Makanisa mengi ya kilokole hapa Bongo hayafundishi tena kuhusu Mpinga Kristo & 666. Kulikoni?

Makanisa mengi ya kilokole hapa Bongo hayafundishi tena kuhusu Mpinga Kristo & 666. Kulikoni?

Nitaji
Nitajie dheebu Moja tu la ukiristo ambolo halikitoka katika ubavu wa Romani Catholic?
Nakushauri tu usome historia ya ukristo au hata na secular history ili upate ukomavu. Maana naona kama unasema ukristo ulianzia na wakatoliki.
 
Nitaji
Nitajie dheebu Moja tu la ukiristo ambolo halikitoka katika ubavu wa Romani Catholic?
Labda kwa ufupi. Kabla ya Nicea Council imani juu ya Yesu haikuwa unified. Kila mtu na lwake. Baadae tena kukatokea mgawanyiko ndio hayo madhehebu unayoyaona leo.
 
Sadaka ya kujimaliza 😀
Ndio akili ya mwafrika ilipofikia hapo. Tutabaki nyuma na kuwa watu wa kudharaulika tu. Wenzetu wanatumia vizuri akili sisi tunafukia akili kwenye mavumbi tunakimbizana kwenda makanisani kuomba miujiiza. Hizi teknolojia tunazotumia wenzetu waliomba miujiza au walijua Mungu amewapa akili so it is their responsibility to develop ideas? Ni aibu.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma mahubiri kuhusu Mpinga Kristo, alama ya mnyama (666) na kitabu cha Ufunuo yalikuwa kawaida sana kuyasikia kuanzia makanisa ya kilokole vijijini huko hadi yale makubwa ya akina askofu Mwakatage na Mwenisongole mijini huku!

Kila baada ya muda ungeyasikia madhabahuni.

Leo ukitembelea makanisa mengi, msisitizo unaonekana kuhamia kwenye mafanikio, ndoa, biashara, uponyaji, ukombozi na maendeleo ya maisha ya kila siku.

Je, mafundisho kuhusu mwisho wa nyakati yamebadilika?

Au viongozi wameona tafsiri zake zimekuwa zikileta hofu, utata na ubashiri mwingi kiasi cha kuamua kuyaepuka?

Biblia bado inataja namba 666 katika Ufunuo 13:18, lakini Wakristo wa madhehebu mbalimbali wamekuwa na tafsiri tofauti kuhusu maana yake—wapo wanaoiona kama ishara ya mfano (symbolic), wengine huiona kama rejea ya mtu au utawala fulani wa kihistoria, na wengine wanaamini inahusu matukio yajayo.

Hakujawahi kuwa na makubaliano ya tafsiri moja kati ya madhehebu yote.

Swali langu ni hili:

- Kwa nini mada hizi zimepungua sana kwenye mahubiri?

- Ni kwa sababu ya mabadiliko ya teolojia?

- Ni kwa sababu waumini wa sasa wanahitaji mafundisho yanayogusa maisha ya kila siku?

- Au bado zinafundishwa, ila si kwa kiwango cha zamani?

- Mbona zama tulizopo kuna kulazimishana saaana kutumia cashless transactions na kupatiwa namba tambulishi, je walokole hizi ndio dalili za ujio wa 666 na mpinga Kristo?!

Ningependa kusikia maoni yenu, hasa wale wanaohudhuria makanisa ya madhehebu tofauti.
Toka kuumbwa kwa mwanadamu wa kwanza hapajatokea mwanadamu aliyeitawala dunia na hata kujiinuwa nafsi yake juu na kujifanya yeye ndiye mungu hapa duniani, hata kujifanya ndiye pekee astahiliye hicho cheo mbele ya wanadamu wote duniani na kulazimisha aabudiwe na watu wote duniani, rejea 2 Wathesalonike 2:3-4

Maandiko yanatuonyesha anguko la kwanza la Adamu akiwa katika bustani ya Eden, rejea Mwanzo 3:1-24. Sura hii ndiyo ilikuwa ni yenye kuonyesha uasi wa Adamu wa kwanza hata kuiingiza uzao wote wa wanadamu katika hatia ya dhambi na mauti. Huyu ndiye Adamu wa kwanza mwenye tafsiri ya namba ya kibinadamu 6.

