Ngiama makanda
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,208
- 3,938
Yeye kakimbilia nanenane stendi, angetega pale makole opp na cbe usafiri upo 24hrsWalio kuambia hakuna mabasi ya usiku walikudanganya.
Karne hii ya teknolijia bado unaenda stendi kubajatisha usafiri? Sasa hiyo smartphone yako ina kazi gani?
Ha ha ha .... 😀😀 Unanisaidia kujua kuwa Dodoma mnaongoza kwa kukusanya mapato?😳😳Kwa kukusaidia tu Dom wanaongoza mapato ya halmashauri Tanzania na mapato ya TRA wapo top 5
Ubora wa mji wowote duniani haupimwi kwa eti "kuchangamka usiku" ingekua hivyo nadhani Las Vegas ingekua inaongoza Marekani kupita hata New York au Los Angeles.
Dodoma wanaongoza Tanzania kwa mipangomiji bora,miundombinu,mtandao mpana wa barabara za lami,miradi mingi inayojengwa na inayotarajiwa kujengwa n.k
Kwani uzi unasemaje?Sisi ndo wakaz wa Dodoma wenyewe, ukiongea Dodoma, usiongelee pale Jamatini pekeake. Nenda huko Mpwayungu, sanzaa, kondoa huko!, pita pale mto bubu!! Uone Kama Kuna daraja lolote mpka sasahivi tangu lile la Mwanzo kusombwa na maji.
Msiishie Laptrona, The bistral, Chakonichako, Rainbow, au Bambalaga... Nenda huko chipanga, chiguruka na chikopelo angalia Hali halisi.
Dodoma haishii Jamatini na Nyerere square
Nimependa ulivyojitahidi kutetea Dodoma kwa mantiki ya karne ya 20, huku ground ikiwa giza saa mbili na stendi ikifanana na hifadhi ya Taifa.Masaa ya ofisi za serikali / bunge ni asubuhi , mchana hadi jioni , SIYO USIKU.
Sasa wewe ulikuwaunatafuta MACHANGU au Mabasi ?
Abiria mmoja mabasi matatu hayakutoshi ?
Kumbukakuwa, makao makuu yanapaswa kuwa katika mkoa ambao una utulivu na upo in-ze mido ya nchi , ili waheshimiwa waweze kukutana kwa urahisi na waweze kufocus. Ndiyo maana Dar haina sifa ya kuwa makao makuu ya nchi, makelele ni mengi, hali mbaya ya hewa, mabasi ni mengi sana [ sori nimemaanisha machangu]
Kila la kheri mkuu, I hope ulikuwa mbunifu ukatumia mkono kujituliza baada ya kutofanikiwa kupata mabasi ya usiku.
Acha dharau zisizo na kichwa.Wenzake wanapandia gari Makole yeye unapuyanga kwenda 8 8 usiku.
Nimecheka sana ulivyopiga hasira kwa hoja ya kawaida ya ground – siasa ya kusafirisha mizigo kwenye mabasi halafu abiria wapande SGR au ndege usiku? Hiyo ni version yenu ya “technology ya taifa” labda.Interview itakuwa imekuvuruga wewe, aliyekuambia.Dodoma hakuna usafiri wa usiku nani? Kwamba ulifika stendi ukauliza wauza maji na matunda kwenye mabasi wakujibu wakati Hadi unamuuliza hajauza hata chupa.moja akujibu nini? Labda nikusaidie hakuna mkoa wenye usafiri mwingi Kama Dodoma, hapa hapa Dodoma kuna mabasi yanoyosafiri usiku, mtu anatoka Dodoma saa nne usku saa tatu asubuhi yupo Zanzibar. Kama ulikosa gari la kurudi kijijini kwenu nitakuelewa maana magari ya vijijini yako pembeni mwa mji. Dodoma ipo katikati ya nchi kuna mageri ya kwenda mikoa karibu yote wewe ulitaka usafiri wa wapi ukaukosa na basi zote lazima ziingie stand kuu Kama Magufuli wanavyofanya. Wewe ulikurupuka kwenda kufanya interview bila kujiandaa unaona matokeo yake, siku nyingine jiandae anayeijua Dodoma akisoma uzi wako atakushangaa Sana. Halafu basi zetu siku hizi ni za mizigo na abiria wachache, tunasafirisha mizigo kwenye basi tunapanda SGR au ndege tukifika jiona tunakwenda kuchukua mizigo yetu iliyosafirishwa kwa mabasi, sema lingine sio usafiri
Kwanza kabisa, sijawahi kutumia Facebook – so hiyo “rudi Facebook” ni attempt ya dhihaka isiyofika.Yaani mtu unajadili eti "uchangamfu wa mji usiku" 😂😂 kwako ndio kigezo cha kupima ubora wa Jiji duuh rudi facebook.
