Makonda alizaliwa kuwa Kiongozi, ni aina ya watu adimu sana kwenye Uongozi wa Juu

Makonda alizaliwa kuwa Kiongozi, ni aina ya watu adimu sana kwenye Uongozi wa Juu

Huyu ni Makonda mwenyewe kaanzisha huu Uzi au mpambe wake katumwa kutusumbua humu, kwa kuangalia picha tu aliyoweka ni Ile anaamini imetokelezea vizuri. Koti tai nk. Picha ya kupeleka ukweni. Ukisoma Cuba ya Buza kwa Mpalanger vitu vidogo havisumbui!

Sasa boss Makonda ni kweli una sifa ya uongozi una sauti yenye mamlaka na mwangwi mkubwa japo samahani mimi binafsi huwa siwakubali watu ambao hawakusoma ulaya na marekani kuna vitu hawana ila naomba please 🙏 chonde chonde mfikishie Mh Rais, Dr Samia ujumbe huu hapa chini. Ni muhimu mno mno!! Please mfikishie kama ulivyo, please mfikishie Leo!

Bimkubwa Samia naomba tusaidie mambo mawili tu SGR Dar-Mwanza/Kigoma iishe haraka ndani ya utawala wako na Nyerere Dam ianze uzalishaji haraka basi nchi itafunguka yenyewe bila kutumia mabango yako nasi tutakuimba na kukuandika kwenye vitabu, Bimkubwa tafadhali naomba achana na mambo mengine hutaweza sababu watu maskini huzaa sana bila mpango na tunaongezeka kila kukicha kwa mamilioni, hata ujenge shule milioni hazitoshi na hata ujenge hospital milioni kila siku hazitatosha ila ukijenga reli ya umeme na mabwawa ya kuzalisha umeme nakuhakikishia tutatoboa! ( Kwa wasomi tu, read Malthus theory of Population).

Nchi za ulaya ni reli na umeme tu vimeleta mapinduzi ya viwanda na utajiri na sio nimesikia bali kwa kuishi na kuona kwa macho mtu unakaa Dar kazini ni Gairo na huwazi, hizo vitu mbili zitaleta kila ambacho nchi inataka kama wawekezaji , barabara, hospital, shule, na viwanda. Hii nimesoma darasani ulaya na kuyaishi hayo maisha. Lazima Wana sisiemu tumsaidie Bimkubwa.
Jumapili njema wapendwa!
 
Back
Top Bottom