Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Wabunge wa upande wa pili (CHADEMA, ACT na CUF) ni vema mkajiunga CCM ili kwa pamoja tujenge nchi

Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Wabunge wa upande wa pili (CHADEMA, ACT na CUF) ni vema mkajiunga CCM ili kwa pamoja tujenge nchi

Yaani CCM hamtaki kabisa Demokrasia ya vyama vingi. Kwa wingi wenu bungeni hebu shaurini marekebisha ya Sheria, futeni vyama vingi
Vifutwe ijulikane ni nchi ya CCM.😂😂
Wanajua wakifanya hivyo, mabeberu wanachomoa betri, malumbesa ya madolari inakuwa basi!!

Wanataka kitumbo mbwatata hawataki kitumbo mbwatata!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hivi kama hakuna vyama vya upinzani vinavyo kubalika na jamii ya Watanzania nini sababu hasa ya kupora kura na wizi?
Kwa nini kutumia NEC na Polisi kupata ushindi badala ya kura? Kama unaishi Tanzania na hayo yanayotokea kwenye uchaguzi huyaoni kwa nini usiitwe KIAZI? tena mbatata kabisa.
Hivi ukiangalia bunge lililopita na hili ambalo hakuna wabunge (wa ukweli wa Chadema) hamuoni tofauti?

Hadi 2010 upinzani ulikua sehemu nzuri sana, ila kwa tamaa za viongozi wenu wapenda fwedha mliharibu wenyewe kwa kukiuza chama kwa mlimwita fisadi

Hapa ndio mnapozidiwa maarifa na CCM

Inasemekana mwaka 1909 Henry Ford aliwaambia wateja wa gari lake aina ya Model T kuwa wana uhuru wa kuchagua gari la rangi yeyote wanayoipenda ili mradi iwe nyeusi.
Hii haina tofauti na nyie kutuuambia kuwa wananchi watakuwa na uhuru wa kuchagua chama chochote cha upinzani ili mradi kiwe CCM au kipate baraka ya CCM.

Upinzani imara utatokeza pale tu ambapo patakuwa na taasisi imara za kuhakikisha kuwa vyama vyote vina haki sawa. Hakuna chama chenye haki ya kuamua taswira ya chama kingine. Ni kama Simba wapewe haki ya kupanga timu na kocha wa timu nyingine. Uamuzi wa chama gani kinastahili kutawala ni wa wananchi na si mwingine. Na haki hiyo ni pamoja na kuchagua chama magumashi kama watakipenda.

Huo upinzani imara unayosema unautaka haupatikana kwa mtindo huu unao upigia debe. Utakuwa ni upinzani jina tu. Kama ilivyo sasa kwenye Bunge letu tukufu. Na itabaki kuwa hivyo hata kama Zitto ataingia mjengoni.

Amandla...

Acheni kutafuta excuses

Kina NYERERE wangesema wanataka taasisi imara za serikali ya wakati ule ziwasaidie tungepata uhuru kweli ???
 
Umeandika saana lakini kitu kimoja tuu uelewe kwamba kujenga chama imara sio lelemama

Unalalamika kuhusu idadi ndogo ya wapinzani bungeni..... sasa kama ndio walipata nafasi ulitakaje? Au kwa sababu kuna upinzani lazima bungeni wawepo wengi hata kama hawajakidhi vigezo?

Upinzani walikaa vizuri sana miaka 2010 lakini walijimaliza wenyewe 2021 kwasabu ya tamaa zao binafsi. Na sasa ndio wamejichimbia kaburi kabisaaaa

Kabla ya kuilaumu CCM tuongee ukweli kuhusu upinzani
Inabidi tuongee ukweli kuhusu CCM pia. Hivi unataka kutuambia kuwa wabunge wote wa CCM wanakidhi vigezo?

Unasema wapinzani walijimaliza. Tuambie ni lini wapinzani wamepewa nafasi ya kushindana katika mazingira sawa na ya CCM? Hii haijawahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi vilivyoanzishwa.

