Makao Makuu ya CHADEMA yafurika, umati wafunga mtaa baada ya Mbowe kuachiwa huru

LEO KONYAGII ITANYWEKA SANA!NA MKEWE HANA KAZI LEO!
 

Mwenye tabia kama zako ndio huweza kuona arakeye. Wewe ni lazima uwe na mtazamo huo kwa sababu unadhani kila mtu anawaza kama wewe!!

Kwa taarifa tu - Mbowe na wenzake sio wahalifu, magaidi nk. Ni mahakama ndio ilikuwa na uwezo wa kuwaita hivo kwa hukumu na haikupata nafasi hiyo. Hao wanabaki raia safi kama wewe. Unaijua dhania ya โ€œinnocent until proven guiltyโ€?

Mtawafuata tena na wengine wengi kwa sababu haki sio kiongozi cha hulka na tabia za waoneaji!! Mnataka asishughulike na alichoanza nacho - ili iwe rahisi kwa ounevu wenu kushamiri. Ni ninyi ndio mtafanikiwa!!!
 
kwani nani anaogopa mahakama na magereza. Toa ujinga wewe MBOWE ni mzalendo namba 1 Tanzania na msimamo wake ni uleule
 
Baada ya mateso yote na safari ngumu alopitia katika kukuza jina na career yake mwishowe akakubali kuishia vile?

Nimemsikitikia sana Halima.
Halima huwa ananiuma kwenye roho yangu kama kidonda.. sikutegemea. Na mpaka leo moyo wangu unakataa kuamini
 
Nimejiuliza tu, baada ya haya Halima Mdee anajionaje?

Anajisikiaje?
Samahani mkuu 'Lusungo', baadhi yetu hatusomi vitu juu juu na kwenda zetu.

Huu mstari wako ulioweka hapa una maana gani? Fafanua kidogo tafadhari.
 
Halima huwa ananiuma kwenye roho yangu kama kidonda.. sikutegemea. Na mpaka leo moyo wangu unakataa kuamini
Sio peke yako, binafsi Halima, Zitto na Dr Slaa nilijitoleaga sana katika kuwapa taarifa nyeti zilizokuza umaarufu na career zao leo wakawa na price tag!! Hawa watu wananiuma sana ila ndo basi tena.
 
Samahani mkuu 'Lusungo', baadhi yetu hatusomi vitu juu juu na kwenda zetu.

Huu mstari wako ulioweka hapa una maana gani? Fafanua kidogo tafadhari.
Halima aliahidiwa Mbowe angefungwa na vikao vya baraza kuu visingefanyika.

Kilichopo ni kuwa Covid19 wanaliwa kichwa na chadema inapeleka wabunge wapya. Haya ni maagizo toka juu.
 
Nmepitwa! HALIMA MDEE na genge lake la Covid-19 wamefanyaje huko??
Inaelekea kuna habari za chini chini ambazo hazijawekwa bayana.

Labda tumwite mkuu Erythrocyte kidogo atupe mwanga juu ya hili. Hii itakuwa ni habari mpya, kama kweli ipo.
 
Mungu,Mbariki Mama Samia,Rais msikivu,Rais mwenye upendo,Rais anayependa raia wake.Mungu mpe uzima,afya,umri mrefu,Rais wetu,kipenzi cha wengi.Ni msikivu kama jina Lake,Samia(kwa kwa lugha za mashariki ya kati,msikivu)
 
Wakati kiongozi wa nchi akiona dhuluma juu ya Haki ni haramu, watu wajinga huona ni halali. Idiot!!
 
Jamhuri wajanja wamejua kuanzia leo ndio walikuwa wanaanza kuvukiwa nguo rasmi wakaona isiwe shida bora wamuache asepe, naamini katoka na wale watuhumiwa wenzake isije kuwa wao wamebaki kwasababu yoyote ile.
 
Acha upumbavu, kama unafikiri kuwa kwa Mbowe kuwekwa mahabusu Ndiyo njia ya kumnyamazisha, utakuwa na uharo kichwani.

Ikiwa tu, amekataa kuomba msamaha mliomlazimisha Hadi mkaomba poo atawezaje kunyamaza.

Ndiyo kwanza mmemwongezea umaarufu, ama kweli kama ninyi ndio washauri wa ccm basi utafiti wa TWAWEZA utaendelea kuwa hai kwa muda mrefu.
 
Halima aliahidiwa Mbowe angefungwa na vikao vya baraza kuu visingefanyika.

Kilichopo ni kuwa Covid19 wanaliwa kichwa na chadema inapeleka wabunge wapya. Haya ni maagizo toka juu.
Ahsante mkuu, kwa taarifa.

Aaah, lakini tafadhali punguza spidi, unakwenda haraka mno kiasi kwamba akili inashindwa ku-process majibu yako haya.

"Maagizo toka juu. Chadema inapeleka wabunge wapya"?

Inamaana CHADEMA sasa wameukubali "UCHAFUZI" uliofanywa na Magufuli 2020? Mbona hii itakuwa kama movie ya kihindi?

Nitastaajabu sana kama haya uliyoandika hapa ndiyo yatakayotokea.
 
Hawajakubali uchafuzi, maza ametaka reconciliation. Hakuna namna zaidi ya chama kujipanga kwaajili ya 2025.
 
Hawajakubali uchafuzi, maza ametaka reconciliation. Hakuna namna zaidi ya chama kujipanga kwaajili ya 2025.
CHADEMA ni lazima wawe waangalifu sana toka hapa kwenda mbele wasije wakaashia kuwa kama NCCR, CUF na kile cha Mrema.

Sisemi wakatae 'reconciliation', lakini ni lazima wawe waangalifu sana wakati huu. Kupeleka wabunge kwenye bunge batili si busara hata mara moja. Na kukataa hilo sio kukataa 'reconciliation', tafadhari nielewe hivyo.
 
Kwa bunge la sasa ni muhimu CHADEMA ikawa na sauti kwa niaba ya wananchi kuliko kususa tukawaacha wananchi wasiwe na sauti za kuwasemea.

Mpaka sasa utakua umepata picha ni madudu mangapi yamepita kwakua tu kuna sauti moja ya CCM bungeni.

To me naona tsa good move.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