Mimi kama mwanasaikolojia ni kwamba mkirogwa mka mpa Uongozi Makonda ni typical Magufuli ila Sasa shida ya Viongozi aina ya Makonda ni mjiandae kuwa dikteta Kwa sababu hataki kukosolewa na anapenda sifa na majivuno na wakurypukaji.Hawapendi kupata kitu Kwa undani.
Mbaya zaidi mtaishia kuwa maskini na Biashara mnazoona zinafufuia Leo Watoto wenu wanapata kazi zitakimbia zote Kwa sababu itafika pointi mtaanza kuitwa majizi,wezi na ujinga mwingine kama huo.
Wale mnaoitwa Wanyonge mtazidi kuwa maskini huku mkijifariji kwamba Watumishi Wana nidhamu 🤣🤣
Wafanyabiashara ni wajanja wanajua kunusa mkianza mchakato wa kunteua utaona fasta wataacha au kupunguza uwekezaji na kuhamishia mitaji Kwa jirani Ili nyie Wanyonge mpige makofi na vigelegele vizuri Kwa Makonda.
Saizi Wanamuogopa Makonda Kwa sababu amepewa Nguvu na Samia na hakuna wa kumgusa.
Mimi binafsi watu dizaini ya Makonda napenda wawe wanaishia level ya PM Kwa usalama wao maana Dunia haiwahitaji watu wenye msimamo mkali na wasio na emotional balance.