Makato ya Mshahara kwa Daktari mpya Serikalini, bado tuna safari ndefu sana

Makato ya Mshahara kwa Daktari mpya Serikalini, bado tuna safari ndefu sana

Kuna mtu anaingia bungeni anasinzia tu, akishtuka anagonga gonga meza kikao kikiisha anapokea posho, jioni unamkuta rainbow au bambalaga, then mwisho wa mwezi anakunja mara 10 ya hicho kipato. Amaa kweli dunia uwanja wa fujo
Halafu Elimu yake ni ya darasa la saba.

Sifa za mbunge anatakiwa ajue kusoma na kuandika na awe na akili timamu
 
Inategemea hiyo ajira, uanlipwa ngapi, sasa Mimi napokea 7M net, kila mwezi, na save 5M, kwa miaka 15 nitakuwa na 900M!kama ni utumwa Wacha ni we mtumwa tu!
Hata ukijiajiri, lazima Uwe mtumwa wa wateja,
Motivation speaker, hivi unajuwa hata school fees English medium ni bei gani?

Wajinga wa mitandaoni ndio wanaweza kuandika ujinga kama huu, si ajabu ukaanza kilimo cha matikiti WhatsApp.
 
Nilivyokuwa nafanya kazi zakuajiriwa ni kodi na nssf tu ndio wanakata bima za afya tunalipiwa. Sasa nyie serikali inakuaje hawalipii
Dada hujui sheria za kazi vizuri. Mwajiri kukulipia bima hiyo alikupa as a fringe benefit, sio haki.
Kwa serikalini, bima unalipia asilimia 6 inaweza kuwa mwajiri 3 nawewe 3 au zote 6 ulipe mwenyewe.
 
Hivi tungekuwa china ya mkoloni mzungu, mshahara ungekuwa sh. Ngapi? Na huduma za jamii zingekuwaje? Mimi bado naota hizo ndoto je tungekuwa wapi? Kujitawala wenyewe bado sana. Mfanyakazi ni injini ya taifa, mfanyakazi akiwa na furaha taifa linafuraha.

Ningependekeza kima cha chini kiwe sh.300,000 hakuna kodi hapo. Mtu alipe kodi rafiki zaidi ya huo mshahara.
 
Kwa makadirio, mshahara wa daktari Serikalini basic ni 1,480,000

HESLB wanakata 222,000
74000 ya PSSSF
kodi ni 290,580
bima ya afya 44,400

Unabaki na 849,020

Toa kodi ya nyumba, bill ya maji, umeme, usafiri na chakula halafu niambie unabaki na sh ngapi?
Lakini wanajenga maghorofa mbona, hela wanatoa wapi???
 
Back
Top Bottom