Kitendo cha kujenga kijijini alipozaliwa ni Ishara kwamba tulipozaliwa ni muhimu kuliko tulipokulia au tunapigia mishemishe.
Wote tungejenga makwetu na kupaendeleza leo tusingekuwa na vijiji tungekuwa na mitaa nchi nzima
Wapo viongozi hapa nchini hata nyumba ya kawaida tu kwao hawana. Mawaziri wengi vijijini kwao hakuna nyumba, wabunge ndo usiseme bila kusahau makatibu wakuu na wakurugenzi .
Tungekuwa na sera yakujenga vijijini hata umeme na maji, barabara na huduma za afya isingekuwa shida
Ile nyumba ya Mbowe haikosi umeme, maji yapo, hospital lazima ipo karibu nk
Ila vyote hivyo vimepelekwa kwa sababu watu wamewekeza
Sisi watu wa kanda ya ziwa tutaendelea kulalamika ila ukweli lazima tukubali vijijini tulipotoka.......JPM alifanya kile mwanasiasa anapaswa kufanya kwao......let us think about our home villages