Makanisa mengi ya kilokole hapa Bongo hayafundishi tena kuhusu Mpinga Kristo & 666. Kulikoni?

Serikali ilitakiwa iwazibiti mana Nabii na Maaskofu wanaotumia Viwanja vya Serikali kufanya shughuli zao za Ibada mfano Mwamposa anatakiwa afukuzwe pale kawe na kule Coco beach umejengwa msikiti uondolewe inakuaje Taasisi ya Dini au Nabii au Askofu ajenge Nyimba ya ibada kwenye Viwanja vya Public, nchi hii inamaeneo Mengi kwanini wasinunue Viwanja vyao wajenge Makanisa yao na Misikiti yao, Mfano pale Coco Beach umejengwa Msikiti sehemu ya starehe sasa wananchi siku ya sikukuu wakija kustarehe na wapenzi wao na wakinywa pombe na kushikana maziwa pembeni ya msikiti nani atakua mchokozi?
 
Mbona jibu la swali lako..lilisemwa na Yesu mwenyewe ...wayahudi na waisrael walimkataa Yesu kwa asilimia kubwa hadi leo.. ndipo Yesu mwenyewe akasema ..."NYUMBA YENU MMEACHIWA UKIWA" haya maneno ya Yesu ndiyo jibu la swali lako ...kwa hiyo Israel siyo taifa teule tena kama ilivyo kuwa zamani ndiyo maana wamekataa mafundisho ya INJILI YA YESU HATA SASA.
 
BAsi sawa

Kuwa kama mtoto, futa kila ulichokariri mwanzo, anza upya.

Mpinga Kristu unayemtafuta yupo anafanya kazi zake kila kukicha. Na anashinda hiyo kazi kwa sababu kila siku anaitafsiri Biblia anavyotaka Yeye

Kila swali nililokuuliza andika chini, andika yafanyie kazi

Achana na mafundisho ya kujibu maswali magumu kirahisi.
Wayahudi wana maandiko mengi mengine wameweka online mengine hawajaweka. Ila humu kuna vitabu au maandiko zaidi ya 3000/- 👇



Kuwa kama mtoto mdogo, anza upya kujifunza.

Asante kwa kunipa mda wako.
 
Mungu akuwahi kuleta kitabu chochote duniani siyo msahafu wala biblia wala torati wala zaburi waoa injili ...Mungu alicho leta duniani ni NENO LAKE ...Na wanadamu kuunda vitabu kwa kupitia hilo neno hivyo tambua kuwa Mungu kamfunua shetani duniani kama ujuavyo kuwa, kwa mujibu wa Mungu mwenyewe, shetani yupo na yupo kwa kazi maalumu nayo ni kuipotosha kweli ya Mungu na kuwapotosha wanadamu ..hivyo mafundisho na maandiko potovu yanayo ingizwa kwenye neno la Mungu hayo ni ya shetani siyo ya Mungu ...Mungu kamruhusu shetani kuwajaribu watu na kwa sababu hiyo yupo.
 
Kuhusu mpinga kristo ni kama shetani tu yupo kwa kazi ya kuipotosha kweli kuwa uongo na uongo kuwa kweli sijapinga ila mimi naijua injili ya kweli kwa asilimia 100 ni tofauti kabisa na injili za makanisani za sasa au injili za madhehebuni ...hata neno MADHEHEBU NI PROJECT YA SHETANI KWENYE DINI YA KWELI HAKUNA MADHEHEBU
 
Mimi ni mwalimu wako, nakufundisha acha ku argue with me.

Kuna uongo mkuwa sana ndio maana unona hata majina yametafsiriwa kwenye Biblia. Jina la mtu linatafsiriwaje? Dunia hii Yesu ana majina mengi mno, ambayo sio uhalisia wake. Watu wanajiita wakristu hata jina la Mungu wanayemuomba hawalijui. Utasikia Adonai, adonai maana yake kiswahili ni Bwana.

Yesu anakupenda sana. Yesu anataka ushike mafundisho Yake. Uishi mafundisho Yake. Upate uzima wa milele

Uzima wa milele sio kuokoka wala sio kutubu. Uzima wa milele hupati ukishakufa. Usifikiri utakufa ndio ufufuke, hapana. Utaishi hata kifo hakimpati yeye ANAYEISHI.

Sio kwamba Yesu alikufa akafufuka. Ni upotofu. Mwili ulikufa roho ya Yesu haijawahi kufa. Alikuwa hai hata akipopata mauti ya mwili

Usitegemee eti utakufa ndio ufufuke. Si kweli, roho iliyokufa imekufa. Roho Yako iweze kuishi inaishi hata baada ya kifo. Wengi watakufa.

