo wao kwa kuweka kodi na sera rafiki?

Mchawi hapa ni serikali tu. Kuna uzi niliwahi kuleta hapa nikielezea jinsi tulivyoingia katika mfumo wa Kifashisti. Hizi ni moja ya dalili zake.

Wamekodolea tu kodi za miamala na vifurushi, wanasahau soko kubwa la uchumi wa kidigitali wanalolikandamiza.
 
Kwan iyo internet wananunua wap!? Watupe ramani tukanunue wenyew huko direct!
 
Haya ndio Kiongozi wa Malaika alikuwa anakuja kuyatekeleza? Ila jamani kama tulikuwa waadhiniwa sijui
 
Khari
Hakuna hujuma yoyote afanye kazi
Una "usoda au ubia" na hao wahujumu mkuu?
 
Hata 40 haijafika tushaanza kuona pengo lake, nchi hii ngumu kweli!!
 
Tangia serikali iagize kurejeshwa kwa bei za awali kwa vifurushi vya simu ni takribani masaa zaidi ya 20 yamepita.
Sio kampuni ya serikali, TTCL wala kampuni binafsi (Tigo, Voda, Airtel na Halotel waliotekeleza agizo hilo.
Kijiswali cha kuchomekea tu, hivi Baba angeagiza hivyo, Kuna kampuni ingekaidi hadi muda huu?, Hiiiiiiii Baghosha!.
Tuwe watii kwa maagizo ya serikali sio kuangalia mtoa tamko
 
Yaaani hawa voda mpk saiv hawajarudishwa,ndio maana hii nchi inabidi iendeshwe kimagufuli magufuli ndio itaenda. La sivyo watazidi kucheka cheka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…