Nilitegemea ungejadili hivi vitu kama mtu aliyeenda shule👇👇
-Mipangomiji
-Mtandao mpana wa barabara za lami
-Miundombinu
-Huduma za Kijamii
-Vyuo Vikuu
-Mapato(Halmashauri+TRA)
-Viwanda
-Uwepo wa mashirika ya kimataifa
-Ofisi nyingi za serikali
-Maghorofa
-Miradi ya ujenzi inayojengwa na inayotarajiwa kujenga n.k
Mkuu umeenda mbali, huwezi linganisha nchi hizo na Tz. Wale wako mbali.Wabongo wanashindwa kutofautisha Jiji la kibiashara na jiji(mji) wa kiserikali.
Jiji au mji wa kibiashara mara nyingi uko busy zaidi kuliko capital city. Refer nchi kama Morocco, South Africa, USA, Ivory coast, Nigeria, and so on
Pole mkuu,miye nilienda Kongwa kwenye Jimbo la aliyekuwa spika. Kurudi mpaka njia panda ya Mbade nilitumia boda, hakuna basi.Nimecheka sana ulivyopiga hasira kwa hoja ya kawaida ya ground – siasa ya kusafirisha mizigo kwenye mabasi halafu abiria wapande SGR au ndege usiku? Hiyo ni version yenu ya “technology ya taifa” labda.
Nilifika stendi kama abiria, nikaona hali halisi – siyo story za watu waliopo Twitter. Kama Dodoma ina usafiri mwingi wa usiku kama ulivyoandika, basi ni usafiri wa invisibility – hata CCTV zingeusaka.
Nilijiandaa, nikaenda interview, nikarudi kazini – sasa kama usiku mmoja wa giza na mabasi 3 umekukasirisha hivi, basi pole…
Sio kila anayesema ukweli ameikosea Dodoma – wengine tumeiona kwa macho, sio kwa screenshots
Pole sana mkuu – naona wote tumeonja ile Dodoma ya survival mode.Pole mkuu,miye nilienda Kongwa kwenye Jimbo la aliyekuwa spika. Kurudi mpaka njia panda ya Mbade nilitumia boda, hakuna basi.
Ushauri wa bure tu rudi facebook kabishane na MEMKWA wenzako ..kama kigezo chako cha kupima ubora wa mji ni kuangalia eti "kuchangamka usiku" basi huna tofauti na MEMKWA .Kwanza kabisa, sijawahi kutumia Facebook – so hiyo “rudi Facebook” ni attempt ya dhihaka isiyofika.
Pili, hoja za "mipangomiji, mapato ya halmashauri, uwepo wa mashirika ya kimataifa" ni nzuri kwenye presentations za maofisini – lakini ground reality ndio kipimo cha maisha ya jiji kwa mwananchi wa kawaida.
Mji usipooishi saa 24, usiku uwe giza, stendi iwe kama pori, usafiri usiwe reliable, watu wasiishi kwa amani nje ya ofisi – hayo yote yanafuta “maghorofa na miundombinu” unayoyapigia debe.
Mimi niliandika kutokana na nilichokiona kwa macho. Kama wewe unaijua Dodoma ya kwenye folders, na mimi naijua Dodoma ya usiku – survivor edition.
Hivi nyie mnaopenda kujitetea kwa barabara za lami ndo huwa mnaishi kwenye barabara hizo au mnaweka godoro stand ya Magufuli?Ushauri wa bure tu rudi facebook kabishane na MEMKWA wenzako ..kama kigezo chako cha kupima ubora wa mji ni kuangalia eti "kuchangamka usiku" basi huna tofauti na MEMKWA .
