Makonda anaeneza ukabila? Ni nini kinamfanya aongee kisukuma huko usukumani?


..Hate speech zipo sana hapa JF.

..Na huwa zinaelekezwa kwa jamii fulani sitaitaja leo.
 
Ningekuwa na Uwezo wa Kuongea Lugha zote ningeziongea popote iwapo muhusika atanielewa..., Lugha kazi yake ni Mawasiliano tu..., Kuogopa kuongea lugha fulani au kutenga wasiojua hio lugha ndio ukabila ila sio kuiongea... Na Politically inaonekana unajali (you speak the same language) kama watu wa Ughaibuni wanavyosema....

Na ingawa sijamsikiliza lakini sidhani kama alifanya hivyo mwanzo mwisho (nadhani alichombeza tu) kama alifanya hivyo mwanzo mwisho hence kutenga majority nchini ambao hawakumuelewa basi atakuwa hakujitendea haki (ni kama kumpigia mbuzi gitaa)
 
Usimsikilize ama na ww ongea Lugha yako
 
Umelogwa siyo bure
 
Unateseka ukiwa wapi goroko wewe?
 
Makabila ambayo wanapenda kuongea vilugha
Wasukuma
Wahaya
Wakurya
Wanyakyusa
 
Tanzania ilijivua nira za ukabila miaka mingi iliyopita.
Hata hivyo kwa sababu ya siasa za ubinafsi unaosababishwa na fikra zenye uoni mfupi, ukabila bado unajijenga.
Tusipochukua tahadhari, tukizingatia kuwa hata shule na vyuo ni vya kata hadi kanda, hii changamoto itaongezeka.
Kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya nne, fikra za ukabila zilikuwa kidogo au chini chini. Mabadiliko makubwa ya viongozi serikalini kwenye awamu ya tano ndiyo yaliyoibua kwa wingi hisia za ukabila na hata kutamkwa wazi wazi kwenye majukwaa ya kisiasa.
Tutahitaji viongozi majasiri, wasio waoga, wanaoweza kusimama wenyewe kudhibiti fikra za ukabila.
Mwanasiasa kuegemea kwenye ukabila au dini ni uthibitisho wa uoga na unafiki.
 
Yupo kwenye kampeni ya 2025, ila utaskia CHADEMA ya wachagga wakati hata huko kwao[Uchagani] hawafanyagi mikutano.
 

Tulieni dawa iwaingie
 
Tulieni dawa iwaingie
Hakuna habari za dawa. Tunahitaji kujenga jamii na taifa la watu wenye fikra zinazoweza kujenga hoja au kujibu hoja kwa facts.
Dawa ni hoja zenye mantiki na weledi, mipasho ya wajinga na wapuuzi tuwaachie wenyewe.
 
Hii mimba ya Makonda uliyo nayo itakutesa sana hadi ufikishe miezi 9.
 
Nimerudia kusoma tena, kumbe wewe mpumbavu sana eti kisukuma kibaya na ungeona aibu kukitumia karne hii!
Tanzania tuna makabila 120+ Sasa aibu na kabila baya ni kisukuma? Pumbavu sana wewe.
 
Tz hatuwazi hayo mambo,hata Muha akiongea kiswahili anakua na rafuzi kiha,but Wala si kitu Tz ukabila si jambo la mjadala kwetu.Relax nawew kusanya watu ongea kikwenu huta pigwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…