Makanisa yanalipa sana! Pastor Tonny Kapola anunua eneo kwa dola milioni tatu Mwenge kwa ajili ya kujenga Kanisa

Mtu anatoa Sadaka ya million 400 yeye anaingiza pesa kiasi gani? Pesa haijawahi kuwa rahisi hivyo
 
Spot on. Hawa watu wana siri nyingi sana sema tu mifumo yetu nayo ni mibovu kwa kujaa rushwa sana.

Hakika kama mifumo yetu ingekuwa makini hawa watu wangekuwa wanaumbuliwa mchana kweupe na kuishia gerezani.
Mifumo ya TZ iko makini na inajua kila kitu sema tatizo rushwa.
 
Dah Sasa hio naona inachukua mda Hadi mtu akuzoee na achilia mbali hilo kua nae karibu utamuonea wapi mtu Yuko angani anaonekana kwa nadra, naona Bora awepo mtu "maalum" wa kurahisisha kwa wanaotaka kuingia "sirini"
Nitakupa mfano mdogo, kuna dada mmoja ndoto zake ilikuwa ni kuwa na mahusiano na watu wazito. Yeye alikuwa ameajiriwa kwenye benki fulani kama 'cashier'

Alichofanya, aliamua kutumia kipato chake kidogo kujigaramia muonekano wake pamoja na mavazi ili aweze kuendana na watu wazito.

Akafanya utafiti, hawa watu wazito huwa wanaenda kula chakula au bata wapi? Baada ya kupata jibu, akagundua huwa wanaenda kwenye yale maeneo ambapo soda ya kawaida uuzwa 5000.

Akajichanga kiasi, akaamua wikiend moja akatembelee yale maeneo huku akijihudumia maji na soda.

Wale watu wazito walipomuona mazingira yale, wakajua ni mwenzao; ndipo mahusiano na ndoto yake ya kuwa na watu wazito ilipoanzia.
 
Sadaka zinafanya kazi makanisa ya mabati tu yale ya Tabata Upogoroni na Kimara bonyokwa labda😂,,, kwa hawa wenye Ministries za kishua kina Kapola na Dale wana deal na mambo mazito zaidi.
Hayo mambo ndio yapi hayo mkuu namimi nifungue kanisa.
 
sadaka za waumini zimemuwezesha kununua eneo ili ajenge kanisa, sio ili ajenge nyumba au mradi wake. Shida iko wapi?
Shida ipo hivi.....

Mungu hakaagi kwenye mijengo ya kifahari bali hukaa mioyoni mwa hao wamuabudio katika roho na kweli.

Ukiujua huu ukweli ndo utaelewa kuwa hao wajenga mijengo ya kifahari ni wezi tu majambazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…