Makamu wa Rais, Samia Suluhu akutana na Mkuu wa Kanisa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo

Hali ikiharibika ndo mama mwenye hekima na busara zake utumwa kuweka mambo sawa, ubarikiwe mama Samia
Hali haiwezi kuharibika kamwe maana aliye mchagua huyo mama ana busara na hekima!
 
Huku akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Nyerere, Askofu Shoo amesema, “pale kanisa litakaposimama na watu wenye mamlaka na kumsahau mnyonge hilo halistahili kuwa kanisa na wala hastahili kuwa mtumishi wa Mungu.”


Maneno mwiba kwa awamu ya 5
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Hakuna mahali popote ilipoandikwa Kanisa kutii mamlaka za Duniani. Bali ni waumini walioambiwa watii mamlaka. Lakini wanakumbushwa tena kuwa yawafaa kumsikiliza zaidi Mungu kuliko mwanadamu. Na pia wanaambiwa wampe Mungu yaliyo yake na Kaisari yaliyo yake.

Uwendawazimu unakuja pale Mamlaka za Dunia zinapodhani kuwa Kanisa linatakiwa kuzitii mamlaka za Duniani. Kimsingi Kanisa ni mamlaka ya Mungu haliwezi kuzitii mamlaka za Dunia.

Kwa sisi wakristo tunaamini Kanisa ni mali na sauti ya Mungu. Kristo ndiye aliyelianzisha Kanisa. Mamlaka za Duniani huanzishwa na wanadamu.

Mamlaka za Duniani hukubaliwa na Mungu kwa malengo maalum. Lengo la kwanza mamlaka za Dunia zinaweza kuwepo kwaajili ya utukufu wa Mungu. Mamlaka hizo kwa kuwa zina baraka ya Mungu, na zipo kwaajili ya utukufu wake, hutenda mema kwaajili ya watu wake. Watu wake hupokea baraka nyingi kutokana na utawala huo.

Lengo la pili Mungu huweza kuzikubali mamlaka za Dunia kuendeshwa na shetani kama adhabu kwa jamii ambayo mamlaka hiyo inatawala. Mamlaka za namna hiyo ziliwahi kutokea na bado zinatokea mpaka leo. Mamlaka hizo huwa zipo kwaajili ya kuwatesa watu wake. Watu wataonja machungu wawapo chini ya tawala za namna hiyo.

Mwanadamu amepewa utashi wa kupima kama mamlaka zinazowatawala zimekubaliwa na Mungu kama baraka kwao au kama adhabu kwao. Wanapogundua kuwa mamlaka ipo kwaajili ya kuwaadhibu, wanatakiwa kumrudia Mungu kwa toba iliyo njema. Maombi yao, yakikubaliwa na Mungu, tawala ile dhalimu hupeperushwa.

Watu wa Mungu hawastahili kufishwa ufahamu wakaamini kila mamlaka ipo kwaajili ya utukufu wa Mungu.
 
Tutajua nani sikio nani kichwa..twendeni tu..leo wanatumiwa na wanasiasa..kesho watatumiwa na mataifa makubwa dhidi ya serikali..sio jambo la kupuuza..hawatakiwi hata kuchekewa hao waendekeza matumbo.
Nakuambi hiviii.....utasubiri sana tena sana.
 
Wewe sijui hata huwa unaandika nini,pumbapumba tupu!

Sasa hapa ndio umeandika uzwazwa gani?

Wapiga debe wa CCM awamu hii ni kinyaa kitupu!
Barbarosa na Jingalao ni mental case. Huwezi kuwategemea hata katika utetezi maana hata uwezo wa kujenga hoja, naamini hawana.
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Kanisa kwanza, serikali baadaye. Kanisa ni kazi ya Mungu, ilihali serikali ni kazi ya wanadamu. Serikali hazidimu, kanisa litadumu milele
 
Mtake radhi Mama Samia kwanza, hawezi kunisaliti mimi kwa lipi? Chunga ulimi wako kijana, huyu Mama ana heshima na busara na hajawahi kukwaruzana na mtu hivyo usivuke mpaka!
Na wewe unakubali kuwa huyu Mama ana heshima na busara kumzidi jiwe?
 
Nakumbuka hata tundu lisu alipopigwa risasi na kukaa hospital miezi bila ujumbe wowote kutoka serekale ilibidi mama akaokoe jahazi
Mama yetu huyu ana hekma sana
 
Tulisema pale mwanzoni serikali imemeza moto,Ila Ile press conference ya Mbatia ilikoleza moto mpaka Nchemba akatumwa kutuliza hali.
Kanisa haliwezi kutishwa,period!
Watu wasipozungumza mawe yatanena pia
 
Hawachelewi kusema huu ni uchochezi, aliuanza Mwl Nyerere
 
Maoni ya askofu shoo wa kaskazini akimpa ushauri askofu mteule Laizer wa kutoka kaskazini pia huku akinukuu maneno ya Mwanasiasa Nyerere badala ya maneno ya Mungu yaliyoko kwenye Biblia.Askofu Shoo joho lake avae tu gwanda la chadema juu avae hilo kofia la uaskofu itapendeza zaidi
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Mashindano ya nini?
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
SICK? Mbona wanaapishwa na viongozi wa dini kwenye hayo madaraka? Na hili la KKKT wameufyata, sasa tusubiri 2020 adhabu ya kukurupuka na ukigeugeu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…