Makanisa mengi ya kilokole hapa Bongo hayafundishi tena kuhusu Mpinga Kristo & 666. Kulikoni?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Nakumbuka miaka ya nyuma mahubiri kuhusu Mpinga Kristo, alama ya mnyama (666) na kitabu cha Ufunuo yalikuwa kawaida sana kuyasikia kuanzia makanisa ya kilokole vijijini huko hadi yale makubwa ya akina askofu Mwakatage na Mwenisongole mijini huku!

Kila baada ya muda ungeyasikia madhabahuni.

Leo ukitembelea makanisa mengi, msisitizo unaonekana kuhamia kwenye mafanikio, ndoa, biashara, uponyaji, ukombozi na maendeleo ya maisha ya kila siku.

Je, mafundisho kuhusu mwisho wa nyakati yamebadilika?

Au viongozi wameona tafsiri zake zimekuwa zikileta hofu, utata na ubashiri mwingi kiasi cha kuamua kuyaepuka?

Biblia bado inataja namba 666 katika Ufunuo 13:18, lakini Wakristo wa madhehebu mbalimbali wamekuwa na tafsiri tofauti kuhusu maana yake—wapo wanaoiona kama ishara ya mfano (symbolic), wengine huiona kama rejea ya mtu au utawala fulani wa kihistoria, na wengine wanaamini inahusu matukio yajayo.

Hakujawahi kuwa na makubaliano ya tafsiri moja kati ya madhehebu yote.

Swali langu ni hili:

- Kwa nini mada hizi zimepungua sana kwenye mahubiri?

- Ni kwa sababu ya mabadiliko ya teolojia?

- Ni kwa sababu waumini wa sasa wanahitaji mafundisho yanayogusa maisha ya kila siku?

- Au bado zinafundishwa, ila si kwa kiwango cha zamani?

- Mbona zama tulizopo kuna kulazimishana saaana kutumia cashless transactions na kupatiwa namba tambulishi, je walokole hizi ndio dalili za ujio wa 666 na mpinga Kristo?!

Ningependa kusikia maoni yenu, hasa wale wanaohudhuria makanisa ya madhehebu tofauti.
 
Ni kweli, umenena vema, wameibuka wachungaji/wainjilisti wapya wasiojua unabii. Hawa wanahubiri mafanikio ya mwilini tu. Hata uwe mdhambi vipi hutahubiriwa uache dhambi. Habari za mpinga kristo hawazijui na hawazielewi ni ngumu kufundisha na kuzihubiri kwa kuwa wao wenye ni sehemu ya mfumo huo ama kwa kujua au kutokujua
 
Siku hizi ukihubiri hayo mafundisho utaonekana ni mshamba uliyepitwa na wakati. Hata wachungaji wazee waliohubiri injili hiyo wamebadilika sana. Wameachana na mafundisho hayo, wanachohubiri ni utoaji na baraka tu. Wanaona habari za mpinga kristo na 666 ni kitisho kwa waumini. By the way huo ni unabii na tayari kwa sehemu ulishatimia
 
So what!!!
 
.
 
Attachments

  • images - 2026-03-11T072226.716.jpeg
    images - 2026-03-11T072226.716.jpeg
    35.2 KB · Views: 16
  • images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    images - 2026-03-11T064212.186.jpeg
    38.8 KB · Views: 19
  • images - 2026-03-11T072153.706.jpeg
    images - 2026-03-11T072153.706.jpeg
    9.4 KB · Views: 17
  • images - 2026-03-11T072504.623.jpeg
    images - 2026-03-11T072504.623.jpeg
    37.3 KB · Views: 17
  • images - 2026-03-12T083108.634.jpeg
    images - 2026-03-12T083108.634.jpeg
    40.9 KB · Views: 19
  • 1555667456310.jpeg
    1555667456310.jpeg
    85 KB · Views: 12
Si hayo tu, ni mengi yameachwa kufundishwa. Iko wapi mikutano ya injili ikihubiri watu waache dhambi na kuokoka? Habari za kutubu na kuacha dhambi zimeachwa kuhubiriwa, mwendo ni maji na mafuta ya upako tu kwa mitume na manabii feki
 
Huo unabii upo pale pale ni lazima utimie hata kama wameacha kuuhubiri
Wanahubiri vizuri tu. Shida waafrika tuliletewa injili kua inatusaidia tu kwenda mbinguni ila hatukufundishwa kuna injili pia ya namna bora ya kuishi duniani na kurithi baraka tulizoambiwa ni za Ibrahim ambaye tunajua kabisa umaskini haukutajwa kwake.
 
Watumishi wengi wanahubiri kile waumini wao wanapenda kusikia, lakini habari ya siku za mwisho na kukemea dhambi huwezi kusikia, lakini ukizungumzia namba 666 inafanya kazi katika hatua za mwanzo, hatua zenyewe ni kuhakikisha idadi ya watu duniani inapungua, lakini pia kuhakikisha jinsia Me wanapungua ili kupoka mamlaka ya kiutawala kutoka kwa Me kwenda kwa Ke, na ndio yanayofanyika, kuongeza kwa maarifa hasa ya teknolojia, unaona sasa hivi hakuna haja ya mwanaume na mwanamke kukutana ili kutengeneza mtoto, mtoto anaweza tengenezwa maabara yote hiyo ni kupinga uwezo wa Mungu na asili yake
 
Nakumbuka miaka ya nyuma mahubiri kuhusu Mpinga Kristo, alama ya mnyama (666) na kitabu cha Ufunuo yalikuwa kawaida sana kuyasikia kuanzia makanisa ya kilokole vijijini huko hadi yale makubwa ya akina askofu Mwakatage na Mwenisongole mijini huku!