Tuwe wa kweli. Badala ya kuwatupia lawama watu ambao wamezuiwa kufanya siasa, wamefungwa with impunity na watendaji wameonyasha wazi kuwa lengo lao ni kukipa ushindi chama fulani bila kujali wataonekana vipi.

Hivi matokeo ya uchaguzi uliopita yamechapishwa? Yakionyesha kura ambazo kila mgombea alipata katika kila kituo cha kupigia kura?

Amandla...
 
Nimeona Lisu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure.
Kuongea ukweli kwenu Ni kuichafua nchi..ndo maana mnaitwa masikini na wanyonge kwasababu ya ujinga wenu kama huu
 
25

Chadema...... 20

ACT wazalendo...... 4

CUF......... 1

Maendeleo hayana vyama!
Kwa hiyo hao ndio wanakwamisha maendeleo? Anataka kuanza vibaya. aache mawenge mawenge ya Jiwe. yeye afanye kazi na wote. Heshimuni kanuni ya dunia kwamba daima kuna nguvu mbili zinazovutana na ndizo hutufanya tutembee, tusonge mbele.

Yeye ni msomi wa uchumi, anajua kabisa kwamba maendeleo yoyote ni matokeo ya ushindani. Kwenye mji tukiwa na duka moja tu hakuna maendeleo. Tutapanga foleni hadi kuchelewa kazi za nyumbani, shambani na ofisini.

Hivi ni utafiti gani uliowahi kufanywa ukaonyesha kwamba nchi ya chama kimoja hupinga hatua kubwa ya maendeleo kuliko nchi ya mfumo wa vyama vingi? Mbona mnakuwa wasomi halafu bado ni wajinga?
 
Sio ccm,sema watanzania hawakai vyama vingi,kwa sababu tayari democrasia ilikuwepo kabla ya vyama vingi,ndio maana hata kwenye tume ya maoni ya mhe jaji Francis nyalali 1991/92, asilimia 80 walikataa vyama vingi,lkn kwa busara ya ccm wakasema acha tuvunje ile kanuni ya wengi wape,ccm ikaruhusu mfumo wa vyama vingi huku watanzania walio wengi walikataa,
Ile haikuwa busara ya CCM kumbe ndiyo maana mwendazake alihitaji somo la historia liwe la lazima, kile kilichopelekea waruhusu licha ya maneno ambayo sina uhakika kuwa ni kweli pamoja na kuwa zinaitwa ni takwimu kuwa majority walikataa ni takwa la mikopo kutoka IMF la uwepo wa vyama vingi ndiyo maana unaona kukaanza kuwa uchangiaji wa gharama kama ada, afya ambazo hapo awali zilikuwa free

Kwa hiyo siyo kweli zilikuwa busara za CCM ni condition ziliwabana na ukitaka kuona hilo kuwa ni kweli ona kwenye huu utawala wa mwendazake alichofanya kwa vyama upinzani ndiyo utagundua hazikuwa busara
 
Ujinga uleule unaendeleza. Hatuna upinzani wa vyama vya siasa serikalini kwa sasa. Sijui kwann unawaongelea. Katika kipindi ambacho udhaifu wote wa serikali hautatokana na upinzani ni kipindi hichi. Dr Vp aliongea kisiasa tu nadhani alikuwa anamaanisha wapinzani wa mitandaoni na mtaani. Hao hawapo katika utendaji.
Mlipoitwa kuandamana ulienda?
Au ulikua online ukisubiria picha za wenzio walioenda??
Hivi unajiita mpinzani halafu unataka Serikali ya chama cha mapindunzi ndio ikusaidie kushika dola wewe uko sawa kweli????
Tena huku unaandika barua nchi isipewe mkopo wa elimu huku unataka dola🤔
Huku unafurahia na kuwapa watesi taarifa za kuliumiza taifa huku unataka dola😐
Huku unazuia mikataba mibovu isivunjwe huku unataka dola

Mtasubiri sanaaa
 
Nimeanza tu hapo juu ulipoanza sijamalizia sababu ni offpoint kabisa kufikiri mm ni mpinzani tena yule wa kuandamana. Endelea tu kukipigania chama kwa mtindo wa kukiharibia. Ungekuwa huna fake Id huwa kuna utaratibu wa kurekebisha watu aina yako.