Lakini katika ramani ya mpango wa wokovu ili kuzishinda nguvu za mauti ilipasa aje Adamu wa pili. Hi ilitokana na sababu ya kuwa hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi ambaye angeweza kufanya hivyo, rejea Ufunuo 5:3-10. Ujio wa Yesu Kristo na kuweza kuzishinda nguvu za mauti na kuzimu akawa Adamu wa pili yaani namba ya kipekee kabisa akiwa ni Mwana wa Mungu yaani mwenye tafsiri ya namba 66 rejea 1 Wakorintho 15:22-29, Waebrania 1:1-14, Ufunuo 1:17-18.

Mwisho wa dhambi, mauti na kuzimu utatokea atakapo funuliwa mpinga Kristo, ataingia jukwaani kwa maigizo kama mtu wa haki, ni mpanda farasi asiyefahamika jina lake lakini amempanda farasi mweupe rejea Ufunuo 6:1-2 lakini Kristo halisi na wa kweli hutambulika kwa jina lake, na ndiye pekee mwenye mamlaka ya kumpanda farasi halisi mweupe, rejea Ufunuo 19:11-16

Kufinuliwa rasmi kwa huyu Adamu wa tatu ndipo utimilifu wa wokovu utakapotimia. Huyu mtu wa kuasi ndiye atakayebeba nafsi ya chapa halisi ya Ibilisi mwenyewe katika umbile la kibidamu, ndiye atakaye ibeba tafsiri ya namba 666 na jina lake halisi ni Mauti na kuzimu itamfuata nyuma yake, rejea Ufunuo 6:7-8, 1 Wakorintho 15:26-28

Kwa hiyo kupitia tafsiri ya namba za kimaandiko hapa tunapa ufahamu kuwa,

*6 ikiwa moja ni namba ya Adamu wa kwanza rejea Mwanzo 1:26-31, 5:12

*66 yaani 6 zikiwa mbili ni Adamu wa pili ambaye ndiye Yesu Kristo rejea Mithali 8:22-31, Yohana 1:17-18, 17:1-5, 1 Wakorintho 15:20-23

*666 yaani 6 zikiwa mpangilio wa 6 tatu ni Adamu wa tatu ambaye ndiye mpinga Kristo rejea Ufunuo 13:18

Huyu Adamu wa tatu ndiye atakaye ipeleka dunia katika mwisho wa historia na mwisho wa wakovu hata idadi ya warithi wa ufalme ujao wa Mungu ipate kutimia. Huyu atakuwa ndiye Adamu atakaye pewa mamlaka ya kidini na kiserikali apate kuitawala dunia yote kwa siku 1,260.

Hawa Adamu watatu ndiyo wanadamu pekee waliopata kibali cha mbingu juu ya utawala wa vitu vyote duniani. Hii ndiyo pattern ya 666 yenye mpangilio wa kutupeleka kwenye uasi mkuu wa kidunia kutokea katika mnara wa Babeli. Wa kwanza na wa pili walipata kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini watatu atakuja kukabidhiwa Ibilisi na nabii wa uwongo na kuunda roho 3 za uchafu mfano wa vyura zipotoshao watu wote.
 
Siku hizi kuna wachungaji vijana hata hawajui kufundisha vitabu vya ufunuo na danieli. Unakuta mchungaji ni kijana anachofurahia ni kurukaruka na praise and worship wale kundi kubwa kama kwaya wanajaa madhabahuni na nyimbo zisizo na upako
Hata hao wa zamani ni waongo na wapotoshaji ...
 
Toka kuumbwa kwa mwanadamu wa kwanza hapajatokea mwanadamu aliyeitawala dunia na hata kujiinuwa nafsi yake juu na kujifanya yeye ndiye mungu hapa duniani, hata kujifanya ndiye pekee astahiliye hicho cheo mbele ya wanadamu wote duniani na kulazimisha aabudiwe na watu wote duniani, rejea 2 Wathesalonike 2:3-4

Maandiko yanatuonyesha anguko la kwanza la Adamu akiwa katika bustani ya Eden, rejea Mwanzo 3:1-24. Sura hii ndiyo ilikuwa ni yenye kuonyesha uasi wa Adamu wa kwanza hata kuiingiza uzao wote wa wanadamu katika hatia ya dhambi na mauti. Huyu ndiye Adamu wa kwanza mwenye tafsiri ya namba ya kibinadamu 6.

Lakini katika ramani ya mpango wa wokovu ili kuzishinda nguvu za mauti ilipasa aje Adamu wa pili. Hi ilitokana na sababu ya kuwa hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi ambaye angeweza kufanya hivyo, rejea Ufunuo 5:3-10. Ujio wa Yesu Kristo na kuweza kuzishinda nguvu za mauti na kuzimu akawa Adamu wa pili yaani namba ya kipekee kabisa akiwa ni Mwana wa Mungu yaani mwenye tafsiri ya namba 66 rejea 1 Wakorintho 15:22-29, Waebrania 1:1-14, Ufunuo 1:17-18.

Mwisho wa dhambi, mauti na kuzimu utatokea atakapo funuliwa mpinga Kristo, ataingia jukwaani kwa maigizo kama mtu wa haki, ni mpanda farasi asiyefahamika jina lake lakini amempanda farasi mweupe rejea Ufunuo 6:1-2 lakini Kristo halisi na wa kweli hutambulika kwa jina lake, na ndiye pekee mwenye mamlaka ya kumpanda farasi halisi mweupe, rejea Ufunuo 19:11-16

Kufinuliwa rasmi kwa huyu Adamu wa tatu ndipo utimilifu wa wokovu utakapotimia. Huyu mtu wa kuasi ndiye atakayebeba nafsi ya chapa halisi ya Ibilisi mwenyewe katika umbile la kibidamu, ndiye atakaye ibeba tafsiri ya namba 666 na jina lake halisi ni Mauti na kuzimu itamfuata nyuma yake, rejea Ufunuo 6:7-8, 1 Wakorintho 15:26-28

Kwa hiyo kupitia tafsiri ya namba za kimaandiko hapa tunapa ufahamu kuwa,

*6 ikiwa moja ni namba ya Adamu wa kwanza rejea Mwanzo 1:26-31, 5:12

*66 yaani 6 zikiwa mbili ni Adamu wa pili ambaye ndiye Yesu Kristo rejea Mithali 8:22-31, Yohana 1:17-18, 17:1-5, 1 Wakorintho 15:20-23

*666 yaani 6 zikiwa mpangilio wa 6 tatu ni Adamu wa tatu ambaye ndiye mpinga Kristo rejea Ufunuo 13:18

Huyu Adamu wa tatu ndiye atakaye ipeleka dunia katika mwisho wa historia na mwisho wa wakovu hata idadi ya warithi wa ufalme ujao wa Mungu ipate kutimia. Huyu atakuwa ndiye Adamu atakaye pewa mamlaka ya kidini na kiserikali apate kuitawala dunia yote kwa siku 1,260.

Hawa Adamu watatu ndiyo wanadamu pekee waliopata kibali cha mbingu juu ya utawala wa vitu vyote duniani. Hii ndiyo pattern ya 666 yenye mpangilio wa kutupeleka kwenye uasi mkuu wa kidunia kutokea katika mnara wa Babeli. Wa kwanza na wa pili walipata kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini watatu atakuja kukabidhiwa Ibilisi na nabii wa uwongo na kuunda roho 3 za uchafu mfano wa vyura zipotoshao watu wote.
Mafundissho uliyo lishwa ni ya UONGO .... 666 NI MWANADAMU ...
Kuna maandiko yanaendelea kumfafanua huyo mnyama yana sema ....huyo mnyama 666, watu wakashangaa "alikuwepo kicha akapotea kisha akawako tena mara ya tatu anapanda kwenda kwenye uhalibifu ....maana ya haya maneno ni MAISHA YA MWANADAMU KUISHI NA KUFA NA KUFUFULIWA SIKU YA KIAMA NA KUTUMPWA JEHANAM KWA HAO WALIO FUATA TAMAA ZA MWILI ...
666 NI MWILI WAKO BINADAMU ...utakuwako , utakufa na utafufuliwa
 
Mafundisho yote mliyo pewa na hao wahuni ni uongo mtupu ...labda wewe unapenda kudanganywa na wahuni wa dini ...mfano ni hiyo 666 ...jibu sahihi kwa asilimia 100% la 666 ni MWILI WAKO MWANADAMU.(666=MWILI WA BINADAMU) je mleta uzi ulisha sikia mtumishi gani au kanisa gani au mitume gani wakisema hivi? ..wote wanakuja na porojo za alinacha.
Mwili wa binadamu sio 666. Umekosea
Ila una jambo la msingi sana kusikilizwa

Uko sahihi
 
💥666 ni mwili wako mwanadamu.
💥 chapa kwenye paji la uso ni nia ovu
💥chapa kwenye mikono ni matendo maovu (yaani kuitimiza hiyo nia ovu kivitendo)
💥kuto kuuza wala kununua isipokuwa wana chapa ya huyo mnyama ..maana yako ni matendo yote ya binadamu yata tawaliwa na dhambi ya tamaa ovu za miili (usifuate tamaa za mwili)
💥chapa ..maana yake ni dhambi...dhambi ndiyo sababu pekee ya watu kutupwa jehanam.
Hapa umeharibu kidogo
But una kitu
 
Hapa umeharibu kidogo
But una kitu
1)666 ni mwili wako mwanadamu
2)chapa ni dhambi
3)chapa ya huyo 666 kwenye mkono ni matendo maovu ya dhambi.
4)chapa ya huyo 666 kwenye paji ni nia ovu za dhambi.
5)kutokuuza wala kununua isipokuwa wana chapa ya mnyama maana yake ni kuwa mwanadamu atatawaliwa na tamaa ovu za mwili katika njia zake zote.
6)huyo mnyama kuwako kisha kutokuwako kisha watu wakashangaa kumwona tena huyo mnyama mara ya 3 maana yake ni "kuishi" na "kufa" na "kufufuliwa" siku ya kihama.
7)mnyama kuonekana mara ya tatu na kupanda kwenye uhalibifu maana yake Mungu atawafufua waovu wote na kuwapeleka jehanam.....

666=MWILI WA BINADAM
 
Mpinga Kristo wa kwanza ni Paulo na barua zake zote na mafundisho yeyote yanayoenda tofautu na Kristu

Mpinga Kristo ni elimu inayokinzana na alichokifundisha Yesu

Ingawa Ukristo kwa asilimia kubwa umekuwa ni chanzo cha kwanza kumpinga Kristo

Mimi ni mkatholic, nimepata mafundisho yote. Kabla sijawahi jua hili
Mfano mafundisho ya kubusu misalaba, mafundisho ya mafuta ya upako, mafundisho ya kunena kwa lugha pasi kujua ni lugha za kishetwani

Ila uhalisia ni kuwa makanisa asilimia 90 yanafundisha tofauti na alivyofundisha Yesu. Huu ndio kumpinga Kristu

YEsu hakuja kupinga Sabato kwa sababu yeye ndie Sabath, hii inafanya niwaze kwa nini ukristo uanzishwe na kupinga lile agano ambalo lilikuwepo toka awali

La mwisho nambari ya mpinga Kristo sio 666, number ya mwanadamu ni 616.
Uhalisia wake umepotezwa na watu sasa wakiamini ni 666. 666 haijawahi tatizo, ila 616 ni number ya mwanadanu katika upotevu, uharibifu

Umoja wetu na Holy One (Cheo Cha Bwana). Unaanzia agano la kale kupitia Musa na Agano jipya kupitia Kristu

Na mwenye masikio asikie.
 
Haya ni mafumbo mawili yenye maana moja ..nikama ndoto ya farao zilikuwa ndoto mbili ila maana ni moja.

Ufunuo 13:16–18 — inataja namba 666, inayohusishwa na “idadi ya mnyama.”
Ufunuo 17 — inaeleza kahaba mkuu, anayeketi juu ya mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi.
 
1)666 ni mwili wako mwanadamu
2)chapa ni dhambi
3)chapa ya huyo 666 kwenye mkono ni matendo maovu ya dhambi.
4)chapa ya huyo 666 kwenye paji ni nia ovu za dhambi.
5)kutokuuza wala kununua isipokuwa wana chapa ya mnyama maana yake ni kuwa mwanadamu atatawaliwa na tamaa ovu za mwili katika njia zake zote.
6)huyo mnyama kuwako kisha kutokuwako kisha watu wakashangaa kumwona tena huyo mnyama mara ya 3 maana yake ni "kuishi" na "kufa" na "kufufuliwa" siku ya kihama.
7)mnyama kuonekana mara ya tatu na kupanda kwenye uhalibifu maana yake Mungu atawafufua waovu wote na kuwapeleka jehanam.....

666=MWILI WA BINADAM
Elimu yako kuhusu hili swala ni ndogo bado ila nimependa unapenda kujifunza

Kuhusu moto na jehanamu😀
Kuna kifo na kuishi, Yesu alifundisha hili
SHinda kifo ili uishi, wengi watakufa na kupotea

Hayo mambo ya moto sijui jehanamu mengi yametengenezwa

Sisi ambao tunataka kuishi tutaishi kupitia Kristu

Way, Truth and Life
 
Mpinga Kristo wa kwanza ni Paulo na barua zake zote na mafundisho yeyote yanayoenda tofautu na Kristu

Mpinga Kristo ni elimu inayokinzana na alichokifundisha Yesu

Ingawa Ukristo kwa asilimia kubwa umekuwa ni chanzo cha kwanza kumpinga Kristo

Mimi ni mkatholic, nimepata mafundisho yote. Kabla sijawahi jua hili
Mfano mafundisho ya kubusu misalaba, mafundisho ya mafuta ya upako, mafundisho ya kunena kwa lugha pasi kujua ni lugha za kishetwani

Ila uhalisia ni kuwa makanisa asilimia 90 yanafundisha tofauti na alivyofundisha Yesu. Huu ndio kumpinga Kristu

YEsu hakuja kupinga Sabato kwa sababu yeye ndie Sabath, hii inafanya niwaze kwa nini ukristo uanzishwe na kupinga lile agano ambalo lilikuwepo toka awali

La mwisho nambari ya mpinga Kristo sio 666, number ya mwanadamu ni 616.
Uhalisia wake umepotezwa na watu sasa wakiamini ni 666. 666 haijawahi tatizo, ila 616 ni number ya mwanadanu katika upotevu, uharibifu

Umoja wetu na Holy One (Cheo Cha Bwana). Unaanzia agano la kale kupitia Musa na Agano jipya kupitia Kristu

Na mwenye masikio asikie.
NImesoma mafundisho ya paulo yapo sahihi kabisa tatizo ni lenu kushindwa kuielewa injili ...leta fundisho unalotilia shaka la paulo nikupe fafanuzi
 
Wasabato nao wameachana na mafundisho hayo, wanafundishana mambo ya afya na uchumi tu katika makambi yao
Kweli mkuu yani utamsikia Askofu, Mchungaji au Nabii kwenye Mahubili yake anazungumzia Uchawi na Utajiri na hawataki kuwaambia ukweli kondoo wao, Yani kila Jumapili kwenye ibada utasikia wewe masiki kwasababu Bibi yako alichukua nyota yako au unapitia matatizo kwasababu ya Mizimu ya ukoo wetu inataka urithi uchawi na Bibi yako huko kijijni amekufunga usifanikiwe kimaisha, unatakiwa ufungue vifungo ulivyofungwa na mizimu yenu.
 
NImesoma mafundisho ya paulo yapo sahihi kabisa tatizo ni lenu kushindwa kuielewa injili ...leta fundisho unalotilia shaka la paulo nikupe fafanuzi
Sawa. Sina cha kukueleza zaidi ya nilichokueleza

Nachokwambia ni kuwa unajua wayahudi walikuwa ni wasomi sana. Na waliandika vitabu vingi zaidi kuanzia torati, zaburi na mithali

Hujawahi kuwaza kwa nini vitabu vya agano jipya asilimia 90 vimeandikwa na wageni?

Kwa nini vitabu hivi vimeandikwa na mataifa kama ugiriki, Roma, Egpty na sio wayahudi.
Ili kutawala watu wazungu walikuja na Biblia, je ulishawahi kuwaza kwa nini?

Ni mpango wao siku nyingi kila siku wanabadilisha Biblia na tafsiri zake

Ila maandiko ya Wayahudi hayabadiliki yako vile vile
Ndio maana Biblia ya Ethopia pia inalindwa kwa asilimia kubwa

YEsu alitumia nguvu kubwa kuwafundisha mitume over years unahisi Yesu alikuwa hajui

Ila paulo alikuja kama mtume Muhammad anajua kila kitu.

YEsu alizunguka akifundisha alikuwa ni mwalimu, Rabbi. Ndio uhalisia wa jambo hili na mfundisho yake yanafichwa unapewa nusu nusu yanapotezwa

Kuhusu number 666 na number 616 unaweza ku google. Wagiriki wa mwanzo walichanganya, na hata ukisoma Biblia za zamani ni 616, unajua kwa nini?

Nakujibu maea ya mwisho. Tafuta maarifa acha kujifunza ni njia sahihi ya kujiweka karibu na Mungu. Na anapenda wanaojifunza.
 
Asaiv watu wengi wanapata taarifa na wanazichuja..Hiko kitambo Social media hazikuweko kwa ukubwa hivo.

Asaiv hata Mchungaji akitoa boko watu wanaelewa na wana mdiscuss.

Jana nimekutana na wasabato Mkoa X wanawapondea vibaya mno watoa mada kwenye makambi yao kuwa wanawapigisha watu hadith hakuna jipya lolote na hawawaelewei.
 
Back
Top Bottom