Makanisa mengi ya kilokole hapa Bongo hayafundishi tena kuhusu Mpinga Kristo & 666. Kulikoni?

Kabisa. Udhaifu wao umesababisha watu tunaishi maisha ya dhambi na kujisahau, ukienda church msisitizo mkubwa upo ktk mambo ya mwili fedha na mafundisho kidogo sana ya imani...watu wamekuwa wazinzi waasherati wala rushwa na kubwa zaidi wasiotaka kukosolewa

Wachungaji maaskofu mitume na manabii wanawania idadi ya waumini iwe kubwa wanaogopa kuwahubiria ukweli
 
Umenikumbusha mchungaji wangu mzee Mwaisabhila
 
Wengi pia hawajaingia deep kuyasoma hayo mafundisho na kuyaelewa kiundani kwa level kama alizokuwa nazo mtumishi Moses Kulola (nimetolea mfano). So hawajui hata wafundishe nini, hata ile ufunuo wanaisoma lakini hawaielewi kwa undani ule unaotakiwa.
Ndio maana walianza kusema Pope John Paul II, ndio mpinga Kristo, akafa wakabadilisha, na mpaka sasa wanasema huyu mpya ndio mpinga Kristo, akifa watabadilisha tena 🤔
 
Mkuu hapa nielimishe zaidi sijakuelewa. Enlighten tafadhali
 
Kwa hiyo wanabadili gia angani
 
Mkuu hapa nielimishe zaidi sijakuelewa. Enlighten tafadhali
💥666 ni mwili wako mwanadamu.
💥 chapa kwenye paji la uso ni nia ovu
💥chapa kwenye mikono ni matendo maovu (yaani kuitimiza hiyo nia ovu kivitendo)
💥kuto kuuza wala kununua isipokuwa wana chapa ya huyo mnyama ..maana yako ni matendo yote ya binadamu yata tawaliwa na dhambi ya tamaa ovu za miili (usifuate tamaa za mwili)
💥chapa ..maana yake ni dhambi...dhambi ndiyo sababu pekee ya watu kutupwa jehanam.
 
Walifikiri ukatoliki ungeeondk kisa kelele zao, oh mpinga Kristo, sjui mpinga Musa......

Wasile wakashiba hasa masalia hawana afya kila kitu kwao ni mwiko
 
wengi pia walikuwa hawana elim ya philosophia, muhubiri ili awe kweli ameshiba knowledge basi yampasa amjue Emmanuel Kant, amjue Spinnozer, Augustin,...
na kadiri vizazi vinavyopata shule hawa wanaofanya miujiza siku zao zahesabika.
 
Siku hizi kuna wachungaji vijana hata hawajui kufundisha vitabu vya ufunuo na danieli. Unakuta mchungaji ni kijana anachofurahia ni kurukaruka na praise and worship wale kundi kubwa kama kwaya wanajaa madhabahuni na nyimbo zisizo na upako
 
mkumbuke na mzee Kulola na habari ya mpinga kristo kwenye gazeti la Msemakweli alilokuwa anatembea nalo kama rejea kwenye mikutano yake ya injili mikoani
Ila nachojua Kulola alikuwa Mwinjilisti zaidi kuliko mwalimu...mwalimu mzuri wa hili fundisho huwa ni mchungaji Munisi wa Kawe, Magembe na wengine
Siku hizi kuna wachungaji vijana hata hawajui kufundisha vitabu vya ufunuo na danieli. Unakuta mchungaji ni kijana anachofurahia ni kurukaruka na praise and worship wale kundi kubwa kama kwaya wanajaa madhabahuni na nyimbo zisizo na upako
Na kununua magari ya kifahari! Hilo ndio wanajua...yaani bora wasijenge kanisa, wasipeleke injili, wasisaidie jamii ila wanunue gari la milioni 200
 
siku hizi michango ni mingi kuliko mahubiri na kingine siku hizi ukiwa na pesa hata utende kosa gani kanisani wala hawakutengi kama ilivyokuwa zaman.
 
Huenda sasa wameelewa teolojia sahihi. Unaposoma unabii katikav biblia lazima utumie Biblical criticism na siyo kusoma kana kwamba unasoma utabiri wa hali ya hewa kwenye gazette. Lazima kwanza ujue mwandishi alikuwa anaandikia hadhira ipi na namnna hadhira ile ilivyoelewa ujumbe ule. Hiyo habari ya 666 na mwisho wz dunia waliandikiwa watu waliokuwa kwenye dhiki kubwa chini ya utawala wa Warumi. Wao walielewa vena kabisa symbolic language.ya kitabu cha Ufunuo. Siku hizi wanatheolojia wanahaha kutafsiri mambo ambayo yalishatokea kuwa ni prophecy to be fulfilled in the future. Mambo ya hovyo tu huko kwenye vyuo vya teolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…