Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Wabunge wa upande wa pili (CHADEMA, ACT na CUF) ni vema mkajiunga CCM ili kwa pamoja tujenge nchi

Yaani CCM hamtaki kabisa Demokrasia ya vyama vingi. Kwa wingi wenu bungeni hebu shaurini marekebisha ya Sheria, futeni vyama vingi
Vifutwe ijulikane ni nchi ya CCM.πŸ˜‚πŸ˜‚
Wanajua wakifanya hivyo, mabeberu wanachomoa betri, malumbesa ya madolari inakuwa basi!!

Wanataka kitumbo mbwatata hawataki kitumbo mbwatata!

Everyday is Saturday............................... 😎
 

Hadi 2010 upinzani ulikua sehemu nzuri sana, ila kwa tamaa za viongozi wenu wapenda fwedha mliharibu wenyewe kwa kukiuza chama kwa mlimwita fisadi

Hapa ndio mnapozidiwa maarifa na CCM


Acheni kutafuta excuses

Kina NYERERE wangesema wanataka taasisi imara za serikali ya wakati ule ziwasaidie tungepata uhuru kweli ???
 
Inabidi tuongee ukweli kuhusu CCM pia. Hivi unataka kutuambia kuwa wabunge wote wa CCM wanakidhi vigezo?

Unasema wapinzani walijimaliza. Tuambie ni lini wapinzani wamepewa nafasi ya kushindana katika mazingira sawa na ya CCM? Hii haijawahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi vilivyoanzishwa.

Tuwe wa kweli. Badala ya kuwatupia lawama watu ambao wamezuiwa kufanya siasa, wamefungwa with impunity na watendaji wameonyasha wazi kuwa lengo lao ni kukipa ushindi chama fulani bila kujali wataonekana vipi.

Hivi matokeo ya uchaguzi uliopita yamechapishwa? Yakionyesha kura ambazo kila mgombea alipata katika kila kituo cha kupigia kura?

Amandla...
 
Kuongea ukweli kwenu Ni kuichafua nchi..ndo maana mnaitwa masikini na wanyonge kwasababu ya ujinga wenu kama huu
 
25

Chadema...... 20

ACT wazalendo...... 4

CUF......... 1

Maendeleo hayana vyama!
Kwa hiyo hao ndio wanakwamisha maendeleo? Anataka kuanza vibaya. aache mawenge mawenge ya Jiwe. yeye afanye kazi na wote. Heshimuni kanuni ya dunia kwamba daima kuna nguvu mbili zinazovutana na ndizo hutufanya tutembee, tusonge mbele.

Yeye ni msomi wa uchumi, anajua kabisa kwamba maendeleo yoyote ni matokeo ya ushindani. Kwenye mji tukiwa na duka moja tu hakuna maendeleo. Tutapanga foleni hadi kuchelewa kazi za nyumbani, shambani na ofisini.

Hivi ni utafiti gani uliowahi kufanywa ukaonyesha kwamba nchi ya chama kimoja hupinga hatua kubwa ya maendeleo kuliko nchi ya mfumo wa vyama vingi? Mbona mnakuwa wasomi halafu bado ni wajinga?
 
Ile haikuwa busara ya CCM kumbe ndiyo maana mwendazake alihitaji somo la historia liwe la lazima, kile kilichopelekea waruhusu licha ya maneno ambayo sina uhakika kuwa ni kweli pamoja na kuwa zinaitwa ni takwimu kuwa majority walikataa ni takwa la mikopo kutoka IMF la uwepo wa vyama vingi ndiyo maana unaona kukaanza kuwa uchangiaji wa gharama kama ada, afya ambazo hapo awali zilikuwa free

Kwa hiyo siyo kweli zilikuwa busara za CCM ni condition ziliwabana na ukitaka kuona hilo kuwa ni kweli ona kwenye huu utawala wa mwendazake alichofanya kwa vyama upinzani ndiyo utagundua hazikuwa busara
 
Mlipoitwa kuandamana ulienda?
Au ulikua online ukisubiria picha za wenzio walioenda??
Hivi unajiita mpinzani halafu unataka Serikali ya chama cha mapindunzi ndio ikusaidie kushika dola wewe uko sawa kweli????
Tena huku unaandika barua nchi isipewe mkopo wa elimu huku unataka dolaπŸ€”
Huku unafurahia na kuwapa watesi taarifa za kuliumiza taifa huku unataka dola😐
Huku unazuia mikataba mibovu isivunjwe huku unataka dola

Mtasubiri sanaaa
 
Nimeanza tu hapo juu ulipoanza sijamalizia sababu ni offpoint kabisa kufikiri mm ni mpinzani tena yule wa kuandamana. Endelea tu kukipigania chama kwa mtindo wa kukiharibia. Ungekuwa huna fake Id huwa kuna utaratibu wa kurekebisha watu aina yako.

Mwenyekiti wa ccm vijana alirekebishwa akasahihisha maombi ya msamaha aliyotoa na kusema si ya chama ni yake binafsi. Ww ni ngumu sababu hili si jukwaa rasmi.
 
PLO Lumumba anaongea uongo?
PLO kuongea ukweli si lazima imaanishe TL anaongea uongo, and vice versa. PLO anaweza kuongea katika eneo moja kusapoti aliyofanya JPM, na TL anaweza kuongea katika eneo lingine kupingana na aliyofanya JPM, na bado wote wakawa sahihi. Waache tu, kila mtu acheze mechi zake, zitakapoisha mahesabu ya point yataamua
 

Unata wapinzani wasaidiwe kushinda???
🀣🀣🀣🀣
 
Mizengo Pinda : "Kuondoa Umasikini na kuchagiza maendeleo kupitia sera zinazolenga ukuaji wa kiuchumi ndiyo agenda kuu"

20 Jan 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda atembelea REPOA

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Peter Pinda alielezea mchango wa REPOA katika kuchangia maboresho ya sera za tawala za mikoa na serikali za mitaa
Source : REPOA Tanzania
 
Hivi kweli unaamini Slaa angeweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kumshinda Kikwete? Na kwa vile Lowasa alijiunga Chadema 2015, Katibu Mkuu aliyekuwepo 2010 -2015 alipoteza vipi mwelekeo?

Kulikuwa na taasisi imara chini ya ukoloni kuhakikisha kuwa haki inatendeka ndio maana nchi yetu ilipata uhuru. Ndio maana wakina Nyerere hawakumwaga damu na yeye mwenyewe hakuna Lupango.

Excuses mnatoa nyinyi kwa kujifanya kuwa makosa yote ni ya upinzani na kuwa walitendewa haki.

Amandla...
 
Yani Magufuli aichafue Nchi visingizo upeleke kwa Lissu.
 
Unata wapinzani wasaidiwe kushinda???
🀣🀣🀣🀣
Hamna mtu alisema wasaidiwe kama ambavyo mnavyosaidiwa nyie. Kinacho takiwa ni asibebwe mtu, sio CCM sio Upinzani. Referee na Linesmen wakae pembeni waache mchezo uendelee bila wao kuingia uwanjani kusaidia timu mojawapo.

Shida yenu ni kuwa hamuamini kuwa ushindi hauwezi kupatikana bila msaada wa dola.

Amandla...
 
Kinachokuuma nini au kuna chako unachompatia?

Nyie mlioko huko mmeibiwa na jiwe sana.
 
Una mimba ya Lissu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…