Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Now naamini abdallah possi hakujiuzuru kwa kupenda
Of course, that's how they do! Kwa nafasi ambazo rais hana mamlaka ya kutimua, wanachofanya ni kuwataka/kuwalazimisha wahusika kujiuzuru!!!
 
Huyu mama alistahili sana nafasi ile nzima sijui ni kwanini jk hakumwona na kumsimamisha badala ya naibu balozi mstaafu wa UN!
Nikupongeze mama kwa kuyaondoa makandokando na manaeno tunayosemwa vibaya upande huo! Natarajia mkulu naye atapanga japo kasafari ka kwenda kumuona kama alivyokuwa anafanya JK alipokwenda SA kumjulia hali yule mwandishi aliyafanyiziwa na vijana wake!
 
sasa nikuchekeshe mdogo wangu! kule nyumbani tulicheza ka mechi cha netiboli majuzi,, kuna wachovu fulani tumewapiga 42 kwa 1, can you believe it?!
 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

View attachment 639832

View attachment 639833

Jambo jema. Ila sasa hii ceremony ya kumwapisha Uhuru isingekuwepo serikali ingepeleka mwakilishi wake NBI kumjulia hali TAL?
 
sasa nikuchekeshe mdogo wangu! kule nyumbani tulicheza ka mechi cha netiboli majuzi,, kuna wachovu fulani tumewapiga 42 kwa 1, can you believe it?!
Mpu.mba.vu mwingine wa kimataifa! Ushindi wa policcm unausifia? Tafuta kibarua kwa mhindi wewe acha kuishi kwa shemeji kugongea jero ya bando! Kwa taarifa yako hao mliowapachika hawana maajabu na wamwnuniwa kinoma huku mtaani na hawana furaha kabisa.
 
Hii habari amepenyezewa mwanadada yule wa US na mtu anaetumia user name ya "binamubananga" ambae amedai yuko Nairobi na aliingia wodini kwa Lissu soon baada ya Mama Samia kutoka..

Aliyoyaeleza bwana huyu kama ni ya kweli, basi tutarajie watu kuumbuka hasa wale wapotoshaji wa kilichoongelewa kati ya Lissu na Mama Samia.

Mahojiano yatakuwa ni kupitia BBC Swahili na mtangazi atakuwa ni John Nene.

Bwana huyu amesema mahojiano hayo pia yatapatikana kupitia mwananchi official.

Tusubiri.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

View attachment 639832

View attachment 639833

Video na picha zimehaririwa sana. Kwa mfano sehemu alipotaka kumkumbatia wakapakata fasta.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom