Makonda alitoa wapi zaidi ya Sh. Bilioni moja kujenga nyumba binafsi. Je, mshahara wa Mkuu wa Mkoa kwa miaka 3 unatosha?

Makonda alitoa wapi zaidi ya Sh. Bilioni moja kujenga nyumba binafsi. Je, mshahara wa Mkuu wa Mkoa kwa miaka 3 unatosha?

Makonda alitumia Madaraka yake vibaya sana ya ukuu wa mkoa, Anapaswa kufunguliwa mashtaka ya uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha

Ni vyema ikafanyika tathmini ya Mali zake Kimehasabu na kodi alizolipa TRA pamoja na Chanzo chake halisi cha mshahara vilinganishwe

Makonda na vijana baadhi walijigeuza wafalme wakati wa utawala wa giza, Walipora chochote na kutisha wafanyabiashara

Mishahara ya wakuu wa Mikoa inajulikana kisheria na sio siri kabisa, Hakuna mkuu wa mkoa anayelipwa pesa kufikia Milioni kumi yaani kwa mwaka ni Milioni mia moja ishirini, Na kwa miaka mitano ni Milioni mia sita

Makonda hajafanya ukuu wa mkoa kwa miaka mitano, Na hata angefanya hiyo kazi hakuna mkuu wa mkoa analipwa mshahara wa Milioni kumi

Kimehasabu Makonda hana uwezo wa Kumiliki Mali alizokuwa nazo kuanzia magari ya kupora ya kifahari na nyumba za kupora za wafanyabiashara

Karma ni mbaya sana, Makonda alilalamikiwa hapa JF kuwa anajenga hekalu huko Mwanza kwao, Anamiliki magari ya watu kwa kutapeli na vitisho vikubwa

Ghorofa linaloonekana kwa sasa analosema la kwake, Kiuhalisia hana uwezo huo hata kidogo wa Kumiliki kwa kazi yake ya ukuu wa Mikoa chini ya miaka minne

Anajitapa eti mdogo wake baada ya kumaliza kusimamia ghorofa lake Mwanza akaanza kusimamia ghorofa alilopora kwa mfanyabiashara GSM lenye thamani ya zaidi ya bilioni moja

Ni muda muafaka kwa Makonda kurudisha Mali kwa wahusika,

Kazi iendelee
Ungetupia picha la hilo ekalu mkuu.

Sent from my SM-A037G using JamiiForums mobile app
 
Hii ndo ile ya kula kwa urefu wa kamba anayosisitiza mama kwa sauti ya upoooleee kabisa, jipimieni......sasa sisi ambao hatuna vyeo, huwezi kupata mafungu ya kujipimia kama akina bashite, unabaki kusulubiwa na maafisa utumishi wakati unapambana upande walau cheo na mshahara upate kaunafuu kidogo......nchi ngumu hii.
 
Hapa simtetei Makonda ni kweli ukiwa mtumishi wa serikali ni lazima uoneshe mali zako na ku declare kabla na baada je vile viapo ni kama fashion tu hawana meno. Lakini angepewa nafasi ya kujieleza bila kumhukumu kwamba kwa mshahara hana uwezo ni kweli lakini labda alikuwa na vyanzo vingine au labda alichukuwa mkopo hatuyajui haya ila tukianza kuulizana basi sio Makonda tu wengi inabidi waulizwe pamoja hata na GSM ndio tajiri lakini je biashara zake inaendana na anayoyafanya, wengi sana inabidi tujieleze tumefikaje hapa tulipo.
GSM siyo mtumishi wa uma, tumeanza na Makonda kwakuwa alikuwa mtumishi wa uma na mapato yake (kama mtumishi) yanafahamika.
 
Jinai haina mwisho.Mama ni mpita njia
Huyu Mtu kila awamu analindwa
Alimpiga warioba utawala wa awamu ya 4 ukamzawadia ukuu wa wilaya
Utawala wa awamu ya 5 ukamzawadia ukuu wa mkoa
Utawala wa awamu ya 6 , ukampa kazi maalum serikalini
Hata hilo eneo lenyewe alilipata awamu ya 4
[emoji116]
20220311_112153.jpg
 
Kwenye kuwabambika matajiri kesi za madawa alipata pesa nyingi.
Pia GSM ilibidi wajisalimishe kwa makonda Ili wasifukuzwe nchini. Walilazimika kulipa kodi kwa makonda Ili wapumue.
Hiyo na GSM wanajuana kitambo toka awamu ya 4 na ndipo walipopeana Hilo eneo. Ugomvi wa ndugu huo
20220311_112153.jpg
 
