Mtoto wa masikini 😂
Hii kauli maana yake si wazazi wake ndio masikini na si yeye
 
  • Je ni akina nani wanapaswa kufungiwa barabara?
  • Zama hizi, kama ulinzi wa viongozi unawezeshwa kwa kufunga barabara, jamaa wa kitengo wajitafakari
 
Ninakubaliana na Philipo na ninaamini kayasema maneno hayo kwa dhati ya moyo wake.

Ila mbona kauli yake hii inafanywa kuwa kama Kampeni ya "promosheni'?

Tayari Kuna "chawa" wanaomnyemelea?
 
Anamaanisha kweli alimwambia Makonda ni lazima ayalipie kodi yale makontena aliyodai ni ya msaada.
 
nilikuwa Dodoma last week, maeneo kama kule kwa waziri mkuu, aliye karibu na huyu mheshimiwa amwambie, awe basi anatoka baada ya watu kwenda church jumapili, tulikalishwa pale kumsubiri Majaliwa apite karibia saa moja, na hakupita wala nini. na ulikuwa muda wa kanisani ibada ya pili saa nne. watu walifyonya sana. magari yamepaki kuanzia royal hadi kule njiapanda wajenzi, atu tunamsubiria mtu apite ambaye ndio sisi tunamlipa mshahara. watu walifyonya balaa. majaliwa anasimamisha sana ule uelekeo wa kwa waziri mkuu kwa wale waliokaa kidogo dodoma wanajua, mwambieni awe anatoka wakati watu walau wameshaenda wanakoenda. kwa waliokuwa dodoma jumapili iliyopita mnajua ninachosema.
 
Unaweza kusema kamaanisha kumbe wapi, wanapenda na kitu enjoy..

Kuna muda wanapigiwa deki na kuzibiwa viraka barabara wapite.
 
Mara nyingi ni kiherehere cha mapolisi kinachotesa watu!
 
I understand but huyo mtu ni nani? He is not a random citizen.
Niliwahi kuwa katika msafara wa Rais Mkapa kule kwao Lupaso sasa alitaka kwenda kumsalimia shangazi yake aliyekuwa anaugua nyumbani kwake. Kwa kuwa nyumbani kwa shangazi yake hakukuwa mbali kama mita 500 toka kwa Mkapa aliamua kwenda kwa mguu na akawaambia walinzi wake wasimfuate.

Kilichotokea walinzi walimgomea pamoja na kuwafokea kwa sauti kali hadi tuliokuwa mbali tukasikia. Alipokuwa anaenda bado walimfuatilia wakipita kwenye mikorosho hadi wakafika naye kwa shangazi yake na wakakaa nje wakimsubiri hadi alipomaliza mazungumzo na kurudi Ikulu ndogo.

Hivyo pamoja na kuwazuia wasimfuate lakini bado walimfuata.
 

Good example but angewaambia police the same wangeendelea kumfuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…