Ninyi mnaosemea mambo ya programming am sure hamna hiyo taaluma.
Iko hivi, haya mashirika ya mtandao kama Tigo, Voda n.k ni wazoefu saana katika kubadili hizi system/programme eneo ya vifurushi, financial matters kama Tigopesa au MPESA.
Endapo hata sasa hivi wakaamua kubadili vifurushi haimaanishi kuwa wanaanza upya, wanaweza wakarestore vile vya zamani, ieleweke kuwa kila wafanyapo marekebisho, yale yaliyopita huwa yanaseviwa, na hii wanafanya kwa ajili ya kutunza records zao ktk Annual General Meeting ama vikao kwa Marketing Departments.
Endapo wao wakaamua kubadili hivi vifurushi ni zoezi la muda mchache tu, wala sio process ndefu kama tunavyotaka kuaminishwa.
Naomba nijibiwe na mtu ambae amefanya kazi kama Head of ICT ktk mashirika kama haya, sio bla bla zenu.
Naungana na mleta mada, ni kiburi cha haya makampuni ya simu, hakuna kingine zaidi ya hapo. Maana wao wanaona ni kama vile usumbufu kwao, isitoshe wao hivi vifurushi before hawajivitoa walikubaliana na TCRA, someni barua ya TCRA vizuri utaona wanakiri kuyatambua mabadiliko hayo.