Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Makampuni mengine yamebadilisha tena tarrifs zao na wala si zile plans za awali...

Mathalani 'Eateli' naona kifurushi cha mwezi wakati huu wa bei za Ndungulile, kwa shilingi 30,000 ilikuwa unapata GB 14, leo hii kwa bei hiyo hiyo wamekngeza hadi kufika GB 26. Wastani wa GB 1 kwa shilingi 1155

Lakini ikumbukwe zamani, 'Eatel' hawakuwa na aina hii ya kifurushi bali kwa mwezi alikuwa anatoa GB 30 kwa shilingi 35,000. Wastani wa GB 1 kwa shilingi 1167
 
Hzo ni programming kijana , sio issue ya overnight, mpo fixed Sana na siasa hata kwenye mambo ya kitaalam Zaid
Programming ndio inarekebishwa haraka kuliko manual, au hujui mambo ya dijitali mkuu? Ila hapa ni siasa inachezwa. Serikali itakuwa imewapandishia kodi, wamerespond nao kwa kupandisha bei, serikali wamewaamuru washushe bei bila kodi kushuka, jamaa wamekomaa.
 
Nikiwa kama mtumiaji mkubwa kampuni hii...naona imeminya sana huduma za nawasiliano...

Haiwezekani kupiga 3/4 nzima mteja anapata 1/4 pekee. Mbaya zaidi serikali imetangaza kutoongeza bei..wao wamebaki na wanatupiga vby
Hongera! @Umepokea #60 (Mitandao Yote) + Dk 80(Halotel) + 4096 MB + SMS 100 hadi 00:23 00/00/2021. Asante!

Hii ni kwa shilingi 10,000/=

Sio fair.


Huyu anaendelea na Ubalozi??
Serikali ndio mbaya wako. We unaamini hawa jamaa wana ubavu wa kupingana na serikali?
 
Airtel wamerudi
Screenshot_20210404-101838.jpg
 
Voda bado wamekaidi agizo
Hamna anayeweza kaidi mzee, achilia mbali na hatua wanazoweza chukuliwa, wao wenyewe watapoteza wateja kwenda mitandao yenye unafuu.

TTCL wamerudi. ZANTEL wamerudi. AIRTEL wamerudi. Alafu wewe ujifanye kichwa ngumu? Ataumia nani kama si wao hapo?
 
Mpaka sasa hivi makampuni ya simu yanaendelea kuuza vifurushi kwa bei ileile onevu ambayo ililalamikiwa na wananchi hapo jana.

Licha ya Serikali kupitia TCRA kuagiza usitishwaji wa viwango hivyo, bado makampuni hayo yamekaidi na yanaendelea 'kuwaibia' wananchi kwa kuuza bando kwa bei ambazo Serikali imezisimamisha.

Tunamtaka Waziri Ndugulile na TCRA mara moja wasimamie agizo lao, la sivyo tunatawachukulia kuwa agizo lao ni la kisiasa na si kwa lengo la kumsaidia mwananchi.

Tunataka kuona mabadiriko ya bei za vifurushi mara moja la Sivyo Andungulile achia nafasi hiyo hutoshi. Umetusababishia wananchi adha kubwa sana kwa kitendo ulichokifanya cha kutaka kumfurahisha Meko kumbe unatuumiza sana wananchi
Hivi ni nani anayechukukuaga hizi nyuzi na kupeleka phoenix? Nimeuliza kwa uzuri tu kwa kutaka kujua.
Screenshot_20210404-110418.png
 
Nilichomaanisha ndiyo hicho kwamba sijui kitu kuhusu programming
Lakini mbona hujatufahamisha chochote zaidi ya kutu crash as if wote tunaijua hiyo progr....
No ngumu ku explain in an easy manner ....we jua sio mchakato wa siku moja hapo labda kuanzia kesho ndo inaweza change
 
Hamna anayeweza kaidi mzee, achilia mbali na hatua wanazoweza chukuliwa, wao wenyewe watapoteza wateja kwenda mitandao yenye unafuu.

TTCL wamerudi. ZANTEL wamerudi. AIRTEL wamerudi. Alafu wewe ujifanye kichwa ngumu? Ataumia nani kama si wao hapo?
Nawapa tu siku ya leo kesho nahamia mtandao mwingine
 
Sijawahi kufahamu aisee. Alafu hawana mtindo wa kutoa credit kwa mtandao husika wala mtoa mada. Kazi ya kuokoteza habari huku na kule!
Credit ya mtandao wanaonesha ila nilikuwa nataka kujua, huwa wanakuwa na agents kila nchi wanaopick na kufilter taarifa kwenye mitandao ama!
 
Back
Top Bottom