Makamu wa Rais Dkt. Mpango apiga marufuku Polisi kufunga Barabara kwenye Misafara
Kulikuwa na hizi mbuzi hapa tukadhani CDM watajifunza:

CHADEMA jifunzeni kwenye Ziara ya Makamu wa Rais Kahama

Hadi watoto wa shule walifungiwa njia. Ajabu na kweli CDM nao wakarudia yale yale Mwanza.

Tukasema wee, tukazodolewa hadi na ma kina joni.

Yakaja haya:

Ulinzi wa viongozi nani alitudanganya?

Ajabu na kweli CDM nao wanafanya yale yale.

Takasema tena weee, tukazodolewa tena hadi na mambuzi mengine. Ila tujuacho kinacho mkera yule kitakukera na wewe "under normal circumstances." Ni suala la muda tu na wapi imesimama.

Ninakazia CDM tusicheze wala kuchezeshwa ngoma na ma CCM. Hayana nia njema na bado tunao uwezo wa kuzicheza ngoma zetu kwa ufasaha tu.

Pole pole, lakini tutafika tu.
 
Tatizo Magari ya msafara nayo yanakuwaga mengi mno,yakiaanza kupita ni all most li saa yanapita hayo tu! Wapunguze Magari kwenye msafara,yabaki hata Magari matano tu, kweli dakika kumi zitatosha! Wwe gari karibu 50 ziko kwa msafara unazani hizo dk 10 zitatosha!!??
Kwa speed zinazotembea dakika 10 mbona zinatosha kabisa.
 
Jana msafara wake umepita mji mmoja kwa spidi kubwa, barabara ilifungwa magari yasipite mpaka msafara wake upite.

Ile barababara kufungwa tu wakajitokeza wanakijiji watutu na pikikipiki zao wasijue kama barabara imefungwa.

Wanakijiji wakafurahia kuona barabara nyeupe wakaziachia pikipiki zao kwa spidi kama zote wasijue mbele kuna polisi. Mara paap wakaishia mikononi mwa polisi. Baada ya msafara kupita walipelekwa kituoni
 
Ukweli siyo fair kufunga masaa 4 kwanini wasifunge hata 30 minutes
Juzi Jumanne, nimetoka Mwanza kwenda Shinyanga, nikiwa nimepanda basi la Malangwa liendalo Singida. Tumefika Usagara, saa tano asubuhi, tukaambiwa tupaki, kwani mbele yetu, Makamu wa Rais anakuja! Baadaye tukaambiwa yupo Misungwi anahutubia mkutano wa hadhara.
Tulikuja kuruhusiwa hapo saa kumi jioni. Mwendo alioondoka nao dereva wetu, ilikuwa balaa. Nilifika Shinyanga saa kumi na mbili jioni.
Kwa kweli, kama itafuatwa alichoagiza, tutamshukuru sana!
 
Rais akiwa anavaa nguo trafiki wanazuia magari kuanzia kibaha had posta. hadi aje atoke ni lisaa limoja aje apite mbezi ni masaaa mawili. sio sawa kwa kweli ila tulivyo na madereva wehu sizan kama dakika kumi zinatosha kabisa. labda pia na magari ya msafara yapungue yawe hata matano na viongozi wajifunze tu kutembea na magari yao tu mtaani.

ananunua tu ka V8 kake anakapiga tunted anapita tu kama wasafiri wengine
 
Ilikuwa ni ushamba na upumbavu kabisa, unachelewesha wagonjwa, watu wanaenda kwenye kesi wengine shuleni, kwanini wasifunge kabla ya dak 5 kupita kiongozi?
 
Rais akiwa anavaa nguo trafiki wanazuia magari kuanzia kibaha had posta. hadi aje atoke ni lisaa limoja aje apite mbezi ni masaaa mawili. sio sawa kwa kweli ila tulivyo na madereva wehu sizan kama dakika kumi zinatosha kabisa. labda pia na magari ya msafara yapungue yawe hata matano na viongozi wajifunze tu kutembea na magari yao tu mtaani.

ananunua tu ka V8 kake anakapiga tunted anapita tu kama wasafiri wengine
Maanake wafunge barabara kabla ya dak 10 kiongozi hajapita
 
Back
Top Bottom