Mwenyekiti wa ccm vijana alirekebishwa akasahihisha maombi ya msamaha aliyotoa na kusema si ya chama ni yake binafsi. Ww ni ngumu sababu hili si jukwaa rasmi.
 
PLO Lumumba anaongea uongo?
PLO kuongea ukweli si lazima imaanishe TL anaongea uongo, and vice versa. PLO anaweza kuongea katika eneo moja kusapoti aliyofanya JPM, na TL anaweza kuongea katika eneo lingine kupingana na aliyofanya JPM, na bado wote wakawa sahihi. Waache tu, kila mtu acheze mechi zake, zitakapoisha mahesabu ya point yataamua
 
Inabidi tuongee ukweli kuhusu CCM pia. Hivi unataka kutuambia kuwa wabunge wote wa CCM wanakidhi vigezo?

Unasema wapinzani walijimaliza. Tuambie ni lini wapinzani wamepewa nafasi ya kushindana katika mazingira sawa na ya CCM? Hii haijawahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi vilivyoanzishwa. Tuwe wa kweli badala kuwatupia lawama watu ambao wamezuiwa kufanya siasa, wamefungwa with impunity na watendaji wameonyasha wazi luwa lengo lao ni kukipa ushindi chama fulani bila kujali wataonekana vipi.

Hivi matokeo ya uchaguzi uliopita yamechapishwa? Yakionyesha kura ambazo kila mgombea alipata katika kila kituo cha kupigia kura?

Amandla...

Unata wapinzani wasaidiwe kushinda???
🤣🤣🤣🤣
 
Mizengo Pinda : "Kuondoa Umasikini na kuchagiza maendeleo kupitia sera zinazolenga ukuaji wa kiuchumi ndiyo agenda kuu"

20 Jan 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda atembelea REPOA

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Peter Pinda alielezea mchango wa REPOA katika kuchangia maboresho ya sera za tawala za mikoa na serikali za mitaa
Source : REPOA Tanzania
 
Hadi 2010 upinzani ulikua sehemu nzuri sana, ila kwa tamaa za viongozi wenu wapenda fwedha mliharibu wenyewe kwa kukiuza chama kwa mlimwita fisadi

Hapa ndio mnapozidiwa maarifa na CCM

Acheni kutafuta excuses

Kina NYERERE wangesema wanataka taasisi imara za serikali ya wakati ule ziwasaidie tungepata uhuru kweli ???
Hivi kweli unaamini Slaa angeweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kumshinda Kikwete? Na kwa vile Lowasa alijiunga Chadema 2015, Katibu Mkuu aliyekuwepo 2010 -2015 alipoteza vipi mwelekeo?

Kulikuwa na taasisi imara chini ya ukoloni kuhakikisha kuwa haki inatendeka ndio maana nchi yetu ilipata uhuru. Ndio maana wakina Nyerere hawakumwaga damu na yeye mwenyewe hakuna Lupango.

Excuses mnatoa nyinyi kwa kujifanya kuwa makosa yote ni ya upinzani na kuwa walitendewa haki.

Amandla...
 
Nimeona Lisu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure.
Yani Magufuli aichafue Nchi visingizo upeleke kwa Lissu.
 
Unata wapinzani wasaidiwe kushinda???
🤣🤣🤣🤣
Hamna mtu alisema wasaidiwe kama ambavyo mnavyosaidiwa nyie. Kinacho takiwa ni asibebwe mtu, sio CCM sio Upinzani. Referee na Linesmen wakae pembeni waache mchezo uendelee bila wao kuingia uwanjani kusaidia timu mojawapo.

Shida yenu ni kuwa hamuamini kuwa ushindi hauwezi kupatikana bila msaada wa dola.

Amandla...
 
Nimeona Lisu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure.
Kinachokuuma nini au kuna chako unachompatia?

Nyie mlioko huko mmeibiwa na jiwe sana.
 
Nimeona Lisu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure.
Una mimba ya Lissu?
 
Back
Top Bottom