Hiyo na GSM wanajuana kitambo toka awamu ya 4 na ndipo walipopeana Hilo eneo. Ugomvi wa ndugu huo
View attachment 2146713
Mbona hata riziwani,fred Lowasa wanajuana tangu awamu ya 4 lakini awamu ya tano akawatenda.
Bashite alidanganywa na wazee wa juju kwamba jiwe akitoka madarakani 2045 ataingia yeye.
Akipigiwa chapuo na pascal mayalla akajawa kiburi akiamini ndoto kutumia
 
GSM siyo mtumishi wa uma, tumeanza na Makonda kwakuwa alikuwa mtumishi wa uma na mapato yake (kama mtumishi) yanafahamika.
Ndio maana nimesema ni yeye kusema kapata wapi pesa yeye hakuwa mtumishi wa umma ila alikuwa ameteuliwa kwenye nafasi ya kisiasa. Unataka kuniambia unaweza kwenda leo kummuliza Kikwete au kina Kinana utajiri wao wametoa wapi wakati walikuwa watumishi tu. GSM ndio anafanya biashara lakini hata mfanya biashara anaweza kutakiwa kuonesha mzunguko wake wa pesa kama unaendana na utajiri wake. Kuna watu wanajificha nyuma ya biashara kufanya yasiyotakiwa. Kama GSM alitoa nyumba ile kwa JPM alikuwa anatoa kama nini? zawadi au rushwa? Hili litabainisha mengi tusiyoyajuwa je wafanya biashara wanatoa hizi mali ili wapate nini? hawa wote lazima waongee nini hasa kiko nyuma ya pazia. Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wahalifu. Unamjengea nyumba kiongozi? kwa lipi
 
Kuhusu kupora lipo wazi, Ila nazungumzka Hilo kiwanja Cha regent estate ni tokea 2013 aliuziwa
2013 alikuwa anachoma mkaa mbezi kimara alipata wapi pesa za kununua kiwanja regent.
 
Mbona hata riziwani,fred Lowasa wanajuana tangu awamu ya 4 lakini awamu ya tano akawatenda.
Bashite alidanganywa na wazee wa juju kwamba jiwe akitoka madarakani 2045 ataingia yeye.
Akipigiwa chapuo na pascal mayalla akajawa kiburi akiamini ndoto kutumia
Nilichomaanisha hao waliuziana hiko kiwanja toka zamani kabla hata makonda hajawa mkuu wa wilaya.
Hivyo Kuna kitu kilikua kinawaunganisha hadi kufikia kuuuziana huko.
 
Makonda alitumia Madaraka yake vibaya sana ya ukuu wa mkoa, Anapaswa kufunguliwa mashtaka ya uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha

Ni vyema ikafanyika tathmini ya Mali zake Kimehasabu na kodi alizolipa TRA pamoja na Chanzo chake halisi cha mshahara vilinganishwe

Makonda na vijana baadhi walijigeuza wafalme wakati wa utawala wa giza, Walipora chochote na kutisha wafanyabiashara

Mishahara ya wakuu wa Mikoa inajulikana kisheria na sio siri kabisa, Hakuna mkuu wa mkoa anayelipwa pesa kufikia Milioni kumi yaani kwa mwaka ni Milioni mia moja ishirini, Na kwa miaka mitano ni Milioni mia sita

Makonda hajafanya ukuu wa mkoa kwa miaka mitano, Na hata angefanya hiyo kazi hakuna mkuu wa mkoa analipwa mshahara wa Milioni kumi

Kimehasabu Makonda hana uwezo wa Kumiliki Mali alizokuwa nazo kuanzia magari ya kupora ya kifahari na nyumba za kupora za wafanyabiashara

Karma ni mbaya sana, Makonda alilalamikiwa hapa JF kuwa anajenga hekalu huko Mwanza kwao, Anamiliki magari ya watu kwa kutapeli na vitisho vikubwa

Ghorofa linaloonekana kwa sasa analosema la kwake, Kiuhalisia hana uwezo huo hata kidogo wa Kumiliki kwa kazi yake ya ukuu wa Mikoa chini ya miaka minne

Anajitapa eti mdogo wake baada ya kumaliza kusimamia ghorofa lake Mwanza akaanza kusimamia ghorofa alilopora kwa mfanyabiashara GSM lenye thamani ya zaidi ya bilioni moja

Ni muda muafaka kwa Makonda kurudisha Mali kwa wahusika,

Kazi iendelee
Ofcoz hakuna mtanzania mtumishi wa umma aliyeweza kujenga nyumba kwa pesa yake ya mshahara wachache wamepata mkopo bank Ila wengi wamejenga kwa pesa za wizi na rushwa huu ndio ukweli mtupu.
 
2013 alikuwa anachoma mkaa mbezi kimara alipata wapi pesa za kununua kiwanja regent.
Bashite huyuhuyu 2013 awe anachoma mkaa? Wengi inaelekea hamjui kabla ya kumpiga warioba na kupata uteuzi alikuwa nani.
 
Back
Top Bottom