Kila baada ya muda ungeyasikia madhabahuni.

Leo ukitembelea makanisa mengi, msisitizo unaonekana kuhamia kwenye mafanikio, ndoa, biashara, uponyaji, ukombozi na maendeleo ya maisha ya kila siku.

Je, mafundisho kuhusu mwisho wa nyakati yamebadilika?

Au viongozi wameona tafsiri zake zimekuwa zikileta hofu, utata na ubashiri mwingi kiasi cha kuamua kuyaepuka?

Biblia bado inataja namba 666 katika Ufunuo 13:18, lakini Wakristo wa madhehebu mbalimbali wamekuwa na tafsiri tofauti kuhusu maana yake—wapo wanaoiona kama ishara ya mfano (symbolic), wengine huiona kama rejea ya mtu au utawala fulani wa kihistoria, na wengine wanaamini inahusu matukio yajayo.

Hakujawahi kuwa na makubaliano ya tafsiri moja kati ya madhehebu yote.

Swali langu ni hili:

- Kwa nini mada hizi zimepungua sana kwenye mahubiri?

- Ni kwa sababu ya mabadiliko ya teolojia?

- Ni kwa sababu waumini wa sasa wanahitaji mafundisho yanayogusa maisha ya kila siku?

- Au bado zinafundishwa, ila si kwa kiwango cha zamani?

- Mbona zama tulizopo kuna kulazimishana saaana kutumia cashless transactions na kupatiwa namba tambulishi, je walokole hizi ndio dalili za ujio wa 666 na mpinga Kristo?!

Ningependa kusikia maoni yenu, hasa wale wanaohudhuria makanisa ya madhehebu tofauti.
Mafundisho yote mliyo pewa na hao wahuni ni uongo mtupu ...labda wewe unapenda kudanganywa na wahuni wa dini ...mfano ni hiyo 666 ...jibu sahihi kwa asilimia 100% la 666 ni MWILI WAKO MWANADAMU.(666=MWILI WA BINADAMU) je mleta uzi ulisha sikia mtumishi gani au kanisa gani au mitume gani wakisema hivi? ..wote wanakuja na porojo za alinacha.
 
kivipi? Fafanua
 
Nakumbuka miaka ya nyuma mahubiri kuhusu Mpinga Kristo, alama ya mnyama (666) na kitabu cha Ufunuo yalikuwa kawaida sana kuyasikia kuanzia makanisa ya kilokole vijijini huko hadi yale makubwa ya akina askofu Mwakatage na Mwenisongole mijini huku!

Kila baada ya muda ungeyasikia madhabahuni.

Leo ukitembelea makanisa mengi, msisitizo unaonekana kuhamia kwenye mafanikio, ndoa, biashara, uponyaji, ukombozi na maendeleo ya maisha ya kila siku.

Je, mafundisho kuhusu mwisho wa nyakati yamebadilika?

Au viongozi wameona tafsiri zake zimekuwa zikileta hofu, utata na ubashiri mwingi kiasi cha kuamua kuyaepuka?

Biblia bado inataja namba 666 katika Ufunuo 13:18, lakini Wakristo wa madhehebu mbalimbali wamekuwa na tafsiri tofauti kuhusu maana yake—wapo wanaoiona kama ishara ya mfano (symbolic), wengine huiona kama rejea ya mtu au utawala fulani wa kihistoria, na wengine wanaamini inahusu matukio yajayo.

Hakujawahi kuwa na makubaliano ya tafsiri moja kati ya madhehebu yote.

Swali langu ni hili:

- Kwa nini mada hizi zimepungua sana kwenye mahubiri?

- Ni kwa sababu ya mabadiliko ya teolojia?

- Ni kwa sababu waumini wa sasa wanahitaji mafundisho yanayogusa maisha ya kila siku?

- Au bado zinafundishwa, ila si kwa kiwango cha zamani?

- Mbona zama tulizopo kuna kulazimishana saaana kutumia cashless transactions na kupatiwa namba tambulishi, je walokole hizi ndio dalili za ujio wa 666 na mpinga Kristo?!

Ningependa kusikia maoni yenu, hasa wale wanaohudhuria makanisa ya madhehebu tofauti.
Wakati hao hao ndo wasambazaji wakuu.

BTW sidhani kama kuna kitu kinaitwa mpinga kristo nje ya vitabu
 
Kwanza hilo jambo fundisho lake ni gumu sana kufundisha mpaka mtu akuelewe. Pili naona wachungaji wengi wamegundua kuwa hilo suala ujio wake sio leo Wala kesho ni wakati ujao sana.

Tatu uhalisia wa maisha yetu ya Sasa hauitaji mambo hayo ya mpinga kristo zaidi unahitaji imani thabiti juu ya kristo na utakatifu imara dhidi ya dhambi sio upinga kristo. Wakati ukifika watakao kuwepo watafundishwa Wacha Sasa hivi watu wajikite kwenye kufundisha imani kama msingi wa kila kitu na utakatifu kama msingi wa kumuona aliye juu.
 
Back
Top Bottom