Hakuna mji wowote Tanzania uliopendelewa mtandao mpana wa barabara za lami kama Dodoma sasa tunakushangaa unapotaka kusema eti usafiri ni changamoto Dom😂😂.Yaani umeenda sikumoja tu kufanya interview alafu unakuja na cconclusion....Pathetic
Hoja yangu ni kuwa hizo nchi nilizotolea mfano miji yao ya kibiashara iko busy zaidi kuzidi miji ambayo wanatumia kama makao makuu ya serikali so siyo lazima Dodoma mlazimishe kwa kuilinganisha na Dar yaani wengi naona Dar mmeset ndo "standard" au kipimo cha kulinganisha na Dodoma. Burundi tu hapo mkoa wa Gitega ndo makao makuu ya nchi ilihali Bujumbura ndo imechangamka zaidiMkuu umeenda mbali, huwezi linganisha nchi hizo na Tz. Wale wako mbali.
kutoka hapo Nane Nane jichanganye uchukue boda tu twn had pale bungen wanatoza had 10k mchana huo mji nmesoma hapo ilaa siutaman hata kuusikia ...Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌
Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.
Lakini balaa lilianzia hapo!
Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.
Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:
Harakati za usiku
Mabasi ya safari za usiku
Taa za barabarani na stendi
Miundombinu ya usalama
Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."
Maswali yangu kwa wana JF:
1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?
2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?
Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Ndio ufahamu siyo kila mtu ni mkazi wa Dodoma!, Hivyo kuwa na utaratibu ni jambo Muhimu sana.Wenzake wanapandia gari Makole yeye unapuyanga kwenda 8 8 usiku.
Huku ni jamiiforums sio facebook humu watu wanabishana kwa hoja na facts sio porojo..umejoin JF una miezi miwili😂😂 tu jifunze kuelemika sio kubisha tu ilimradi na wewe uonekana unabishana wakati huna hoja wala content yoyote zaidi ya ushabiki na porojo.Hivi nyie mnaopenda kujitetea kwa barabara za lami ndo huwa mnaishi kwenye barabara hizo au mnaweka godoro stand ya Magufuli?
Mtu anauliza kuhusu hali ya usiku, usafiri, na uhai wa jiji baada ya saa mbili – wewe unaleta PowerPoint ya miundombinu. Huko ndo kufeli kuelewa hoja kwa staha.
Hata nikikaa siku moja tu Dodoma, kama ninatembea kwa miguu usiku, nikaona stendi ipo maporini, taa zipo ila watu hakuna, mabasi manne tu – hiyo ni experience halisi, sio fantasy ya mijadala ya ofisini.
Na ushauri wako wa “rudi Facebook na MEMKWA” ni dhaifu sana. Haujibu hoja, unajificha kwenye kejeli za kizamani. Siku nyingine ukiona mtu amegusa udhaifu, badala ya kukanusha kwa mikwara, jibu kwa hoja. Otherwise, hiyo keyboard yako inapiga makelele tu bila substance.
Ah, kumbe hoja zako zinapimwa kwa ID ya kujiunga JF, siyo yaliyosemwa? Hii nayo mpyaHuku ni jamiiforums sio facebook humu watu wanabishana kwa hoja na facts sio porojo..umejoin JF una miezi miwili😂😂 tu jifunze kuelemika sio kubisha tu ilimradi na wewe uonekana unabishana wakati huna hoja wala content yoyote zaidi ya ushabiki na porojo.
Kwa kukusaidia tu 👇
👉stendi ya mabasi nanenane Dodoma ni km 7 tu kutoka City Centre..stendi karibia zote za miji mikubwa nchi hii zipo nje ya mji.
👉Kutokana na ubora wa mipangomiji+miundombinu unafanya jiji la Dodoma kuwa na hali ya usalama wa juu ndiomana ni marachache sana kusikia matukio makubwa ya ujambazi Dom
Mkuu, Ulifika Dodoma au Hydom?Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌
Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.
Lakini balaa lilianzia hapo!
Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.
Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:
Harakati za usiku
Mabasi ya safari za usiku
Taa za barabarani na stendi
Miundombinu ya usalama
Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."
Maswali yangu kwa wana JF:
1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?
2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?
Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.