Haya mambo ya motoni achana nayo. Kuna maisha na kuna kifo, tafuta KUISHI

Nenda kasome Injili zote 4. Ona jinsi mpinga kristo amavyoleta ukinzani. Soma kwa umakini Usinijibu. 👇👇

Mathayo 28:1–10 — Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walifika kaburini. Kulikuwa na malaika mmoja aliyeketi juu ya jiwe.

Marko 16:1–8 — Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo, na Salome walifika. Walimkuta kijana mmoja aliyevaa vazi jeupe ndani ya kaburi.

Luka 24:1–12 — Wanawake kadhaa walifika, akiwemo Mariamu Magdalena, Yoana, na Mariamu mama yake Yakobo. Waliona wanaume wawili waliovaa mavazi yenye kung'aa.

Yohana 20:1–18 — Mariamu Magdalena alifika kwanza na kuona jiwe limeondolewa. Baadaye Petro na mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. Mariamu aliwaona malaika wawili ndani ya kaburi.

Leo jioni tunaingia Sabato, Bwana wa Sabato akuongoze kujua yake ambayo yamefichwa na kushikiliwa na upotevu.
Kafanye kazi zako kama kawaida ila kikubwa usisahau kujifunza niliyokufundisha.
 
Anayejua hiyo namba 666 imetokana na hesabu gan anisaidie
 
Hakuna cha ualimu wowote ulionao jina ni kama lugha tu ...usiwe mpumbavu kama waislamu wanaodhani mungu anasikia kiarabu tu ...mungu aangalii tamshi bali dhamira ya ndani inayo beba tamshi husika ...ndiyo maana kuna neno moja linaweza kuwa ni tusi kwa lugha fulani ila ni jema kwa lugha nyingine. Hivyo Yesu au Mungu kuitwa mungu badala ya Allah au God au Yehova siyo kosa ...tumia akili wacha kuwa mpumbavu kisha unajiita mwalimu wa upumbavu .... 666= mwili wake mwanadamu....hakuna fafanuzi ya kweli zaidi ya hii ..tena imeandikwa "hapo ndipo ilipo subira ya watakatifu" yaani watakatifu wote hufanya juhudi na subira ya kuzishinda tamaa za mwili ndiyo maana yake.
 
Anayejua hiyo namba 666 imetokana na hesabu gan anisaidi
666 = ni hesabu ya kibinadamu maana yake ni MWILI WAKO ...TENA MWILI WA BINADAMU NDIYO MILANGO YA KUZIMU HIVYO KUISHINDA MILANGO YA KUZIMU MAANA YAKE NI KUZISHINDA TAMAA(NGUVU) ZA MWILI
 
666 = ni hesabu ya kibinadamu maana yake ni MWILI WAKO ...TENA MWILI WA BINADAMU NDIYO MILANGO YA KUZIMU HIVYO KUISHINDA MILANGO YA KUXIMU MAANA YAKE NI KUZISHINDA TAMAA ZA MWILI
asante sana
Nachojiuliza why watumie 666 kwanin wasitumie 555?
 
asante sana
Nachojiuliza why watumie 666 kwanin wasitumie 555?
Hata 555 siyo kosa ni fumbo ...ndoto ya farao aliota ng'ombe na masuke ..usiseme kwa nini asiote mbuzi na mihogo, ni nosense ...666 ni fumbo tu cha muhimu kwenye fumbo ni jibu sahihi.
 
asante sana
Nachojiuliza why watumie 666 kwanin wasitumie 555?
Hata 555 siyo kosa ni fumbo ...ndoto ya farao aliota ng'ombe na masuke ..usiseme kwa nini asiote mbuzi na mihogo, ni "nosense" ...666 ni fumbo tu cha muhimu kwenye fumbo ni jibu sahihi
 
Sawa.
 
Injili unayo ieleza hapa ina makosa mengi pia ...mfano kuhusu watakatifu kufa na kuwa hai ...hapa upo sahihi kwa namna moja ila umekosea kufaham namna ya pili .. wapo watakatifu ambao wamekufa mwili na nafsi na wapo watakatifu ambao wamekufa mwili tu bali nafsi zao zinaishi mbinguni yaani wapo hai mbinguni ...ndiyo maana MUNGU AKASEMA KUWA WALE WATAKATIFU WALIO TANGULIA MBUNGUNI AWATAINGIA KWENYE PEPO TEULE MPAKA WATAKATIFU WALIOPO MAKABURINI MWILI NA NAFSI WATAKAPO FUFULIWA SIKU YA KIAMA NA KUINGIA PAMOJA KWENYE MAKAO MAPYA WA WATAKATIFU WALIOTOKEA DUNIANI ...TENA IMEANDIKWA KUWA WALE WATAKATIFU WALIO LALA MAKABURINI WATASEMA SIKU YA KIAMA ITAKAPO KARIBIA KUWA "MUNGU NI HADI LINI KUJA KUHUKUMU" hivyo siyo watakatifu wote wanao kufa nafsi zao xipo hai mbinguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…