Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angalau tunawapendaga watu wasiopendaga makuu !!Mtumishi wa Mungu Dr Mpango!
Hapo Ireland Msafara wa Biden unapishana tu na magari mengine!
Kila kitu ni protokali na usalama wa viongozi ni taaluma so asitupangie.Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena Barabara zikifungwa kwa masaa mengi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao.
Dr. Mpango amewaomba radhi Wananchi kwa usumbufu walioupata baada ya jana Barabara kufungwa kwa saa nne ili veve apite "Nilishamwambia IGP na nirudie kuwaambia Makamanda wa Polisi wa Mikoa, mambo ya kufunga barabara kwa masaa mengi kisa tu Mtoto wa masikini Philip Mpango anapita hapana"
"Jana naambiwa mmefunga Barabara mpaka masaa manne haiwezekani, kwanini?, sitaki kusikia tena hili linajirudia, muambizane na wanaopokea msafara huko tutakakopita"
"Acheni Wananchi wapite kwani dakika 10 hazitoshi), masaa manne kweli!? Nawaomba radhi ya dhati kabisa Wananchi"
======
Kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango inafuatia Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Jijini Mwanza kufunga Barabara kwa Saa 4 katika ziara yake na kusababisha foleni na adha kwa Watumiaji Barabara wengine.
Kitendo hicho kimefanya Dkt. Mpango kuwaomba radhi Wananchi huku akiwahoji Polisi kama Dakika 10 hazitoshi kupisha Misafara. Pia, amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kutorudia tena utaratibu huo.
Kumekuwa na Malalamiko ya Wananchi ya mara kwa mara kuhusu Misafara ya Viongozi kusababisha Foleni na usumbufu katika maeneo mbalimbali Nchini lakini bado suala hilo halijapatiwa ufumbuzi.
Hata dakika 20 sio mbaya lakini masaa hiyo sio sawa kabisa ! Ni uonevu !!Kwa speed zinazotembea dakika 10 mbona zinatosha kabisa.
Polisi pia walimfuata wakiwa na AK 47 kwenye mikorosho!Good example but angewaambia police the same wangeendelea kumfuata?
Wanatudhihaki tu.Sidhani km ana maanisha hilo.
Yanajali basi.nilikuwa Dodoma last week, maeneo kama kule kwa waziri mkuu, aliye karibu na huyu mheshimiwa amwambie, awe basi anatoka baada ya watu kwenda church jumapili, tulikalishwa pale kumsubiri Majaliwa apite karibia saa moja, na hakupita wala nini. na ulikuwa muda wa kanisani ibada ya pili saa nne. watu walifyonya sana. magari yamepaki kuanzia royal hadi kule njiapanda wajenzi, atu tunamsubiria mtu apite ambaye ndio sisi tunamlipa mshahara. watu walifyonya balaa. majaliwa anasimamisha sana ule uelekeo wa kwa waziri mkuu kwa wale waliokaa kidogo dodoma wanajua, mwambieni awe anatoka wakati watu walau wameshaenda wanakoenda. kwa waliokuwa dodoma jumapili iliyopita mnajua ninachosema.
Halafu kanichefua alipochomekea eti "mtoto wa masikini Mpango anapita" hawa watu ndo maana miaka na miaka bado wametuweka utumwani maana hawana akili wala utashi wa kuchukia umasikini. Mtu kujiita maskini anaona sifa sana alale kwenye nyumba ya tembe basi.Nadhani Mzee Filipo kabla ya kuongea hoja yake, alitakiwa aulizane na wataalamu wa usalama kwa nini wanataka barabara iwe wazi, na jinsi gani yeye akiwa anataka kupita sehemu, basi apite kwa wakati aliowaahidi Polisi. Kuliko achelewe na apite nje ya ratiba aliyoahidi wana usalama, halafu alalame
Zile confidence za enzi za corona kukataa chanjo na kuacha kuvaa barakoa, tuliona matokeo yake, pia taifa lina kumbukumbu ya ajali ya Edward Moringe Sokoine, taifa haliko tayari kurudia makosa.
Na wananchi wenye mawazo kama mtoa mada pia ni wengiTuna mambo ya hovyo sana.
Nchi hii, kwa kiasi kikubwa, umaskini unachangiwa na Serikali na watendaji wake.
Serikali haioni thamani ya muda. Kuna wakati nakumbuka nilikuwa Mwanza. Saa 9 alasiri tumesimamishwa Nyegezi kupisha msafara wa Waziri Mkuu. Muda huo wa saa 9, Waziri Mkuu alikuwa Shinyanga. Halafu alipotoka Shinyanga akasimama Misungwi kuwasalimia wananchi.
Mwanza alifika saa 12.30 jioni
Yaani zaidi ya masaa 3 wananchi wamesimamishwa eti kupisha msafara wa Waziri Mkuu.
Fikiria watu wamesimamishwa tokea Nzega mpaka Mwanza. Ni watu elfu ngapi. Kama watu ni watu 10,000 shughuli zao zimesimama, na kama kila mmoja anaingiza sh 20,000 kwa saa, ina maana ni sawa na 20,000 x 3 x 10,000 = 600,000,000. Hiyo ni kwa siku 1 na kwa kiongozi mmoja. Bado kuna Rais, Makamu wa Rais, siku hizi mpaka makamanda wa polisi wakipita mnasimamishwa. Kwa mwaka, mambo haya ya ajabu yanaliingizia Taifa hasara kiasi gani?
Nadhani tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa Polisi wa kufikiri na kupanga. Kinachofanyika hakistahili kuwa hivyo. Uwekwe utaratibu ambao utazuia kuwasimamisha wananchi zaidi ya nusu saa kupisha misafara ya viongozi wa kitaifa.
Huu upuuzi haupo kwenye mataifa yaliyoendelea. Sisi maskini tuliotakiwa kuutumia muda vizuri zaidi, ndiyo tunaoongoza katika kutothamini muda. Umaskini wa kichwani unatufanya kuwa maskini wa kila kitu, isipokuwa kuzaliana..
Sio ulofa na upumbavu..Kusimamisha watu barabarani masaa matatu hadi manne kisa kuna kiongozi ni ulofa na upumbafu wa hali ya juu.polis mjitathimini.
Baada ya kusoma hapo kwenye "Kusa mtoto wa masikini Mpango anapita" , hapo tayari najua anatania tu.Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena Barabara zikifungwa kwa masaa mengi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao.